econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Kwa maoni yangu naona CHADEMA inahitaji uongozi mpya kabisa. Naona watu wengi wanaangalia cheo Cha Mwenyekiti na kuacha kuangalia vyeo vingine. CHADEMA inahitaji Mwenyekiti mpya mwenye msimamo sio Leo anasema hivi kesho anabadilika. CHADEMA inahitaji mwenyekiti atakaye kuwa nembo ya chama ambayo kila mmoja ataitazamia.
Pia CHADEMA inahitaji Makamu Mwenyekiti mpya bara na visiwani. Makamu Mwenyekiti ambaye ni Kijana mwenye ushawishi na msimamo. Makamu Mwenyekiti anatakiwa kuwa mwenye maono sawa sawa na Mwenyekiti na mwenye itikadi sawa sawa na Mwenyekiti. Tumeona kwenye uongozi wa Sasa hivi, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Wana itikadi tofauti. Mwenyekiti ni vugu vugu Kwa CCM anashadadia maridhiano na CCM wakati Makamu Mwenyekiti yeye ni mpinga maridhiano na Hana urafiki na CCM . Hivyo ni muhimu Makamu Mwenyekiti ajaye awe na itikadi sawa na Mwenyekiti wake ili chama kisonge mbele.
Pamoja na hayo, CHADEMA inahitaji kuwa na Katibu Mkuu ambaye ni msomi wa Hali ya juu na mwenye ushawishi. CHADEMA inahitaji katibu Mkuu mpya mwenye exposure ya mambo ya utawala na fedha. Ambaye atakuja na mkakati wa kuijenga CHADEMA kiuchumi. Kutafuta wafadhili ndani na nje ya nchi watakao isaidia CHADEMA kwenye harakati zake. Katibu Mkuu asiwe mwanasiasa Sana, siasa awaachie Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti. Yeye aje na mbinu za kuleta fedha CHADEMA. CHADEMA ikikuwa kiuchumi ndipo mwanzo wa kushika Dola utaanza. Kwa Sasa chama hakina pesa hata za kuweka mawakala wa uchaguzi kwenye vituo vyote nchini, so Katibu Mkuu ajaye afanikishe hilo. Kwakweli tunahitaji Katibu Mkuu Mpya ambaye ni msomi aliyebobea kwenye utawala.
Pia, Kuna nafasi ya muhimu Sana ambayo CHADEMA inahitaji mtu mpya. CHADEMA inahitaji Mkurugenzi mpya wa Sera, Bunge na Mawasiliano. Huyu anatakiwa awe Kijana mwenye ushawishi kwa vijana na mwenye uwezo wa kuhamasisha vijana waje kujiunga CHADEMA. Kijana mbunifu na mwenye uwezo wa kuelezea matamko ya chama yakaeleweka. Mwenye uwezo wa kuingia sokoni na vijiweni kuongea na wananchi. Mkurugenzi wa Sasa wa Sera, Bunge na Mawasiliano Ndugu Mrema, amejitahidi kwa nafasi yake ila nadhani ni muda akiapisha damu changa. Maana CHADEMA inahitaji kuchukua base ya vijana ambao ndio wengi na ili kufanya hivyo inahitaji msemaji Kijana na mbunifu kwenye uhamasishaji.
Kama CHADEMA tunataka mabadiliko na kuhamasisha watu wajiunge kwenye chama, tufanye mabadiliko ya uongozi na kuleta watu watakao tupeleka mbele.