CHADEMA, Jeshi la Polisi na Nipashe; taarifa hizi zilizosambaa mitandaoni zinawahujumu

CHADEMA, Jeshi la Polisi na Nipashe; taarifa hizi zilizosambaa mitandaoni zinawahujumu

Kuna taarifa zilizosambaa mitandaoni leo kuwa zaidi ya Askari 10 wakiwa na silaha za moto walikuwa wamezingira Ofisi za CHADEMA Mbeya ambako kulikuwa na Kikao cha Ndani cha BAWACHA! Taarifa hizi ziliripotiwa na NIPASHE na kusambaa katika mitandao ya kijamii. Ni kawaida yetu kutaka kujiridhisha na jambo lo lote kabla ya kulipazia sauti!

Katika kutaka kujiridhisha, Ofisi ya Haki ya Askofu ilimtafuta Mwenyekiti wa BAWACHA Jimbo la Mbeya, Mama Mwakimomo ambaye amekataa kuwepo kwa tukio hilo. Alipotafutwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mheshimiwa Joseph Mwasote (China) ambaye naye amekataa kuwepo kwa tukio hilo. Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA Mbeya, Mzee Kimariyo amesema kuwa yeye hana taarifa za tukio hilo.

Mtandao wa NIPASHE ambao ndio ulikuwa chanzo cha taarifa hizo, ulipotembelewa majira ya Saa 9 Alasiri haukuwa na habari hiyo! Je, NIPASHE waliripoti tukio hilo kisha wakaifuta muda mfupi baada ya kugundua kuwa habari ile haikuwa ya kweli? Kama ni hivyo, kufuta sio suluhisho, suluhisho ilikuwa ni kwa NIPASHE kutokoea hadharani na kukanusha habari ile? Kama siyo NIPASHE walioripoti taarifa ile, ni nani basi hao wanaotumia jina na nembo ya NIPASHE kwa ajili ya kuleta taharuki katika jamii? Watu hao wanapaswa kusakwa na Jeshi la Polisi na NIPASHE wenyewe!

Je, kuna watu ndani ya CHADEMA Mbeya ambao wanaweza kuwa ndio chanzo cha kuleta taharuki katika jamii? Kama ni hivyo, watakuwa wanafanya hsyo kwa manufaa ya nani na ili iweje? CHADEMA kinatakiwa kufanya uchunguzi wa kina kujiridhisha kuwa watu hao hawatoki ndani yao, wakiwagundua wanapaswa kuwachukulia hatua! Je, ni watu wasioitakia mema CHADEMA? Je, ni watu wanaotaka kudhoofisha sauti za kutetea haki hivyo wanabuni taarifa za uwongo ili siku zikiletwa taarifa za kweli watu wazipuzie?

Kwa vyo vyote vile, taarifa hizi zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu tukio hilo kama ni za kutungwa ni hujuma kwa CHADEMA na NIPASHE. Pia taarifa hizo kama sio za kweli zinalichafua Jeshi la Polisi pasipo sababu. Tunawashauri wahusika watafute njia ya kutengeneza mambo yao na taasisi husika zilizotajwa hapo juu, vinginevyo kuna hatari kubwa mbele yao inayowakodolea macho!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile MwamakulaView attachment 1992237
Naunga mkono hoja ,ila tumefikaje hapa, mbegu hii wameitengeza police wenyewe KWa kamata kamata ya Wanachama waCHADEMA, Sasa imekua Kama tamaduni na watu wamezoea ,so hata taalifa yoyote iwe ya kusingiziwa police vs Chadema ,au la jamii KWa Sasa itaichukulia ni kweli , jeshi la police ludini nyuma kujikwaa sio kuanguka
 
Back
Top Bottom