Yaani hizi hoja zako zimenifanya nicheke ile mbaya, eti upinzani ukitaka kuitoa ccm imuunge mkono Magufuli, halafu 2025 ndio ichukue nchi. Umesema upinzani lakini umeitaja cdm tu. Sasa ngoja tuone kwenye uhalisia wa hizi hoja zako.
- UDP na TLP wamemuunga mkono Magufuli, hivyo tutarajie kuwa 2025 watachukua nchi kwa hii nadharia yako? Kwa taarifa yako Magufuli angeachiwa safari hii apite bila kupingwa angejiongezea muda wa kukaa madarakani. Wapinzani kushiriki uchaguzi huu, tena wakiwa wamefanyiwa kila aina ya ukatili, na kuendelea kupata watu wengi kwenye mikutano yao, ni wazi kuwa hakuna uwezekano tena wa nchi hii kuendelea kuongozwa tu na ccm kwa kura halali.
- Kwa taarifa yako ujenzi wa miundombinu ni tabia binafsi ya Magufuli na sio ccm. Hivyo hata akitangazwa mshindi sio akishinda bado ataendelea na hiyo miundombinu. Mpaka sasa tayari Magufuli ana miradi miwili mikubwa ya 15t+, na yote analazimisha amalize ndani ya muda wake halali wa kisheria, iwapo hatachezea katiba. Mpaka sasa hakuna mradi hata mmoja uliofikia robo ya kukamilika na tayari wananchi wameshaumia sana. Hivyo kama ni kutua hela hajatoa hata nusu ya pesa yaani 7t. Hivyo anatakiwa ndani ya hii miaka mitano lazima apate 8-10t, ni wapi atapata hizo hela, achia mbali mahitaji mengine? Kwa vyovyote kufika hiyo 2025 bado ccm itazidi kuwa kwenye wakati mgumu maana kupata hizi hela za kumalizia hiyo miradi ni kiama.
- Hoja ya cdm kuchukua nchi ikiwa imejaa miundombinu ya kila namna, na kuwa rahisi kuendesha nchi kwa kujali maslahi ya mtu mmoja mmoja. Hoja hii ni kiini macho, tazama deni la taifa mpaka sasa ni kiasi gani toka awamu hii iingie madarakani. Ni wazi serikali sasa inakopa sana, huku terms za mikopo ikiwa inafahamika na mtu mmoja na genge lake. Katika mazingira hayo, una uhakika gani wa kuendesha nchi kirahisi ukiwa na madeni mazito hivyo? Kuhusu hoja ya Corona hapa ndio nimeona hujui unaoongea nini, kwani Corona Ni ugonjwa wa kudumu mpaka useme wazungu watalazimisha nchi iwekwe lockdown? Halafu acha upotoshaji wa kijinga, ni nani anataka kuchukua nchi ili apewe maelekezo na wazungu? Hii ni dhahiri uko na hoja za kuokoteza.
- Kwamba sasa hivi cdm imeshiriki uchaguzi huu na haitashinda hata kidogo. Kwani kushiriki ni lazima ushinde? Ingekuwa kushiriki kwenye ushindani wowote lazima ushinde, basi ligi kuu ya nchi yetu ingekuwa na simba na yanga tu maana ndio wenye uwezo wa dhahiri kushinda ligi. Halafu uchaguzi mkuu sio urais tu, bali kuna wabunge na madiwani, na kura za urais hutoa wabunge wa viti maalum. Kama miaka hii mitano tuliaminishwa kuwa ccm imeua upinzani, na kinachoonekana ni tofauti, ni kipi kitafanya sasa na hiyo 2025 isiwe rahisi kuitoa ccm? Kwa taarifa yako cdm ingeingia mkenge wa huu ushauri wako fake, kufika 2025 katiba ingekuwa imeshabadilishwa na ingehalalishwa kuwa upinzani umekufa.
Ndg yangu nataka nichangie kwenye pointing ya 4 tu. Mtoa mada hakusema vyama vya upinzani visishiriki uchaguzi huu. Alisema wasingeweka mgombea kwenye nafasi ya rais tu. Maanake nafasi nyingine za ubunge na udiwani waweke. Kuhusu kuangalia kura za rais kutoa wabunge wa viti maalum, huku ndo kuangalia maslahi ya muda mfupi na kuacha kupanga mipango ya muda mrefu. Katika siasa wakati mwingine lazima kukubali kupoteza maslahi fulani ya muda mfupi kwa ajili ya vitu vikubwa zaidi. Mtoa mada nimemkubali pointi zake. Na wewe hongera kwa kuchangia lakini kwenye ukweli ni muhimu tukubali. Mimi sijawahi kupigia kura ccm lkn safari hii namchagua magufuli tu kwenye Urais. Kwa wabunge na madiwani bado napima.