CHADEMA isitishe maandamano, isiingie kwenye mtego wa Polisi. Umma una maswali mengi kwa Polisi tunataka majibu

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Kwa watu wanaoujua mchezo wa chase huu mchezo uchezwa na watu wenye akili tu.

CHADEMA isikubali kufungwa chase na watu wenye akili ndogo kama hawa, iko hivi; umma wa Tanzania tuna maswali lukuki kwa jeshi lililofeli la Polisi na tunataka majibu ya kueleweka akiwemo huyo muuaji wao killing machine.

Sasa bad timing CHADEMA ikiingia kwenye mtego wa Polisi kututoa kwenye reli ili tujadili maandamano hakika mtatukosea sana Watanzania.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Ni heri hata Dr. Nchimbi ameongea diplomatic language sometimes ni mtu unaweza kukubaliana naye kuliko mtego ambao wameutega Polisi kwa CHADEMA ni kutuondoa kwenye mstari.

CHADEMA kwepeni huu mtego wa kiboya kutoka kwa watu waoga na wasio na weledi wowote.
 
Kwa watu wanaoujuwa mchezo wa chase huu mchezo uchezo uchezwa na watu wenye akili tu...
Sijui kwanini, ila naamini mahitaji ya Chadema yanaweza kutimizwa mapema kabla ya siku iliyotangazwa kuandamana. Hivyo, zoezi hilo linaweza lisifikie.

Huenda tamko lao lilikuwa ni sehemu ya kuhimiza kuharakishwa kwa ripoti ya polisi, na kuwa yenye maelezo ya kina na sio ya mtindo wa funika kombe kama ilivyo kawaida yao.

Isitoshe, uhusiano wa jeshi la polisi na mama si mzuri sana kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake. Na mara nyingi amekuwa akiwakosoa hadharani kwa uzembe na kuonea watu.

Hivyo, kwa presha hii ya Chadema ya kujumuisha ya madaraka ya ukuu wa nchi, ni kama inaongezea pilipili kwenye kidonda kibichi cha uhusiano wao usio na afya.

Bila shaka uhusiano wa mama na polisi unaweza kuzidi kuharibika kama watafanya kosa la kutokuwa serious na jambo hili na kuweka pabaya ukuu wake wa nchi.

Ova
 
Sijui kwanini, ila naamini mahitaji ya Chadema yanaweza kutimizwa mapema kabla ya siku iliyotangazwa kuandamana. Hivyo, zoezi hilo linaweza lisifikie.

Huenda tamko lao lilikuwa ni sehemu ya kuhimiza kuharakishwa kwa ripoti ya polisi, na kuwa yenye maelezo ya kina na sio ya mtindo wa funika kombe kama ilivyo kawaida yao.

Isitoshe, uhusiano wa jeshi la polisi na mama si mzuri sana kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake. Na mara nyingi amekuwa akiwakosoa hadharani kwa uzembe na kuonea watu.

Hivyo, kwa presha hii ya Chadema ya kujumuisha ya madaraka ya ukuu wa nchi, kwenye suala hili la utekaji linaongeza pilipili kwenye kidonda cha uhusiani wao.

Bila shaka uhusiano wa mama na polisi unaweza kuzidi kuharibika kama watafanya kosa la kutokuwa serious na jambo hili na kuweka pabaya ukuu wake wa nchi.

Ova
Umezungumza nadharia tupu zisizo halisi. Hakuna uhusiano wowote mbaya kati ya polisi na raisi, polisi ni watu wa kupokea order tu hawana ubavu wa kwenda kinyume na boss wao
 
Kwa watu wanaoujuwa mchezo wa chase huu mchezo uchezwa na watu wenye akili tu...
Hata kama ultimatum ikipita, siwashauri chadema waandamane.

Adui number 1 wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania si watu wanaofanya jinai ila chadema.

Ikitokea vifo kwenye hayo maandamano, Mungu aepishilie mbali, hasara itakuwa kwa chadema.

Please olisi kimoyomoyo wanaomba hayo maandamano yafanyike wapate pa kutokea
 
Umezungumza nadharia tupu zisizo halisi. Hakuna uhusiano wowote mbaya kati ya polisi na raisi, polisi ni watu wa kupokea order tu hawana ubavu wa kwenda kinyume na boss wao
Kusoma jambo na kuelewa ni uwezo pia, ambao siyo kila mtu huwa nao. So, nipokee tu kwa namna hiyo hiyo ulivyoelewa, kisha nikuache. Ikiwa utapata wa kukuelewesha ni heri.

Labda hukumbuki kisa cha mama kuwahi kukamatwa na polisi kwa sababu ya gari lake kuwa likiwaka taa moja wakati akitoka harusini.

Hizi ndizo baadhi ya kauli zake kwa Jeshi la Polisi:
"Inawezekana kesi haziji vituoni kwa sababu watu wamekata tamaa, kwa kuwa wakija hawapati haki zao."
Agosti 25, 2021

"Haiwezekani polisi wafanye mauaji, halafu wajichunguze wenyewe."
Februri 04, 2022

"Kwa muda mrefu, Jeshi la Polisi linasifika vibaya, ilikuwa muhimu kuanza kuliangalia, ili watu walitazame vizuri, jeshi linapaswa kuwa kimbilio na sio kilio cha watu."

"Vitendo vinavyofanywa na askari polisi barabarani, huwezi kudhani kwamba wamehitimu mafunzo."
Julai 21, 2022

"Kutokana na kukithiri kwa rushwa ndani ya jeshi la polisi, tutalazimika kutumia kamera."
Septemba 4,2023

Ova
IMG_20240914_020913.jpg
 
Attachments

  • IMG_20240914_020913.jpg
    IMG_20240914_020913.jpg
    161 KB · Views: 3
Nijuavyo kwa nguvu kubwa wanayowekeza polisi sioni cdm wakiandamana, labda cdm watoke hadharani waipe polisi muda wa mwezi mmoja kuja na ripoti ya watekaji, na walipo watu wanaotuhumiwa kutekwa na alitefanya mauaji ya Ali Kibao.

Ifahamike polisi na serekali ni wahusika wa huu utekaji, hivyo watahakikisha wanatumia nguvu kubwa kuficha ukweli.
 
Mkuu umezungumza sawa! Kwa kuwa Rais ameshatoa maelekezo uchunguzi ufanyike ingawa naamini hautafanyika leo au kesho ilikuwa busara kutoandamana.
Hata hivyo sina hakika kama kuna mwanachama wa CHADEMA atakayekuwa tayari kuingia barabarani.
Upande mwingine nadhani CHADEMA inaitikisa Serikali kujua kama iko serious au la.
 
CHADEMA kwepeni huu mtego wa kiboya kutoka kwa watu waoga na wasio na weledi wowote.
Hujaeleza lolote linalo eleweka, umebaki tu kuzunguka na "huo mtego" usio elezeka.
Hao polisi wameweka mtego wa kuwateka waTanzania na kuwaua ili iwanase CHADEMA. Sasa unataka CHADEMA wafanye nini, waendelee kusubiri na wengine wao waendelee kutekwa na kuuawa, eti kwa kuogopa mtego?

Haya ni mawazo ya ajabu sana.

Hebu anza na kuwahimiza hao wanaoweka mitego, wawaachie walio wateka kwanza. Hiyo itakuwa ni ishara ndogo ya kuwasaidia CHADEMA wasitishe hayo maandamano. Lakini pamoja na hayo; kwa nini udhani CHADEMA kuandamana ni mwiko. Kwani maadamano nchi hii yamezuiwa lini? Na kwa nini na hao polisi mnadhani maandamano ya CHADEMA ni lazima yawe na athari, kama siyo hao polisi wanao panga kusababisha maafa mengine?
 
@Dk Matola Phd huo mtego mbona mm sijauona? jamani hebu acheni kuwatoa nguvu wanachadema .tulipofika sio kabisa..hayajawakuta ndo maana.. hebu tuweni na umoja basi
 
Kwa watu wanaoujua mchezo wa chase huu mchezo uchezwa na watu wenye akili tu.

CHADEMA isikubali kufungwa chase na watu wenye akili ndogo kama hawa, iko hivi; umma wa Tanzania tuna maswali lukuki kwa jeshi lililofeli la Polisi na tunataka majibu ya kueleweka akiwemo huyo muuaji wao killing machine.

Sasa bad timing CHADEMA ikiingia kwenye mtego wa Polisi kututoa kwenye reli ili tujadili maandamano hakika mtatukosea sana Watanzania.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Ni heri hata Dr. Nchimbi ameongea diplomatic language sometimes ni mtu unaweza kukubaliana naye kuliko mtego ambao wameutega Polisi kwa CHADEMA ni kutuondoa kwenye mstari.

CHADEMA kwepeni huu mtego wa kiboya kutoka kwa watu waoga na wasio na weledi wowote.
Naunga mkono hoja, Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!
P
 
Hujaeleza lolote linalo eleweka, umebaki tu kuzunguka na "huo mtego" usio elezeka.
Hao polisi wameweka mtego wa kuwateka waTanzania na kuwaua ili iwanase CHADEMA. Sasa unataka CHADEMA wafanye nini, waendelee kusubiri na wengine wao waendelee kutekwa na kuuawa, eti kwa kuogopa mtego?

Haya ni mawazo ya ajabu sana.

Hebu anza na kuwahimiza hao wanaoweka mitego, wawaachie walio wateka kwanza. Hiyo itakuwa ni ishara ndogo ya kuwasaidia CHADEMA wasitishe hayo maandamano. Lakini pamoja na hayo; kwa nini udhani CHADEMA kuandamana ni mwiko. Kwani maadamano nchi hii yamezuiwa lini? Na kwa nini na hao polisi mnadhani maandamano ya CHADEMA ni lazima yawe na athari, kama siyo hao polisi wanao panga kusababisha maafa mengine?
Maandamano ni haki ya kikatiba lakini inaeleweka wazi maandamano yana nguvu ya kuangusha serikali yoyote.

Kukishakuwa na tention kama hii serikali haiwezi kukubali maandamano lazima watumie mdomo wa Polisi.

Sasa hapa ndipo mnamuonaga Mbowe hafai kwa sababu ni lazima apime damage itakayotokea.

Chadema iking'ang'ania kuandamana wao ndio watakuwa loser, kwanza hawatopsts support ya umma, watakwenda wanachadema tupu kupigwa virungu na kupata ulemavu tu.

Mimi siamini katika ukondoo, lakini ni wrong timing kwa Chadema kuandamana sasa wao ndio watakaopoteza na maswali yote tunayosubiri majibu ndio itakuwa imetoka hiyo.

Watanzania tuwe na subira freedom is coming.
 
Kwamba freedom is coming tomorrow sio🤔

Kesho haijawahi fika,

Maandamano ndio njia pekee yenye majibu na suluhu ya maswali yote.
 
Back
Top Bottom