Ccm mnaishauri chadema chakufanya?Mzee Mtei na marehemu Bob Makani walikuwa wanajua strategies unazoongea sana na ndiyo maana CHADEMA ikapanda hadi kuwa ilivyo leo, ila sasa hivi inaelekea kifo cha mende.
Mtanyoka mwaka huu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ccm mnaishauri chadema chakufanya?Mzee Mtei na marehemu Bob Makani walikuwa wanajua strategies unazoongea sana na ndiyo maana CHADEMA ikapanda hadi kuwa ilivyo leo, ila sasa hivi inaelekea kifo cha mende.
Ni kati ya mabandiko mazuri yenye hoja nzito nimepata kusoma JF. Hongera sana
Upinzani hawana uwezo wa kuishinda CCM hata miaka 100 ipite
CHADEMA ni watu wa matukio, kesho wakiona Lissu amejaza stendi thread zitajaa humu za kudai Lissu aapishwe, ooh watu wameichoka CCM na bla bla kibao, kivumbi cha Kigoma Leo kimewanock out kidogo. Kuna vitu tu wananchi wanatamani Rais avisikie na wanamtumia Lissu kufikisha huo ujumbe, ila inshort wanazengo hawamwamini na sad enough wengi wao sio wapiga kura.
CHADEMA ipo poor organized, viongozi wapo scattered, sio Mbowe, sio Nyalandu wote wanafight for survival, Lissu anajaribu kupambana na somehow amerestore some spirit, but alone without strategic, it is impossible to outshine full organized CCM. Ni kichekesho kuona CCM inakabidhi nchi Kwa genge ambalo halieleweki kama CHADEMA, Broadcast zote, jaji mkuu, NEC, wanatangaza CHADEMA imeshinda, what a fu-ck ....
Kwa Safari hii CCM haihitajiki hata kutumia another alternative japo wamejipanga, kura tu zinatosha, wasiyumbishwe na makelele ya chura wao kama tembo waendelee Tu kuyanywa maji.
Membe alinena Jambo la msingi sana japo walimbeza, kuitoa CCM ni zaidi ya ushabiki wa kwenye majukwaa ambalo hawalijui hata hao mabeberu wapo upande wa CCM.
Time will tell!Ccm mnaishauri chadema chakufanya?
Mtanyoka mwaka huu.
Kila ikifika jioni, huwa nasikiliza kampeni za vyama kikiwemo CHADEMA nikitegemea kwamba labda watakuwa na sera mpya za kistaarabu, kwa bahati mbaya sijaona kitu cha namna hiyo.
Kwanza kabisa, sijasikia sera mahsusi za kuweza kuwashawishi Watanzania hasa wenye akili timamu. Zaidi sana nasikia tu sera za kuwavutia vijana wa rika fulani ambao kwa kweli hawajakomaa kiakili, wapo kwenye kipindi cha Bendera fuata upepo na waliojaa mihemko tu.
Kwa hiyo, mpaka leo hii Magufuli amemwacha Lissu mbali saaaaaana. Mimi huwa napita pita mitaani na vijiweni kufanya utafiti kidogo. Asilimia kubwa ya watu hata wa CHADEMA wanamkubali sana Magufuli, na wengi wanasema kwa upande wa Rais watampa kura Magufuli.
Kwa nini Magufuli? Pamoja na sababu zingine, lakini jinsi alivyoshughulikia Issue Corona, watu wanamkubali sana Magufuli. Huyu mwingine shida inayompunguzia sifa ni kukosa staha, adabu, ustahimilivu nk. katika kuongea. Ikumbukwe kuwa, Watanzania hawajazoea na hawapendi shari.
Umenena, watanzania wengi bado ni wakarimu na wanapenda watu wanyeyekevu. Lissu anasema sana kama mtu mwenye dharau na kuonyesha anajua kila kitu (muck know) na watanzania hawapendezwi na hilo.
Yaani hizi hoja zako zimenifanya nicheke ile mbaya, eti upinzani ukitaka kuitoa ccm imuunge mkono Magufuli, halafu 2025 ndio ichukue nchi. Umesema upinzani lakini umeitaja cdm tu. Sasa ngoja tuone kwenye uhalisia wa hizi hoja zako.
- UDP na TLP wamemuunga mkono Magufuli, hivyo tutarajie kuwa 2025 watachukua nchi kwa hii nadharia yako? Kwa taarifa yako Magufuli angeachiwa safari hii apite bila kupingwa angejiongezea muda wa kukaa madarakani. Wapinzani kushiriki uchaguzi huu, tena wakiwa wamefanyiwa kila aina ya ukatili, na kuendelea kupata watu wengi kwenye mikutano yao, ni wazi kuwa hakuna uwezekano tena wa nchi hii kuendelea kuongozwa tu na ccm kwa kura halali.
- Kwa taarifa yako ujenzi wa miundombinu ni tabia binafsi ya Magufuli na sio ccm. Hivyo hata akitangazwa mshindi sio akishinda bado ataendelea na hiyo miundombinu. Mpaka sasa tayari Magufuli ana miradi miwili mikubwa ya 15t+, na yote analazimisha amalize ndani ya muda wake halali wa kisheria, iwapo hatachezea katiba. Mpaka sasa hakuna mradi hata mmoja uliofikia robo ya kukamilika na tayari wananchi wameshaumia sana. Hivyo kama ni kutua hela hajatoa hata nusu ya pesa yaani 7t. Hivyo anatakiwa ndani ya hii miaka mitano lazima apate 8-10t, ni wapi atapata hizo hela, achia mbali mahitaji mengine? Kwa vyovyote kufika hiyo 2025 bado ccm itazidi kuwa kwenye wakati mgumu maana kupata hizi hela za kumalizia hiyo miradi ni kiama.
- Hoja ya cdm kuchukua nchi ikiwa imejaa miundombinu ya kila namna, na kuwa rahisi kuendesha nchi kwa kujali maslahi ya mtu mmoja mmoja. Hoja hii ni kiini macho, tazama deni la taifa mpaka sasa ni kiasi gani toka awamu hii iingie madarakani. Ni wazi serikali sasa inakopa sana, huku terms za mikopo ikiwa inafahamika na mtu mmoja na genge lake. Katika mazingira hayo, una uhakika gani wa kuendesha nchi kirahisi ukiwa na madeni mazito hivyo? Kuhusu hoja ya Corona hapa ndio nimeona hujui unaoongea nini, kwani Corona Ni ugonjwa wa kudumu mpaka useme wazungu watalazimisha nchi iwekwe lockdown? Halafu acha upotoshaji wa kijinga, ni nani anataka kuchukua nchi ili apewe maelekezo na wazungu? Hii ni dhahiri uko na hoja za kuokoteza.
- Kwamba sasa hivi cdm imeshiriki uchaguzi huu na haitashinda hata kidogo. Kwani kushiriki ni lazima ushinde? Ingekuwa kushiriki kwenye ushindani wowote lazima ushinde, basi ligi kuu ya nchi yetu ingekuwa na simba na yanga tu maana ndio wenye uwezo wa dhahiri kushinda ligi. Halafu uchaguzi mkuu sio urais tu, bali kuna wabunge na madiwani, na kura za urais hutoa wabunge wa viti maalum. Kama miaka hii mitano tuliaminishwa kuwa ccm imeua upinzani, na kinachoonekana ni tofauti, ni kipi kitafanya sasa na hiyo 2025 isiwe rahisi kuitoa ccm? Kwa taarifa yako cdm ingeingia mkenge wa huu ushauri wako fake, kufika 2025 katiba ingekuwa imeshabadilishwa na ingehalalishwa kuwa upinzani umekufa.
Watu wenye shari utawaona tu. Matusi, kejeli, nk. Mungu akusaidie.
Nimekupa ukweli wako kwenye huu uhuni ulioandika hapa, hivyo unatafuta maneno ya utetezi dhaifu. Kaa kimya, au huu ushauri wako anzisha chama utumie mbinu hizo za kichovu kuchukua nchi.
Ukweli unauma ndo maana unatoka povu. Ukweli utabaki kuwa ukweli. Kama umechukia meza wembe. CDM mwaka huu sahau ushindi na mwaka 2025 sahau ushindi. Kwa sababu ya udhaifu wenu katika kupanga mikakati, itawagharimu kweli. Mtabaki kutukana tu. Hiyo ndo itabaki kuwa sera yenu kuu. Wenzenu wataendelea kujijenga kwa kurekebisha makosa. Nyie mtaendelea kusindikiza na jeuri ya matusi. Acha uje uone kivumbi tarehe 28 Oct. Hata mkinyang'anywa ushindi, hakuna mtu atakayeandamana kutetea wahuni. Watanzania sio wajinga.
Macho ya wenye dunia yote yako Tanzania hiyo October 28 ndugu. Subiri uone CCM anavyoshikishwa adabuNichukie nini, mimi nimekupa kitu na box. Hiyo tarehe 28 unayotambia hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Sio hata tukinyang' anywa ushindi, maana ni lazima ushindi uporwe, kwani ccm imekata moto kwenye ushindani. Hilo suala la kuandamana kaa ukiomba ukondoo uendelee, kinyume na hapo jiandae kutapika hirizi. Muhuni mkubwa ww.