Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Lojiki ya kufikiria ya Watanzania wenzengu mara nyingine inaniacha nashindwa kuwaelewa. Sielewi kwa nini suala la Mbowe na Lissu kugombea uenyekiti liwe jambo linalotishia uhai wa Chadema.
Tukirudi nyuma, hatuwezi kusema Nyerere aliacha uongozi kwa sababu aliishiwa fikra sahihi na ghafla Mwinyi akawa bora kuliko Nyerere. Mara nyingine kuwa na nafasi y uongozi na kuwapisha wengine ni jambo la ustaarabu tu, hasa ikiwa umekuwa katika nafasi hiyo kwa mika 5, au 10, au hata zaidi ya ishirini. Mara nyingine mabadiliko mazuri na makubwa yanakuja kwa sababu tu kuna macho mapya katika uongozi.
Na hii ni sababu mojawapo Chadema wamekuwa wakisisitiza sana kwa nini wanataka kuitoa CCM madarakani, kwamba CCM imekuwapo madarakani muda mrefu na wameanza kujisahau, kuna mambo wanachukulia Tanzania na Watanzania kwa ujumla for granted, na hivyo ni bora chama kingine kishike uongozi wa nchi, ili kuja na mawazo mbadala. Kwa hili nawaelewa sana.
Lakini sasa nisichoelewa, kama hii filosofia ya Chadema ya mabadiliko ya uongozi wa nchi yanayohitaji CCM iondoke na labda Chadema wapewe nafasi, kwa nini wao wenyewe wanashindwa kuitumia ndani ya chama chao katika suala la Tundu na Mbowe kuwania nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema?
Nawauliza Chadema, kama ni sawa Mbowe kuendelea uenyekiti zaidi ya miaka 20, kwamba amefanya kazi nzuri na kama amefanya makosa wanadamu wote tuna mapungufu hivyo aendelee tu, kwa nini sasa, kwa kutumia kanuni hiyo hiyo, si sawa CCM kuendelea kutawala mkijua wazi vyama vyote vina mapungufu? Kwani Nyerere aling'atuka kwa sababu Mwinyi alikuwa mbadala bora zaidi kwa Nyerere?
Kumbuka Mwinyi alisema akijilingnisha na Nyerere, yeye alijiona kichuguu n Nyerere mlima Kilimanjaro! Mnaweza kumona Mbowe kuwa Mlima Kilimanjaro, na Lissu kichuguu cha huko Sekenke, lakini filosofia ya maisha ni kukubali mabadiliko yanapostahili, hasa kama kutoyakubali kunaweza kuleta mtafaruku.