Elections 2010 CHADEMA iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee

Status
Not open for further replies.

kitila,

without going deep, inakuaje utaratibu uliouweka wewe mwenyewe, unakiukwa kwenye hiyohiyo taratibu na kuanza kwenda beyond chadema kusema huyu anachagulika au huyu la???

hiyo intelligensia mnayo-apply sasa si mngeitumia toka mwanzo tu m-save pesa basi kwa uchaguzi mkuu??? You guys are contradicting yourselves and the main reason is you look to who has money, which to me say that kwenye procurement na nyinyi mpo

I am just disappointed because you dont practice what you preach
 

Hata mimi humfikiria hivyo wakati mwingine. Ni kama vile Mchungaji Mtikila alivyoanza siasa (mapema miaka ya 90) alivyopata mashabiki wengi sana lakini jinsi miaka ilivyokuwa inakwenda ikaonekana dhahiri hakuwa na specific aims zilizoelweka katika kuwakomboa "walalahoi" kutoka kwa hao "magabachori." Sasa hivi anakula sahani moja na hao "magabachori!'

Mjadala wa kuhusu CCJ na MMKJJ wiki kadha zilizopita pia zilionyesha kuwa kulikuwa a lot behind ushabiki wa Mzee wa Jamvini (as some one has called him here) that what actually meet the eye. Siku hizi nazisoma baadhi ya makala zake na topic zake za JF 'with a pinch of salt, as they say.'
 
hawezi kujibu, mkuki mtamu kwa nguruwe, hata leo umwambie mbowe au zitto wapishe kaja mtu potential, wanaweza hata kuvua yale magwanda watembee uchi

just sad really
 
hawezi kujibu, mkuki mtamu kwa nguruwe, hata leo umwambie mbowe au zitto wapishe kaja mtu potential, wanaweza hata kuvua yale magwanda watembee uchi

just sad really
nimecheka sana Acid unajua ku practise demokrasia ni gumu sana MKJJ anasema hayo kwa vile yuko nje ya uwanja akiingia ndani anaweza hata kujifunga goli na kumpiga chenga kipa wake.
 
nimecheka sana Acid unajua ku practise demokrasia ni gumu sana MKJJ anasema hayo kwa vile yuko nje ya uwanja akiingia ndani anaweza hata kujifunga goli na kumpiga chenga kipa wake.
huyo ndiyo bingwa wa kujichanganya.... ana very controversial statements na ukimwambia badae anasema "wasnt me"

waswahili wanasema kuchamba kwingi kutoka na najisi
 
Kwa hili ninakubaliana kabisa na mwanakijiji. Maana ya kuendesha uchaguzi ni kumpata mshindi, na msingi mkubwa wa demokrasia ya uchaguzi ni kuwa mshindi hupatikana kwa wingi wa kura halali chni ya utaratibu uliopo. Inawezekana kabisa kuwa mshindi wa ndani ya CHADEMA hataweza kuwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu, lakini hiyo ndiyo demokrasia yenyewe tunayotaka kuimarisha.

Kwa vile akina dada hao ndio waliopata kura nyingi za halali chini ya utaratibu halali uliopo, waacheni waendelee kuipeperusha bendera yenu. Inawezekana kweli Mpendazoe ana nafasi kubwa ya kushinda, lakini kama yeye ni mwana demokrasi kweli ni lazima pia akubaliane na msingi huo wa demokarasia, na kama anakipenda chama, basi atumie influence ambayo ingempa yeye ushindi kuhakikisha kuwa mgombea wa chama chake ndiye anashinda katika jimbo hilo- yaani amsaidie kupiga kampeini kwa nguvu na uwezo wake wote kama ambavyo angejifanyia mwenyewe.
 
Kwa hili ninakubaliana kabisa na mwanakijiji. Maana ya kuendesha uchaguzi ni kumpata mshindi, na msingi mkubwa wa demokrasia ya uchaguzi ni kuwa mshindi hupatikana kwa wingi wa kura
Na kwa hili hapa chini je unaungana naye...... huyu jamaa si wa kumwekea mdhamana anaweza kukugeuka wakati wowote leo kasema hivi kesho anakana matamshi yake..........

Wabunge waliogongana Richmond warudishwe
Maana yake hataki tena kuheshimu kura ya maoni anataka NEC ya CCM ifanye hisani kuwarudisha anaowataka yeye hata kama hawakushinda sijui ndiyo demokrasia ya MKJJ anayoitaka.
 
hivi kuna anaejua hao wagombea walipigiwa kura na watu wangapi? (naomba jibu lisije kwa mfumo wa asilimia kama inawezekana)
 
ugomvi na nani?
we unajua kabisa upinzani tanzania wanachama kichele halafu unataka votes in numbers!!! tutakupa kwa asilimia tu, hayo mengine unayoyataka hatuwezi, siyo utaratibu wetu, kwanza chama chetu bado kinakua, hatuwezi kufikia mebmbers 40,000 kama monduli
 

ndugu Kitila hivi mnajuaje kuwa mtu anachagulika kuliko mwingine mkiwa ofcn? ikiwa wapiga kura walimkataa? hizo si bange tuu jamani
kwa hili nafikiri CHADEMA ni mbovu kuliko hata CCM (angalau wale CCM walitoa sababu ya rushwa ama uraia, nyie sababu ni nini?.
na kama hili linafaa kwenu do not waste resources kupiga kura za maoni
 
Kitu cha msingi kabisa kuzingatia katika mjadala huu ni kwamba, kwa CHADEMA, inayofanya uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge na hata urais ni Kamati Kuu. Kura za maoni na Maoni ya Kamati ya Utendaji ni nyenzo tu za kuisaidia Kamati Kuu kufanya maamuzi na kutoa mapendekezo yake kwa vyombo vya juu zaidi kimaamuzi. Ndio maana hata Dk Slaa aliombwa kugombea na Kamati Kuu baada ya utafiti wa takribani mwaka mmoja, na wala sio kwamba yeye alijitokeza. Hii ni kwa sababu swala la uongozi kwa CHADEMA, hasa kwa kazi kubwa kama ubunge na urais ni swala zito la chama na nchi, badala ya kuwa swala la mtu binafsi. Kwa wenzetu, kama walivyowahi kusema wao wenyewe, ni swala la mtu binafsi na familia zao. To us the party and the country stand taller than the individual. We are prepared to hurt an individual if that hurting will heal the party and the nation. Tatizo ninaloliona katika mjadala huu ni kwamba watu wanajadili with a CCM system in mind. Ours is a different system altogether. If there is something wrong with the system, then let the debate deal with it.
 
we unajua kabisa upinzani tanzania wanachama kichele halafu unataka votes in numbers!!! tutakupa kwa asilimia tu, hayo mengine unayoyataka hatuwezi, siyo utaratibu wetu, kwanza chama chetu bado kinakua, hatuwezi kufikia mebmbers 40,000 kama monduli

Acid samahani kwa kukukwaza............i was just pondering yaliyosemwa na Luteni kuwa labda wagombea walipigiwa kura na watu 12 na wa kwanza kushinda kwa kura sita, kwa hiyo kutengua maamuzi ya hao watu 12 kwa mgombea bora zaidi si tatizo.

nilikuwa najiuliza hivi aliyoyasema Luteni yawezekana kweli au ni ya kusadidika kama mfumo dume wa chadema uliotajwa na mwanakijiji.

juu ya hivyo nashukuru kwa jibu lako ............inaonyesha Luteni yuko karibu na jibu zaidi ya nilivyodhani....
 
Kwa hiyo utaona hapa kuwa utaratibu wa kuwapata wagombea ubunge ndani ya CHADEMA unatofautiana mno na ule wa CCM. Kwa hiyo ulinfganifu uliofanywa sio wa kimantiki.

Ni kweli kuna tofauti kwa kiasi lakini bado kuna mambo ya Rufaa kwenda Kamati Kuu, na Kamati Kuu kuwa na final say. Binafsi ningependa sana kuona utaratibu unatengenezwa ili mambo yote yaishie huko huko Jimboni. Kwamba, mchakato mzima wa kura za maoni unasimamiwa vizuri, kwa uwazi na kwa haki ili kuja kuondoa malalamiko yoyote. Na zaidi, uchujaji wa wagombea unafanywa kama ulivyosema kwenye ngazi hizo za jimbo na wanaachwa wagombee atakayeshinda ameshinda. Lakini, kurudisha nguvu zaidi kwa Kamati Kuu kuhusu wagombea naamini ni mfumo wa ki CCM. Unaweza kufaa kwa wakati huu lakini huko mbeleni Chadema itakaposhika madaraka utatuletea matatizo yale yale tunayoyaona kwa CCM.
 

KUrudia wimbo ule ule, kwa watu wale wale ukitegemea watacheza ni kujisumbua. NImeshatolea jibu hilo. Nilishachukua msimamo huo August 3, 2010 kwenye facebook yangu:

 
hawezi kujibu, mkuki mtamu kwa nguruwe, hata leo umwambie mbowe au zitto wapishe kaja mtu potential, wanaweza hata kuvua yale magwanda watembee uchi

just sad really

CHADEMA, Hii mada ni kwa faida yenu kuliko vinginevyo, inabidi mfikirie mara mbili; Kuna watu tumeamua kuchukua Likizo maalum ili Uchaguzi utukute TZ angalau tumpatie Kura Yetu Dr. Slaa; sasa nyinyi mnaanza Mambo ya Ki-CCM: Mnatukatisha tamaa. Kuhusu swala la 'potential' Just imagine; huu ni mfano tu anyway!!! Mbowe sasahivi anakubali kuwa Dr. Slaa ni Potential ndani ya Chadema kwa nafasi ya Urais, imagine Jimboni kwa Mbowe patokee tatizo wakati wa uchaguzi, tarehe iahirishwe, na wakati uchaguzi unarudiwa Dr Slaa awe amepoteza nafasi ya Urais, kisha wanachama waseme Dr. Slaa ni potential kuliko Mbowe, kwa hiyo mbowe kaa pembeni umpishe Dr. Salaa agombee ubunge, ..... Hapo utaona moto wake.. Mweeee!!!
 


Kamati kuu si malaika inahusishwa kundi dogo ambalo kuna wakati linaweza lisijue hali halisi ya huko mitaani. maoni ya wananchi kama yamesimamiwa vizuri kimsingi ndiyo yanatoa picha ya wagombea. hata hizi tafiti zinazoongelewa huwa ni mkusanyiko wa maoni ya wananchi. suala hapa ni kamati kuu kupingana na maoni ya wananchi, huko mbeleni hamwoni yatakuja kuleta tafrani kubwa sana???
hivi ikiwa mgombea ana ushawishi na kamati kuu si ndiyo mtasema anachagulika?????? kwa sababu ana watetezi huko na kumbe wananchi hawamtaki?
 

hivi kuna anaejua hao wagombea walipigiwa kura na watu wangapi? (naomba jibu lisije kwa mfumo wa asilimia kama inawezekana)


hapa ni patamu kweli

lakini kama kwenye mchujo wanachama walikuwa wachache kwanini uchaguzi usirudiwe kuliko kupanga matokeo ofcn?
 

I am just interested to know what kind of healing to the nation if you take a middle finger that has been there and replace it with a thumb from another animal [i refer rachel versus Mpendazoe... who to me is a political prostitute who was ready to go to kinondoni simply because he was defeated by rachel, huko kishapu kafukuzwa?]

Kitla my colleague, vijana wa leo wengi hasa professional wana imani sana na ninyi na mkichakachua tu, basi mmevunja nguvu balaa, and that may work against you for the coming 20 years plus
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…