PreGE2025 CHADEMA jiandaeni, G55 imekuja kutoa changamoto ya uhuru na demokrasia ndani ya chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Honest mimi pia sielewi nn kinahitajika hapa kuhusu reforms awali nilivyoichukulia na joto lake muda unavyoenda ni tofauti kabisaaa.....

Awali ilikua hatutasusia uchaguzi ila hautafanyika..... Leo imekua tupo tayari kufanya uasi.
Acha upotoshaji usio na tija boss.
 
Ahsante mkuu wanachama wao pia hawalioni hili wameshupaza shingo wameamua kuyapa kipaumbele mawazo ya kiunaharakati wasijue siasa na unaharakati ni maji na mafuta. Mwisho G55 ataonekana alikua na mawazo bora kuliko wanavyoviita vikao vya chama
Juzi uchaguzi wa SM umenajisiwa, hao G55 walikuwa wapi, wanapata wapi imani sasa na huo uchaguzi mkuu kuwa utakuwa wa haki?
 
Acha upotoshaji usio na tija boss.
Mkuu naomba nielezee logic ya hii kauli "No Reform No election" niambie utekelezaji wake utafanyikaje kwa mazingira open ya kidemokrasia na yasiyo na mashaka ya uasi na kutumika kimawazo.... Mazingira yasiyo na uwezeshwaji kutoka mataifa ya nje na uratibu wenye ufanisi kwa ulinganifu wa muda na mawazo ya vikao vya chama
 
Mimi kama mfuatiliaji naona wenye shida ni wanaokataa kwenda na Lissu. Baada ya uchaguzi hiyo 50/50 walioshindwa walitakiwa kuendana na malengo ya Chama chao chini ya mwenyekiti mpya. Kung'ang'ania mpasuko au kususa ili wabembelezwe au maridhiano ni jambo la la kitoto. Lissu analeta KITU kipya ambacho kilikuwa hakijazoeleka katika siasa.
 
Juzi uchaguzi wa SM umenajisiwa, hao G55 walikuwa wapi, wanapata wapi imani sasa na huo uchaguzi mkuu kuwa utakuwa wa haki?
Sasa Mkuu leo ukisema CDM hashiriki uchaguzi nini matokeo yake?? Mpaka sasa G55 anasema anaendelea na taratibu za uchaguzi maana yake nini?? BUSARA iwaongoze viongozi wenu na hapa ndo muda wa wazee kustepup... CCM HAKUA MJINGA KUMUWEKA WASIRA PALE ALIPO ni mkakati wa kuendana na mgombea pekee kwa sababu haukukubalika kwa wananchama wote. HECHE na LISUU are of the same mind mother mkiwategemea mtapatwa na aibu. U need think tank kubwa haswa kipindi hiki.
 
Hakuna mabadiliko.hakuna uchaguzi. Chaguzi zetu sasa zimekuwa ni sehemu ya kuua wapinzai, kuwaacha na vilema vya maisha. Tutaendela kushiriki chaguzi za aina hiyo hadi lini? Kwanini wapinzani wageuke wahanga wa chaguzi za aina hiyo? Ni bora tupaze sauti zetu kuwa hizi si chaguzi bali ni uhayawani, tukiweza kuuzuia kwa nguvu ya umma tutazuia, tukishindwa kelele yetu na ujumbe wetu utakuww umefika.

Nikuulize, ww una maslahi gani na hizi chaguzi za kihayawani, na madhila yote wanayopitia wapinzani, hadi uone ni sahihi chaguzi ziendelee kufanyika kwa madhila haya dhidi ya wapinzani?
 
Mkuu tatizo kinatekelezeka hicho kitu kipya??? Watanzania unawajua lakini na kama unawajua utakubaliana na mimi kwamba modality ya kuiwezesha ajenda ya mabadiliko haitokua mpya.
 
Waendelee kushiriki kwenye chaguzi ambazo wala hawana uhakika wa kutangazwa washindi hata wakishinda? Waendelee kushiriki kwenye chaguzi zinazoua wafuasi wao na kuwaacha na vilema vya maisha? Au inatakiwa washiriki tu ili ww ufurahi?
 
Unaongelea nguvu ya umma ipi mkuu ya hawa watanzania vijana wa betting na kushinda mtandaoni??? Unadhani Serikali kuwaacha mfanye maandamano nchi nzima walikua wajinga??? Kile kilikua kipimo mkuu kilifanyiwa tathimini ya kina na kimeonesha TZ kutimiza malengo kwa maandamano haiwezekani...
Ndo mana nimekudikeza je utawashawishi vip watu kuepeuka vinasaba vya uasi na uratibu usio mashaka ya kutumika
 
Waendelee kushiriki kwenye chaguzi ambazo wala hawana uhakika wa kutangazwa washindi hata wakishinda? Waendelee kushiriki kwenye chaguzi zinazoua wafuasi wao na kuwaacha na vilema vya maisha? Au inatakiwa washiriki tu ili ww ufurahi?
Ajenda ya Mabadiliko imeibuka zaidi baada ya uchaguzi na hapo ikashika kasi..... Ingia kwenye uchaguzi shindana ukilenga kuipa ajenda hii muda.

Umedokeza umeeleweka kwa wananchi.. watake wakuchague waone madudu zaidi then ingia kwa nguvu zote kulenga 2029.

Unajipa muda mrefu kwa kuratibu mambo yako... Unapata muda wa kutoa makandokando yako yote ya ndani ya chama.... Unawapa wananchi kukuamini zaidi..
 
Kwa taarifa yako watu wana uwezo wa kufanya hicho unachoamini hakiwezekani, kinachotakiwa ni mazingira wezeshi tu. Zimbabwe hapo si Mugabe alikuwa anawatawala kama mabinti wa shule ya msingi, walipoingia barabarani mbona hakuamini?
 
Sijasema haiwezekani ila muda wa hilo bado mkuu sio mwaka huu na utaniamininkwenye hili muda ni rafiki mzuri... Watanzania wanapaswa kujengwa kwanza na sio kuja na wazo la kuwatoa ghafla
 
Hiyo ya kusema 2029, ikifika 2030 itasemekana hadi 2035. Wakati ni sasa, si lazima yakidhi utashi wako, lakini kitakachofanyika sasa kitapanda mbegu ya siku zijazo. Ni hivi, NRNE.
 
Sijasema haiwezekani ila muda wa hilo bado mkuu sio mwaka huu na utaniamininkwenye hili muda ni rafiki mzuri... Watanzania wanapaswa kujengwa kwanza na sio kuja na wazo la kuwatoa ghafla
Kama watu hawatakuwa tayari, si kosa la viongozi, wao wametekeleza wajibu wao. Watakapokwama wengine wataendelea, lakini wakati ni sasa na sio muda mwingine.
 
Hiyo ya kusema 2029, ikifika 2030 itasemekana hadi 2035. Wakati ni sasa, si lazima yakidhi utashi wako, lakini kitakachofanyika sasa kitapanda mbegu ya siku zijazo. Ni hivi, NRNE.
Sawa mkuu..... Ila pia nikwambie tu mbegu ya mabadiliko (ideology) haifanywi kama ambavyo CDM Wanaifanya kwa sasa.... Na mtu kama HECHE na LISSU hawawezi kuipanda hiyo mbegu kwa muda huu.
 
Sawa mkuu..... Ila pia nikwambie tu mbegu ya mabadiliko (ideology) haifanywi kama ambavyo CDM Wanaifanya kwa sasa.... Na mtu kama HECHE na LISSU hawawezi kuipanda hiyo mbegu kwa muda huu.
Ipandwe mara mbili, hata wasipofanikiwa lakini watakuwa wamejaribu. Hivyo hawana cha kujutia watakuwa wamefanya kwa uwezo wao.
 
Pumbavu , hata uyu ,mwanamke cathe ,alikua mtu mzuri tu, ila sasa amakua kinyago ghafla
 
M
Ahsante mkuu wanachama wao pia hawalioni hili wameshupaza shingo wameamua kuyapa kipaumbele mawazo ya kiunaharakati wasijue siasa na unaharakati ni maji na mafuta. Mwisho G55 ataonekana alikua na mawazo bora kuliko wanavyoviita vikao vya chama

Lissu kwanza sio mpya ni old stock aliyelelewa na kufanya kazi kwa muda mrefu ndani ya chama.
Pili mentor wa Lissu ni Mbowe,baada ya Lissu kuhangaika kwenye vyama tofauti bila kupata ubunge akaja Chadema, na Mbowe akamtengeneza hadi akapata ubunge.
Tatu Lissu kufanikiwa kwake kisiasa kulitegemea Mbowe na hata pale Lissu alivyopata majanga Mbowe ndio alikuwa dira hadi huyo Lissu mnaemuona hapa anadunda.

Mwenyekiti, pandikizi ni yupi?
Yule asietaka uchaguzi ili CCM ichukuwe 100% au yule anayetaka watu wapambane kwenye sanduku la kura ili wananchi wenyewe watetee haki yao ya kidemokrasia.
lakini tutapata wabunge japo tutafinywa tukiwa tunawaanda wananchi kuandaa katiba mpya.
Conclusion yawezekana wasaliti wa chama ni wale walio mstali wa mbele kupinga uchaguzi usifanyike.
 
Ipandwe mara mbili, hata wasipofanikiwa lakini watakuwa wamejaribu. Hivyo hawana cha kujutia watakuwa wamefanya kwa uwezol

Umemaliza mkuu watu kuna kitu hawakioni kabisaaa
 
Huku ccm tungekwisha wala vichwa. Sasa hivi wanakimbizana na TRA, takukuru na polisi.

Wamtafute malisaa mzee, alivyohoji upitishwaji wa mgombea noni kimemkuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…