Wakati wa mapambano ya kutafuta haki, unatakiwa kutafuta umoja wenye nguvu na kila mwenye dhamira njema bila ya kujali ukubwa au udogo wake.
Pamoja na maneno mengi hasi na chanya, binafsi naamini vyama kama ACT Wazalendo na CUF, vina watu makini, wenye ushawishi, utashi na dhamira njema, na wanapitia madhira yale yale wanayoyapitia CHADEMA, na wananchi kwa ujumla, japo kwa viwango tofauti.
Viongozi kama Zitto Kabwe, naamini bado ana nguvu, ujasiri na ushawishi pia.
DHuluma ya CCM dhidi ya umma wa Watanzania, ituunganishe Watanzania wote wenye dhamira njema, iviunganishe vyama vyote vya siasa vyenye dhamira njema, hata kama vyama hivyo pengine havina nguvu zinazolingana.
Hivyo ni muhimu, ikiwezekana, Kamati kuu ya CHADEMA ijadili namna ya kushirikisha vyama vyote vyenye dhamira njema, katika kufikia uamuzi wa pamoja, juu ya hatua za kuchukua baada ya uchaguzi kuharibiwa kwa kiwango kisichotibika.
Ushauri wangu, kwanza ni kuitaka serikali kuufuta uchaguzi huu kwa kuwa ni haramu. Uchaguzi uitishwe upya na usimamiwe na Tume ya uchaguzi, waziri Mchengerwa afunguliwe mashtaka ya uhaini, kwa kosa la kutaka kuteka mamlaka ya wananchi .Ni uchaguzi umechochea chuki dhidi ya ccm na serikali yake.Mimi sina chama.ILA KWA UCHAGUZI WA SAFARI HII WATANZANIA TUMECHAGULIWA NA VIONGOZI WA CCM WATU WA KUTUONGOZA.SERIKALI IMEPOKA MADARAKA YA WANANCHI.