CHADEMA isitishe maandamano, isiingie kwenye mtego wa Polisi. Umma una maswali mengi kwa Polisi tunataka majibu

Kwa watu wanaoujua mchezo wa chase huu mchezo uchezwa na watu wenye akili tu.

CHADEMA isikubali kufungwa chase na watu wenye akili ndogo kama hawa, iko hivi; umma wa Tanzania tuna maswali lukuki kwa jeshi lililofeli la Polisi na tunataka majibu ya kueleweka akiwemo huyo muuaji wao killing machine.

Sasa bad timing CHADEMA ikiingia kwenye mtego wa Polisi kututoa kwenye reli ili tujadili maandamano hakika mtatukosea sana Watanzania.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Ni heri hata Dr. Nchimbi ameongea diplomatic language sometimes ni mtu unaweza kukubaliana naye kuliko mtego ambao wameutega Polisi kwa CHADEMA ni kutuondoa kwenye mstari.

CHADEMA kwepeni huu mtego wa kiboya kutoka kwa watu waoga na wasio na weledi wowote.
WAmepewa muda miaka 7,hawajatafuta majibu kwa hiari,sasa wanasubiri wayatafuye kwa viboko?
 
Chadema wanataka majibu ya hatma ya wanachama wao waliotekwa, Wana haki ya kudai hilo.
P anasahau kuna kale kamnyama kadogo kana pambana na simba na mwenyewe anasepa,kale kanakula nyoka,na haya nyuki.
 
Kusoma jambo na kuelewa ni uwezo pia, ambao siyo kila mtu huwa nao. So, nipokee tu kwa namna hiyo hiyo ulivyoelewa, kisha nikuache. Ikiwa utapata wa kukuelewesha ni heri.

Labda hukumbuki kisa cha mama kuwahi kukamatwa na polisi kwa sababu ya gari lake kuwa likiwaka taa moja wakati akitoka harusini.

Hizi ndizo baadhi ya kauli zake kwa Jeshi la Polisi:
"Inawezekana kesi haziji vituoni kwa sababu watu wamekata tamaa, kwa kuwa wakija hawapati haki zao."
Agosti 25, 2021

"Haiwezekani polisi wafanye mauaji, halafu wajichunguze wenyewe."
Februri 04, 2022

"Kwa muda mrefu, Jeshi la Polisi linasifika vibaya, ilikuwa muhimu kuanza kuliangalia, ili watu walitazame vizuri, jeshi linapaswa kuwa kimbilio na sio kilio cha watu."

"Vitendo vinavyofanywa na askari polisi barabarani, huwezi kudhani kwamba wamehitimu mafunzo."
Julai 21, 2022

"Kutokana na kukithiri kwa rushwa ndani ya jeshi la polisi, tutalazimika kutumia kamera."
Septemba 4,2023

Ova
View attachment 3095320
Kuwahi kukamatwa huko zamani hiyo si sababu ya kusema sasa hivi hawapatani. Huko zamani hakua boss wao. Ni kama ambavyo mkuu wa mkoa wa morogoro Adam malima alivyowahi kukamatwa barabarani miaka michache nyuma, basi leo useme mkuu wa mkoa morogoro hapatani na polisi. Hayo matukio hutokea ikiwa huna nafasi kubwa, leo kuna polisi anaweza mkamata barabarani?

Kaka hizi nukuu kwa kiongozi yoyote huzitoa ili kuweka mambo sawa sababu kuna polisi ambao hawana maadili. Lakini hii tafsiri yake sio kuwa hapatani na jeshi la polisi lote. Zipo pia nukuu nyingi zaidi za kuwasifia. Je hapo tutasemaje? Si mama Samia tu maraisi hata waliopita kikwete, magufuli wote waliwahi kutoa kauli za kuwashutumu polisi. Lakini haikua na maana hawapatani nao

Kwa muundo wa serikali JMT hakuna polisi ana nguvu yoyote mbele ya mamlaka ya Raisi. Hii kutopatana ni uongo. Raisi ana nguvu ya kufanya chochote kuanzia IGP Hadi kwa private wa chini kabisa.
Ungeniambia jeshi(JWTZ) ningekuelewa sababu muundo wao ni tofauti kidogo, lakini sio polisi ambao hata mkuu wa mkoa tu anawaamrisha anavyotaka
 
Maandamano ni haki ya kikatiba lakini inaeleweka wazi maandamano yana nguvu ya kuangusha serikali yoyote.

Kukishakuwa na tention kama hii serikali haiwezi kukubali maandamano lazima watumie mdomo wa Polisi.

Sasa hapa ndipo mnamuonaga Mbowe hafai kwa sababu ni lazima apime damage itakayotokea.

Chadema iking'ang'ania kuandamana wao ndio watakuwa loser, kwanza hawatopsts support ya umma, watakwenda wanachadema tupu kupigwa virungu na kupata ulemavu tu.

Mimi siamini katika ukondoo, lakini ni wrong timing kwa Chadema kuandamana sasa wao ndio watakaopoteza na maswali yote tunayosubiri majibu ndio itakuwa imetoka hiyo.

Watanzania tuwe na subira freedom is coming.
Wakiandamana au wasipoandamana bado huwezi kupata majibu yoyote. Lilipotokea tukio la lissu hakuna walioandamana na bado majibu hayakutoka.
Kuna ile issue ya yule sativa kilichotokea lakini bado hakuna majibu yoyote. Kama unasubiri majibu basi Hakuna majibu utapata. Hata hivyo maandamano bongo bado hayana nguvu ya kuangusha serikali wala kubadilisha kile ambacho serikali imedhamiria kufanya
 
Kuwahi kukamatwa huko zamani hiyo si sababu ya kusema sasa hivi hawapatani. Huko zamani hakua boss wao. Ni kama ambavyo mkuu wa mkoa wa morogoro Adam malima alivyowahi kukamatwa barabarani miaka michache nyuma, basi leo useme mkuu wa mkoa morogoro hapatani na polisi. Hayo matukio hutokea ikiwa huna nafasi kubwa, leo kuna polisi anaweza mkamata barabarani?

Kaka hizi nukuu kwa kiongozi yoyote huzitoa ili kuweka mambo sawa sababu kuna polisi ambao hawana maadili. Lakini hii tafsiri yake sio kuwa hapatani na jeshi la polisi lote. Zipo pia nukuu nyingi zaidi za kuwasifia. Je hapo tutasemaje? Si mama Samia tu maraisi hata waliopita kikwete, magufuli wote waliwahi kutoa kauli za kuwashutumu polisi. Lakini haikua na maana hawapatani nao

Kwa muundo wa serikali JMT hakuna polisi ana nguvu yoyote mbele ya mamlaka ya Raisi. Hii kutopatana ni uongo. Raisi ana nguvu ya kufanya chochote kuanzia IGP Hadi kwa private wa chini kabisa.
Ungeniambia jeshi(JWTZ) ningekuelewa sababu muundo wao ni tofauti kidogo, lakini sio polisi ambao hata mkuu wa mkoa tu anawaamrisha anavyotaka
Ndiyo maana nasema kusoma na kuelewa jambo ni uwezo ambao kwa bahati mbaya wewe huna. Hakuna mahali nimesema Polisi wana nguvu mbele mamlaka ya Rais. Hilo limekuja kwa uelewa wako wewe.

Labda, unapata shida kuelewa kuhusu uhusiano mzuri au mbaya wa watu fulani, kwani hili nalo hutaka uelewa mpana kidogo wa jambo husika, hivyo wala sikulaumu kwa huko kutokuelewa kwako, ni kawaida.

Kwani, cheo kipya cha Naibu Waziri Mkuu, kimeletwa kwa sababu gani?
Nikifafanua kuhusu cheo hicho kipya cha NWM kimekuja kwa sababu ya uhusiano usio na afya wa mkuu wa nchi na PM, siyo kama vile kusema PM ana mamlaka kuliko Rais.

Mtangulizi wake alimrudisha Kaganda HQ na kumvua u-RPC baada ya kauli ya kulaumu polisi kuchukua rushwa ya 'laki mbili kwenye doria ya Ashok, na kuwa njaa zao wanahamishia kwenye mifuko ya watu'.

Hata SP Kalanje baada ya kumtolea bunduki Nape, si alipelekwa Mtwara kuwa OC-CID, yaani akawa mkubwa zaidi. Uhusiano wa watu utauona kwa matendo na kauli zao, ila kama una akili ya kung'amua.

Uhusiano wa watu kuwa mbaya au mzuri hakuhusu ukubwa au udogo wa mtu. Kama ilivyokuwa kwenye mgogoro wa Ndugai na Masele wakati ule na mambo ya Bunge la Afrika.

Hata mzazi na mtoto wake wanaweza kuwa na uhusiano mbaya, na mzazi akabaki kuwa mzazi. Hata January alimwita JPM mshamba kwa sababu ya uhusiano mbaya, na bado alibaki kuwa ni mwenyeki wa chama chake anayeamua kuhusu yeye kichama.

Ova
 
ungetupa sababu tuone kwann wanaandamana
Kama ndizo zinafanya yafanyika hakuna haja ya kuogopa usemayo
 
Maandamano ni haki ya kikatiba lakini inaeleweka wazi maandamano yana nguvu ya kuangusha serikali yoyote.

Kukishakuwa na tention kama hii serikali haiwezi kukubali maandamano lazima watumie mdomo wa Polisi.

Sasa hapa ndipo mnamuonaga Mbowe hafai kwa sababu ni lazima apime damage itakayotokea.

Chadema iking'ang'ania kuandamana wao ndio watakuwa loser, kwanza hawatopsts support ya umma, watakwenda wanachadema tupu kupigwa virungu na kupata ulemavu tu.

Mimi siamini katika ukondoo, lakini ni wrong timing kwa Chadema kuandamana sasa wao ndio watakaopoteza na maswali yote tunayosubiri majibu ndio itakuwa imetoka hiyo.

Watanzania tuwe na subira freedom is coming.
Mkuu 'Matola' pamoja na kwamba wewe unajiona siyo "kondoo", lakini watu wa aina yako hadhi yenu wakati mwingine mnajiweka kuwa chini ya kiwango cha hao "kondoo".

Serikali inayo fanya mambo yasiyofaa, ili kuwanasa (mtego) wananchi wake (CHADEMA); hiyo serikali bado unaiamini inafanya mambo kwa maslahi ya wananchi? Hiyo serikali ndiyo imekuwa mhalifu; sasa unataka wananchi wafanye nini?

Mhalifu yupo mtaani kwako, kawatia hofu raia wote wa mtaa na hakuna hata mmoja wenu aliye tayari kumkabiri. Mbaya zaidi kunazuka wapuuzi ndani ya jamii yenu kuwatisha hata wale wanaojaribu kutafuta njia za kumkabili huyu mhalifu,... hii inaingia akilini kweli?

Hakuna anayetafuta maafa ndani ya nchi yetu, lakini vitendo vinavyo fanywa na hawa watawala sasa hivi ni wazi lengo lao ni kutupeleka huko.
Waambie hao polisi; bado kuna muda wa kutosha kabla ya maandamano; waeleze hao watu walio potezwa wako wapi; au hata waonyeshe juhudi wanazofanya; lakini unapokuja hapa na vitisho tu kwa watu kama unavyo fanya wewe; elewa kwamba Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kuwaondoa viongozi madarakani kwa nguvu.

Ninakudharau sana na hivi vihoja vyako vya kipuuzi unavyo leta hapa.
 
Maxence Melo naomba msaidieni huyu mwenye ID ya Kalamu jinsi ya kutumia JF kwa usahihi. Kwenye post ya 12 katika thread hii amechanganya mambo hadi shida kumwelewa.

Kwa sasa mfundisheni tu, ili baadaye ashiriki vizuri kwenye mijadala.

Ova
Kwani kilicho kukwaza hapo ni kipi hasa mkuu 'Mdakuzi', kiasi kwamba uone nahitaji msaada unao niitia hapa.
Nimetumia JF miaka mingi hapa; sasa nashangaa wewe unataka nipewe mafunzo ya matumizi yake?

Kilicho tokea katika bandiko hilo ulilotaja hapo, ni 'formating' tu; lakini maelezo yake hayana upungufu wowote.
Jaribu kutumia akili kidogo kudadisi hali unayo iona, badala ya kukimbilia kwenye hitimisho lisilo husika.

Kama unayo mengine, tujadili hayo, lakini siyo upuuzi huu ulioweka hapa.
 
Mkuu 'Matola' pamoja na kwamba wewe unajiona siyo "kondoo", lakini watu wa aina yako hadhi yenu wakati mwingine mnajiweka kuwa chini ya kiwango cha hao "kondoo".

Serikali inayo fanya mambo yasiyofaa, ili kuwanasa (mtego) wananchi wake (CHADEMA); hiyo serikali bado unaiamini inafanya mambo kwa maslahi ya wananchi? Hiyo serikali ndiyo imekuwa mhalifu; sasa unataka wananchi wafanye nini?

Mhalifu yupo mtaani kwako, kawatia hofu raia wote wa mtaa na hakuna hata mmoja wenu aliye tayari kumkabiri. Mbaya zaidi kunazuka wapuuzi ndani ya jamii yenu kuwatisha hata wale wanaojaribu kutafuta njia za kumkabili huyu mhalifu,... hii inaingia akilini kweli?

Hakuna anayetafuta maafa ndani ya nchi yetu, lakini vitendo vinavyo fanywa na hawa watawala sasa hivi ni wazi lengo lao ni kutupeleka huko.
Waambie hao polisi; bado kuna muda wa kutosha kabla ya maandamano; waeleze hao watu walio potezwa wako wapi; au hata waonyeshe juhudi wanazofanya; lakini unapokuja hapa na vitisho tu kwa watu kama unavyo fanya wewe; elewa kwamba Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kuwaondoa viongozi madarakani kwa nguvu.

Ninakudharau sana na hivi vihoja vyako vya kipuuzi unavyo leta hapa.
Ikiwa ni mmoja au sehemu ya watekelezaji wa utekaji huu,au mshabiki wa mambo haya atakupuuza.Ili ikiwa ni timamu na asiye amini katika mambo haya atakuelewa na hao watoa vitisho atawasaidia kujua wanapokwamia.
 
Hivi huyu killing machine hatuwezi kujifanya wananchii wenye hasira tukamchomoa nafsi...
 
Kwani kilicho kukwaza hapo ni kipi hasa mkuu 'Mdakuzi', kiasi kwamba uone nahitaji msaada unao niitia hapa.
Nimetumia JF miaka mingi hapa; sasa nashangaa wewe unataka nipewe mafunzo ya matumizi yake?

Kilicho tokea katika bandiko hilo ulilotaja hapo, ni 'formating' tu; lakini maelezo yake hayana upungufu wowote.
Jaribu kutumia akili kidogo kudadisi hali unayo iona, badala ya kukimbilia kwenye hitimisho lisilo husika.

Kama unayo mengine, tujadili hayo, lakini siyo upuuzi huu ulioweka hapa.
Kama unaona ile post ilikuwa sawa, basi naomba unisamehe. Endelea tu huo mtindo wako wa kupost.

Ova
 
Ni kweli kabisa kuandamana ni haki na jeshi la Polisi lina haki kuyazuia kwasababu za kiusalama, kuandamana maandamano yaliyo zuiwa ni kushiriki maandamano haramu.
P
P nawewe unaachaje kuingizwa kwenye uchunguzi utakao fanywa juu ya ujinga huu unaoendelea hapa kusadikika zaidi ya miaka 7 iliyopita,bila majawabu,hata pale yalipo takiwa kutolewa?
 
Kwa watu wanaoujua mchezo wa chase huu mchezo uchezwa na watu wenye akili tu.

CHADEMA isikubali kufungwa chase na watu wenye akili ndogo kama hawa, iko hivi; umma wa Tanzania tuna maswali lukuki kwa jeshi lililofeli la Polisi na tunataka majibu ya kueleweka akiwemo huyo muuaji wao killing machine.

Sasa bad timing CHADEMA ikiingia kwenye mtego wa Polisi kututoa kwenye reli ili tujadili maandamano hakika mtatukosea sana Watanzania.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Ni heri hata Dr. Nchimbi ameongea diplomatic language sometimes ni mtu unaweza kukubaliana naye kuliko mtego ambao wameutega Polisi kwa CHADEMA ni kutuondoa kwenye mstari.

CHADEMA kwepeni huu mtego wa kiboya kutoka kwa watu waoga na wasio na weledi wowote.
Hoja kuntu walio tekwa wako wapi?
 
Tarehe 23 tutarajia vilema wapya, Polisi wameonya atakae kaidi atakutana na FFU huku pembeni JW wamesema watakuwa wanafanya usafi, uoga wako ndio maisha yako, kumbuka mashujaa siku zote huwa wanapewa heshima na waoga.
 
Polisi hamna jibu wanatoa kwahiyo anza kufanya mazoezi ya kukimbia kwaajili ya maandamano, wao polisi naona wameshaanza mazoezi ya kukimbia
 
Kuwahi kukamatwa huko zamani hiyo si sababu ya kusema sasa hivi hawapatani. Huko zamani hakua boss wao. Ni kama ambavyo mkuu wa mkoa wa morogoro Adam malima alivyowahi kukamatwa barabarani miaka michache nyuma, basi leo useme mkuu wa mkoa morogoro hapatani na polisi. Hayo matukio hutokea ikiwa huna nafasi kubwa, leo kuna polisi anaweza mkamata barabarani?

Kaka hizi nukuu kwa kiongozi yoyote huzitoa ili kuweka mambo sawa sababu kuna polisi ambao hawana maadili. Lakini hii tafsiri yake sio kuwa hapatani na jeshi la polisi lote. Zipo pia nukuu nyingi zaidi za kuwasifia. Je hapo tutasemaje? Si mama Samia tu maraisi hata waliopita kikwete, magufuli wote waliwahi kutoa kauli za kuwashutumu polisi. Lakini haikua na maana hawapatani nao

Kwa muundo wa serikali JMT hakuna polisi ana nguvu yoyote mbele ya mamlaka ya Raisi. Hii kutopatana ni uongo. Raisi ana nguvu ya kufanya chochote kuanzia IGP Hadi kwa private wa chini kabisa.
Ungeniambia jeshi(JWTZ) ningekuelewa sababu muundo wao ni tofauti kidogo, lakini sio polisi ambao hata mkuu wa mkoa tu anawaamrisha anavyotaka
Sasa hata Kwa upande wa Jwtz ni nani anaweza kuwa na mamlaka mbele ya Rais?
 
Back
Top Bottom