Mkuu
tindo wewe ni mtu ambaye sikutegemea ni wa kukata tamaa mapema hivyo. Ati wadai
Sio hata tukinyang' anywa ushindi, maana ni lazima ushindi uporwe. Yawezekana nawe wewe ni mmoja wa waliokata tamaa ya ushindi baada ya kushuhudia Mgombea wa chama badala ya kunadi Sera anaporomosha matusi na kutishia vurugu, kwenye kampeni zake.
Kuna dalili za kukata tamaa hadi, hata wewe Mkuu
tindo kuanza kutoa sababu za kushindwa vibaya. Ati
Hiyo tarehe 28 unayotambia hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Mjinga ni mmoja wa wale wanaoamini nyomi kwenye kampeni ndiyo kura za ushindi.
Mjinga ni yule anayeamini matusi, kejeli, kebehi, na kudharilisha mgombea mwingine ni turufu au mtaji wa kisiasa kupata kura, na akashangiliwa.
Mjinga ni yule anayehamasisha vurugu asipotangazwa mshindi kwa kuaminisha wapiga kura, kwenye kampeni, kuwa yeye tayari amekwisha kuwa mshindi, na wakamshangilia.
Mjinga ni yule anayeamini yeye ni bora kuliko Mtanzania yeyote na wapumbavu na malofa wakamshangilia.
Sitajarii Mkuu
tindo, wala siamini kuwa wewe ni mmoja wa hao!
Mkuu
tindo najiuliza, kwa sauti kubwa, WanaCHADEMA humu JF na nchini kote hali itakuwaje chama kutelemka hadhi ya Chama Kikuu cha Upinzani?
Wenye kujitambua (M/kiti wa chama, Katibu Mkuu na Wajumbe wa Kamati Kuu) wameamua kumwacha Mgombea wao wa Urais ajichimbie kaburi lake mwenyewe. Kama ni viongozi makini ni wakati wa kuweka nguvu kwa wabunge na madiwani, kwenye maeneo ambayo bado wana angalau nguvu kidogo ya kisiasa. Wasipofanya hivyo, nina uhakika (100%) CHADEMA itaanguka vibaya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.