KIJITOSAMAKI
Member
- Sep 2, 2020
- 29
- 16
- Thread starter
-
- #41
Macho ya wenye dunia yote yako Tanzania hiyo October 28 ndugu. Subiri uone CCM anavyoshikishwa adabu
Nichukie nini, mimi nimekupa kitu na box. Hiyo tarehe 28 unayotambia hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Sio hata tukinyang' anywa ushindi, maana ni lazima ushindi uporwe, kwani ccm imekata moto kwenye ushindani. Hilo suala la kuandamana kaa ukiomba ukondoo uendelee, kinyume na hapo jiandae kutapika hirizi. Muhuni mkubwa ww.
Mkuu tindo wewe ni mtu ambaye sikutegemea ni wa kukata tamaa mapema hivyo. Ati wadai Sio hata tukinyang' anywa ushindi, maana ni lazima ushindi uporwe. Yawezekana nawe wewe ni mmoja wa waliokata tamaa ya ushindi baada ya kushuhudia Mgombea wa chama badala ya kunadi Sera anaporomosha matusi na kutishia vurugu, kwenye kampeni zake.
Kuna dalili za kukata tamaa hadi, hata wewe Mkuu tindo kuanza kutoa sababu za kushindwa vibaya. Ati Hiyo tarehe 28 unayotambia hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Mjinga ni mmoja wa wale wanaoamini nyomi kwenye kampeni ndiyo kura za ushindi.
Mjinga ni yule anayeamini matusi, kejeli, kebehi, na kudharilisha mgombea mwingine ni turufu au mtaji wa kisiasa kupata kura, na akashangiliwa.
Mjinga ni yule anayehamasisha vurugu asipotangazwa mshindi kwa kuaminisha wapiga kura, kwenye kampeni, kuwa yeye tayari amekwisha kuwa mshindi, na wakamshangilia.
Mjinga ni yule anayeamini yeye ni bora kuliko Mtanzania yeyote na wapumbavu na malofa wakamshangilia.
Sitajarii Mkuu tindo, wala siamini kuwa wewe ni mmoja wa hao!
Mkuu tindo najiuliza, kwa sauti kubwa, WanaCHADEMA humu JF na nchini kote hali itakuwaje chama kutelemka hadhi ya Chama Kikuu cha Upinzani?
Wenye kujitambua (M/kiti wa chama, Katibu Mkuu na Wajumbe wa Kamati Kuu) wameamua kumwacha Mgombea wao wa Urais ajichimbie kaburi lake mwenyewe. Kama ni viongozi makini ni wakati wa kuweka nguvu kwa wabunge na madiwani, kwenye maeneo ambayo bado wana angalau nguvu kidogo ya kisiasa. Wasipofanya hivyo, nina uhakika (100%) CHADEMA itaanguka vibaya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Inatosha kama una amini hujakata tamaa. Hivyo basi, hamasisha, wanaounga mkono upande wako watumie uhuru na haki yao kupiga kura kwa amani.Sioni ukataji tamaa wangu ni upi hapo.
Inatosha kama una amini hujakata tamaa. Hivyo basi, hamasisha, wanaounga mkono upande wako watumie uhuru na haki yao kupiga kura kwa amani.
Lugha ya kuhamasisha vurugu kuwa tayari mgombea huyo ni mshindi, hata hatua ya kupiga kura bado, si dalili za amani.
Kwasababu ya upovu na uroho,unashindaje wakati huna tume huru,huna katiba ya Warioba?Upinzani hawana uwezo wa kuishinda CCM hata miaka 100 ipite
Na iwe hivyo.Acha upotoshaji wa kijinga, hakuna popote anaposema yeye ni mshindi, na atalazimisha kutangazwa mshindi, bali amesema iwapo atashinda na kuachwa kutangazwa mshindi hatamuachia Mungu.
Na iwe hivyo.
Kama ana uhakika wa ushindi iweje ahamasishe watu kuingia barabarani?
Chama kimegeuzwa mali ya mtu na washkaji zake. Watakula jeuri yao, Oct 28.Mzee Mtei na marehemu Bob Makani walikuwa wanajua strategies unazoongea sana na ndiyo maana CHADEMA ikapanda hadi kuwa ilivyo leo, ila sasa hivi inaelekea kifo cha mende.