CHADEMA: Katiba mpya si ya wananchi!

CHADEMA: Katiba mpya si ya wananchi!

Freshthinking

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
621
Reaction score
108
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimedai kushtukia mchakato wa Katiba Mpya nchini na kubashiri kuwa Katiba hiyo haitakuwa na tija kwani inalenga kuwalinda na kuwanufaisha watawala badala ya wanachi.
Chadema wamedai kuwa pindi kitakaposhika madaraka, chama hicho kitaamua haraka kuisuka upya Katiba hiyo ili iwape nguvu,mamlaka na masilahi wananchi.

Hayo yalisemwa kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ruaha wilayani Kilosa na Mwanasheria wa chama hicho, Mabere Marando.

Source: Mwananchi 26/12/2012

Bila ushabiki tujadili hii kauli.
>>> Hivi ina mantiki yoyote kwa sasa ilhali mchakato wa katiba bado unaendelea?
 
Ndugu masalia kama unafurahia jinsi tume ya katiba inavyochakachua maoni ya wananchi kuhusu katiba basi endelea na uasi wako.
Mimi nimeshajiandaa kupiga kura ya hapana dhidi ya katiba mpya ya tume, ninachoendelea kufanya kwa sasa ni kuwahamasisha wananchi wenzangu tujiandae kuikataa katiba ya tume kwa kuipigia kura ya hapana.

Kwakuwa bado unazongwa na usaliti ulioufanya dhidi ya chama ndo maana sasa umeanzisha mkakati wa kupinga kila kinachofanywa ama kusemwa na viongozi wetu ili kujaribu kuwin public sympathy!its too late kamanda safari hii huchomoki...
 
.

Huo mzimu unakutesa sana! Sasa CHADEMA walikwenda ikulu kukubaliana kitu gani na Rais?

Nilifikiri CHADEMA ingewaanda wananchi kutoa mawazo na kuyasimamia. Hiyo katiba ya CHADEMA itaandaliwa na na nani wakati huo?
 
Baeleze, waambie, tell them, Bhatebhi mwita weito.
 
Huo mzimu unakutesa sana! Sasa CHADEMA walikwenda ikulu kukubaliana kitu gani na Rais?

Nilifikiri CHADEMA ingewaanda wananchi kutoa mawazo na kuyasimamia. Hiyo katiba ya CHADEMA itaandaliwa na na nani wakati huo?

Kwanza mapendekezo mengi ya msingi ya Chadema hayakuzingatiwa, na wewe ulitakiwa kujua hilo kuliko mimi.

Pili tume inatembea na katiba yake tayari, haya maoni ya wananchi ni usanii tu ndio maana jaji warioba anakuwa mkali sana kwa watu wanaomkosoa yeye na tume yake namna wanavyoendesha zoezi la kukusanya maoni.

Tatu, watu wanaotoa maoni wasiyoyapenda tume wamekuwa wakiwatisha ama kuwazuia kuendelea kuongea.

Nne, ccm na mshirika wao cuf wameandaa maoni na kuwapa wanachama wao, sasa sisi hatufanyi upuuzi kama huo kwani tunataka katiba ya wananchi wote na si katiba ya wanachama wa Chadema pekee.
 
Mimi nimeshajiandaa kupiga kura ya hapana dhidi ya katiba mpya ya tume, ninachoendelea kufanya kwa sasa ni kuwahamasisha wananchi wenzangu tujiandae kuikataa katiba ya tume kwa kuipigia kura ya hapana.
Mwita,

Status quo walioshika madaraka walishaliona hilo mapemaaaaa..... Wameandika kwenye sheria ya Katiba mpya kifungu cha 5 cha Ibara ya 36 kwamba, wananchi mkijifanya ujuaji wa kupiga kura ya hapana huo ndio utakuwa mwisho wa mchakato, na Katiba itabaki hii hii!
 
Marando yuko sahihi kabisa.
Hakuna lolote la maana katika mchakato huu wa katiba mpya litazaliwa.

Kwanini CCM tunayo tayari katiba mpya halafu wakati huo huo tume bado inakusanya maoni?
 
Back
Top Bottom