Uchaguzi 2020 CHADEMA inahitaji political strategists kuishinda CCM


Ndg yangu nataka nichangie kwenye pointing ya 4 tu. Mtoa mada hakusema vyama vya upinzani visishiriki uchaguzi huu. Alisema wasingeweka mgombea kwenye nafasi ya rais tu. Maanake nafasi nyingine za ubunge na udiwani waweke. Kuhusu kuangalia kura za rais kutoa wabunge wa viti maalum, huku ndo kuangalia maslahi ya muda mfupi na kuacha kupanga mipango ya muda mrefu. Katika siasa wakati mwingine lazima kukubali kupoteza maslahi fulani ya muda mfupi kwa ajili ya vitu vikubwa zaidi. Mtoa mada nimemkubali pointi zake. Na wewe hongera kwa kuchangia lakini kwenye ukweli ni muhimu tukubali. Mimi sijawahi kupigia kura ccm lkn safari hii namchagua magufuli tu kwenye Urais. Kwa wabunge na madiwani bado napima.
 

Niambie kutokuweka mgombea wa urais kuna athiri vipi malengo ya muda mrefu.
 

Kwa mawazo yako CDM haina strategists? Kama hiyo ndiyo update mpya ya kina katawi - ujue makopo na kuyarokota tayari kuna wahusu.

Kumwachia jiwe hadi 2025 siyo option. Huyu kama CCM ina strategist yeyote wa maana alipashwa kushauri hilo. Jiwe kwa kushindwa kutenda na hata kushindwa kusimama na haki anachukiwa kuliko maelezo.

Jiwe hafai. Hana unyonge wowote ati kuna haki yoyote apewe Kwa lipi la maana alilofanya?
 
Mtoa mada ameeleza vizuri athari za kuweka mgombea kwenye uchaguzi huu. Labda urudie kuisoma uielewe.

Mamba anashauri watu kuvuka mto salama. Hayo kama siyo maajabu ya Firauni basi hakuna mengine.
 
Tatizo ni Vyombo vya kutoa Haki kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Vyombo vya ulinzi na Usalama ambavyo kwa kila mbinu vinaisaidia CCM kubaki madarakani.HAPA NDIPO PENYE TATIZO!
Kwa hiyo hata kama ingekuwa mwaka 2025,2035,2045,nk uwezekano wa Chama cha Upinzani kuitoa CCM madarakani kwa mazingira haya haupo!
Hili litamalizwa mwaka ambao Wananchi watakapofikia ukomo wa Uvumilivu kisha waingie mabarabarani kuleta Mapinduzi yasiyotarajiwa.
 
Tatizo ccm ina watu wenye kukipenda chama kama chama pamoja na mapungufu yake ila upinzani kuna watu wenye kuchukia huu utawala wa ccm.

Huwa nafikiri kuwa kama kweli ccm imechokwa na watu na kuchukiwa na ipo madarakani kwa nguvu ya dola tu,basi sidhani kama ingewezekana hata kuwasomba watu kwenye malori(watu waliyoichoka ccm na huichukia) na kuwapeleka kwenye kampeni za ccm au kwamba hao watu wejipeleke wenyewe kwenye mikutano ya ccm kuangalia wasanii,hao watu watakuwa hawako serious.
 
Muda wa kuandika ujinga unaupata wapi?
 
Dola (Majeshi) yakae pembeni uone kama CCM itasalia madarakani kupitia boksi la kura

Hujui mambo ya National Security and Politics ndo maana unasema Majeshi likae pembeni. Anayedhani Majeshi yakae pembeni kwenye politics anajidanganya. Haipo popote duniani. Majeshi ni sehemu ya politics za nchi husika. Tofauti ni kwamba hawagombei nafasi za kisiasa tu basi.
 
Chadema kikwazo cha kutoshinda ni tumeccm hii tumefake kamwe haiwezekani kuwatangaza Chadema kama washindi. Ccm imechokwa Nchi nzima.

CCM ikishindwa Ni bora kuongozwa na CUF sio CDM. CDM ni vibaraka wakubwa, wezi na watakuwa wasaliti wa nchi hii. Huwezi kukabidhi nchi kwa watu wanoonekana dhahiri watapoteza maslahi ya taifa. Watu wanaopanga kuweka rehani madini ili kupata pesa za kuendesha nchi, akili zao zimefilisika. Watauza nchi kwa Wachina mara moja halafu wachukue chao waende Ughaibuni. Hakuna sera ya maana waliyoitangaza hadi sasa. Sera yao ni matusi, kejeli, vurugu. Hawana haja na maendeleo ya nchi, tungewaona kwenye maendeleo ya Chama chao kwa matumizi mazuri ya ruzuku.
 

Akili yako ni dhaifu sana. Hiyo njia nakuhakikisha haitawafanikisha kwa lolote.
 
Povu zitoooo lakini wakati huo huo huyo mwizi aliyekwapua 2.7 trillions kama ilivyoripotiwa kwenye ripoti za CAG Assad na CAG Kichere ndiye unamuona mzalendo!!! Wapuuzi kama wewe ni tatizo kubwa Nchini

 
Umemaliza mkuu, you nailed it. Hakuna cha strategy wala bibi yake strategy wakati mwenzio tegemeo lake kuu ni kuiba ushindi through NEC, polisi and other organs... Just imagine mkakati wa kuengua wagombea was full of figisu halafu useme Kuna strategies??
 
Ilani nzima ipo humu mitandaoni in pdf umeshaipakua na kuisoma kwa utulivu au unapanua domo kama mamba??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…