The Invincible
JF-Expert Member
- May 6, 2006
- 6,006
- 3,275
Kama kutakuwa na objectivity katika kulijadili suala hili basi huenda lawama dhidi ya Chadema zingeweza kuwa tofauti.Chama hiki kinakabiliwa na dilemma ya demokrasia,na sio kosa lao.Nitoe mfano japo sio wa kisiasa.Hivi timu inapopanda daraja na kufanikiwa kucehza ligi kuu,je ikitaka kutwaa ubingwa (na sio kushiriki tu kwenye ligi hiyo) haitopaswa kuunda timu ya ushindi?Of course,itakuwa sio haki kuwatosa wachezaji walioipandisha timu daraja lakini what if viwango vya wachezaji hao haviwezi kustahimili mikikimikiki ya ligi kuu?Na what if kama kuna wachezaji mahiri wenye potential ya kuleta kombe kwenye timu hiyo wapo willing kujiunga nao?
Tukija kwa Chadema,tunafahamu kuwa kura zao za maoni licha ya kujumuisha wanachama wachache (kutokana na idadi ndogo ya active members) pia sio sample mwafaka sana ya potential voters kwenye uchaguzi mkuu.Hilo sio kosa hasa ikizingatiwa kuwa hata CCM imekuwa ikipata kura nyingi zaidi ya idadi ya wanachama wake milioni 5 or so.Tutambue kuwa siasa za Tanzania,na sehemu nyingi Afrika bado zinaelemea zaidi kwa mgombea kuliko chama.Huo ni mfumo ambao utachukua miaka mingi kubadilika.
Ni kwa kutambua hivyo basi Chadema wanalazimika kufanya maamuzi magumu ya kupata wagombea wenye potential ya kutoa upinzani kwa CCM na pengine kukiwezesha chama hicho kupata idadi kubwa ya wabunge.Sasa je mnaoitakia mema Chadema mngependa "waridhishe demokrasia kwa kupitisha wagombea wenye uwezo haba wa kushinda" au waje na wagombea wanaoweza kuipatia ushindi?Tukumbuke huu ni mwaka wa uchaguzi na la muhimu zaidi ni ushindi HALALI.Mnaolinganisha udikteta wa CCM na "huu wa Chadema" mnasahau kuwa wakati "udikteta huu wa Chadema" unalenga kupata wagombea wenye potential ya ushindi (na process hii haisukumwi na rushwa au ufisadi) CCM hufanya mchezo huo kwa vile tu flani ana fedha za kutosha,anaweza kuhonga wapiga kura wengi na pengine anakidai chama hicho fadhila flani.
Pengine ni muhimu kwetu kutafakari kwa mapana zaidi dhima ya demokrasia hasa kwenye mwaka wa uchaguzi a kujiuliza,kwa mfano je linapokuja suala la kuteua wagombea kipi kiwe muhimu zaidi: wagombea walioteuliwa kwa njia za demokrasia au nafasi ya wagombea hao kushinda kwenye uchaguzi husika alimradi uteuzi wao haufanywi kwa njia zisizo halali?Au,kipi kiwe kipaumbele kwa chama katika mwaka wa uchaguzi kati ya kuenzi demokrasia na nafasi ya chama kufanya vizuri alimradi processes hizo zinafanywa kihalali na transparent?
Nami pia naona kuna kasoro fulani katika kujadili hili suala. Watu tunataka kulazimisha democracy and nothing but absolute democracy. Ukiangalia suala hili positively, inaonekana kama Chadema wanatumia busara. Ukienda kwenye extreme nyingine, inaonekana chama kinatumia ubabe. Hapo naona kizungumkuti tu.
Binafsi naamini Chadema hakina nia mbaya, ila kuweka wagombea watakaoshinda kwenye hayo majimbo. Kama wengine walivyosema, vyama vya upinzani havina nguvu sehemu nyingi. Hivi fikiria, kura za maoni ziendeshwe DP, chama cha Mtikila katika jimbo fulani huko Dodoma. Halafu ghafla bin vuu mzee Malecela anahamia hicho chama, na anakuwa kati ya wagombea wa kupigiwa kura za maoni. Anaangushwa katika kura hizo. DP itafanya vema kufuata demokrasia kwa kumwacha mzee Malecela pembeni? Thubutu!
With young democracy in a fragile political party, prudence and wisdom is of paramount importance in the party. That is strategic!