Kiranga,
Mkuu wangu uchaguzi nchini unawapa ushindi wagombea wenye popular vote sasa unachouliza haswa ni kipi?
Chama ni shirika la usafiri lenye vyombo vya usafiri kama mabus na kadhalika, kuwafikisha wananchi kule wanakotaka kwenda lakini hawawezi kufika huko pasipo dereva. Na kila bus linahitaji dereva. Usinambie dereva wa Scania hawezi kuendesha Volvo.. hiki ndio sisi tunachokataa.
Kama Chadema wanahitaji dereva anayeweza kuongoza msafara wa wakazi wa Segelea yupo na kaachishwa kazi na shirika la CCM.. hakuna sababu Chadema wasimpe kazi unless sababu zenyewe zitokane na utovu wa adabu au criminal record. Kinyume cha hapo kama ni mzuri na anaweza kuongoza isipokuwa kumetokea rabsha za unafiki kumuengua, Chadema wanaweza kumtumia mtu huyo (kuimpa ajira) kufika wanakotaka kufika.
Ila kitu kimoja Chadema hawawezi kukifanya.. Chadema hawawezi kuwapa hawa jamaa wadhifa wa juu kukiongoza CHAMA. Yaani kama lile swali lako linalohusiana na kumpa mgeni Uaskofu. Kiongozi yeyote wa Chama ni lazima awe amebobea siasa za chama na kuaminiwa zaidi na sio swala la Ubunge au Udiwani kwani nafasi hizi zinagombewa na mtu yeyote mwenye kufikiri anaweza kushawishi na kushinda kura za popular.
Maadam hawa wageni wote hawashiki madaraka ya juu ya chama sioni ubaya wowote kuwapa udereva wa bus ikiwa wao wataweza kuwafikisha abiria wetu tunakotaka kwenda.
First off, uchaguzi nchini hauwapi ushindi wagombea wenye popular vote, unawapa ushindi wagombea waliopitishwa na vyama na kupata popular vote, big difference, so do not try to misrepresent that.
Ninachouliza ni kwamba, kama watu ni purist wa democracy kihivyo na wanataka watu wenye popular support bila chujio la chama, what is the point of having these parties? Kwa nini tusiviondoe vyama vyote na kuwashindanisha wagombea kama watu tu, na atakayepata popular vote awe mbunge, no chama no middleman's b.s ?
Chama kina umuhimu gani kama mnachojali ni popular vote na direct democracy? Next thing you know hata hii nayo mtasema si democracy iliyo direct enough, tutataka turudi kama Athens ya kale, nchi nzima iende Dodoma ku debate budget.
How do you like that now? Si unataka pure democracy bwana?
Democracy iliyo ordered ni lazima iwe na mipaka ya common sense, otherwise itakuwa anarchy. Na moja kati ya mipaka hii ni vyama kuwa na uwezo wa kumkubali au kumkataa mtu kutokana na sababu zake. Kama kuna wanachama wa chama hiki wanampenda sana huyu mtu wanaweza kukubali maamuzi ya chama au kuamua vingine (kuhama chama na huyu mtu etc).
At the end of the day, kama mnaamua kuwa na vyama, vipeni role ya ku play. Haina maana kuwa na vyama wakati maamuzi yote yanafanywa directly na wananchi, kama ni hivyo - tunataka direct democracy- ondoeni vyama vyote, wananchi waamue directly kwa kuwashindanisha watu.
Halafu assertion yako ya ku distinguish uongozi w chama na ubunge katika context ya upinzani bongo sasa hivi ni laughable.Vyama hivi visivyo na visibility, mbunge wa chama ni kiongozi wa chama tayari, ataenda bungeni kutetea sera za chama sasa sijui una maana gani hapo.