Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Unyama mliofanyiwa dunia nzima imeona na wala hakutakuwa na mshangao wowote iwapo mtakataa kuonewa tena , mmeuawa waziwazi , mmeteswa waziwazi , mmekamatwa hovyo hovyo , mmekatwa mapanga kwa namna walivyotaka , mmebambikwa kesi nyingi za kutunga , mmefungwa bila huruma , mmenyanyaswa kwa kiwango ambacho hakuna binadamu anayeweza kuvumilia
Hujuma za uchaguzi mnazofanyiwa nchi nzima na hasa kwenye Majimbo ya Chato , Mlimba , Kilombero na kwingineko itoshe kuwaamsha na kuanza KUMTUKUZA MUNGU kwa kukataa dhuluma kwa vitendo , ama hakika subira yavuta heri , hakuna tena nafasi ya kukubali kuonewa na watendaji wachovu wasiojua lolote kuhusu Demokrasia .
Mungu ibariki Chadema