CHADEMA: Kuahirishwa kesi ya Wabunge 19 wanasogeza muda

CHADEMA: Kuahirishwa kesi ya Wabunge 19 wanasogeza muda

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Wanachama wa CHADEMA, jana walionyesha kutoridhika na kukasirishwa na sababu za kuahirishwa kesi ya wabunge 19 wa viti maalumu waliofukuzwa uanachama wa chama hicho.

Kesi hiyo iliahirishwa kwa madai kuwa shahidi ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) Bara, Hawa Mwaifunga alifika mahakamani, lakini hakuweza kuendelea na ushahidi wake kutokana na kuugua.

Hivyo, Jaji Cyprian Mkeha anayeisikiliza aliiahirisha hadi Novemba 3, mwaka huu.

Hata hivyo, baadhi ya wanachama wa CHADEMA nje ya Mahakama walisikika wakilalamika kuwa sababu iliyotolewa haina ukweli, bali ni mbinu ya kuchelewesha kesi ili waendelee kubakia bungeni, madai ambayo yaliungwa mkono na baadhi ya viongozi wa BAWACHA.

Lakini kiongozi wa jopo mawakili wa wabunge hao, Ipilinga Panya alipinga madai hayo, akisisitiza kuwa mteja wake anaumwa na hata kwenda mahakamani jana walimshinikiza tu, “Hata CHADEMA wenyewe wanalifahamu tatizo lake.”

Walichokisema wanachama CHADEMA
Aliyekuwa mwenyekiti wa mpito CHADEMAJimbo la Segerea, James Haule alisema hawezi kupinga kama kweli mtu anaumwa. “Hii inawezekana kuna suala la kuvuta muda tu, kwa sababu, ilipoahirishwa kesi Oktoba 13, waliomba itajwe Novemba 4, wakakataliwa. “Lakini leo imerudi ileile tarehe iliyokataliwa, hiyo ndio inatia mashaka kwamba huenda sababu ni ya kutungwa,” alisema.

Maoni hayo pia yameungwa mkono na Mwenyekiti wa Bawacha mkoani Tabora, Monica Ncharo aliyesema kuwa alivyomwangalia Mwaifunga hadhani kama ni mgonjwa.

“Sisi tumemkuta pale ni mzima anatembea, anaongea na wenzake. Sidhani kama ni sahihi kesi kama hii ikaahirishwa maana anaonekana ni mzima kabisa. Nadhani huo ni mchezo wa kuchelewesha muda ili waendelee kuwepo bungeni,” alisema Monica.

Naye Katibu wa Bawacha Mbeya, Lucy Ngondo alihoji kama anaumwa kwa nini alifika mahakamani hapo.

Wakili afafanua
Akijibu madai hayo, wakili Panya alisema kuwa mteja wake anaumwa kweli na alitaka asifike mahakamani bali atume tu barua na vyeti vya daktari. “Tulimwambia ni vema awepo, haitakuwa busara kwa Mahakama tuahirishe kwa barua na vyeti vya daktari. Tulikuwa kwenye kizimba kesi ni ya kwenu, tafadhali njoo iahirishwe ukiwepo. Na hata kesho atakuwa Aga Khan kwa ajili ya kuendelea na matibabu.”

Alisema kuwa tatizo hilo ni la muda mrefu tangu mwaka 2019, ambapo alilazwa juma zima katika Hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya matibabu ya mgongo.

“Hata CHADEMA na hasa hao BAWACHA wanalijua na hata viongozi wa CHADEMA wanajua huwa ana tatizo la mgongo na huwa hasafiri muda mrefu,” alisema wakili Panya. Alisema kuwa hata alipoitwa ofisini hapo alielezea na akamuuliza wakili Kibatala kama amesahau kuwa alilazwa hospitalini hapo wiki nzima wakawa wanakwenda kumuona, lakini Kibatala akacheka tu.
 
Chadema badala ya kupambania haki za watanzania, matokeo yake wako wanashitakiana na wabunge wao wanao wanaotetea maslahi ya chama Chao.

Nashauri chadema waachane na hii kesi matokeo yake wajikite kukijenga chama Chao.

Na Jao wabunge waache waendeleza na kazii Yao, na pia chama kiazimie kuwasamehe majembe hayo yachape kazii ILI chama kisongembele na kufanya mikakati minginee. Kushinda mahakamani na WANACHAMA wako hii haileti afyaa.

Chadema kutaneni na WANACHAMA wenu, Kisha sameheaneni na kumtambua hamtaongoza malaika wa mbinguni wasio na makosaa.

Futeni kesi zote mahakamani peaneno mikono, jengeni upya chama. Kumbukeni suluhisho la mapambano kama hayo Huwa hayanamshindi kamili. Niushauri wangu tuuu.

Asanteni
 
Chadema badala ya kupambania haki za watanzania, matokeo yake wako wanashitakiana na wabunge wao wanao wanaotetea maslahi ya chama Chao. Nashauri chadema waachane na hii kesi matokeo yake wajikite kukijenga chama Chao. Na Jao wabunge waache waendeleza na kazii Yao, na pia chama kiazimie kuwasamehe majembe hayo yachape kazii ILI chama kisongembele na kufanya mikakati minginee. Kushinda mahakamani na WANACHAMA wako hii haileti afyaa. Chadema kutaneni na WANACHAMA wenu, Kisha sameheaneni na kumtambua hamtaongoza malaika wa mbinguni wasio na makosaa. Futeni kesi zote mahakamani peaneno mikono, jengeni upya chama. Kumbukeni suluhisho la mapambano kama hayo Huwa hayanamshindi kamili. Niushauri wangu tuuu. Asanteni
Wewe ni mjinga kama wajinga wengine.
Katiba ya chama lazima ilindwe.
 
Wewe ni mjinga kama wajinga wengine.
Katiba ya chama lazima ilindwe.
Kuilinda nikuchalangana na WANACHAMA wennzio na makesi yasiyoishaa? Hivi chadema ikiachana na Jao wabunge 19 itapoteza mvuto wakee?? Chama kijikite kujenga WANACHAMA wapya kulikokushinda mahakamani na kutumia garama za bule ambazo zingefanya mambo mengine Kwa MAENDELEO ya chama.
 
Kama huyo ameumwa kwanini wasingebadilisha aende kuhoji mwingine?

Kuna uzembe umefanyika.
 
Kuilinda nikuchalangana na WANACHAMA wennzio na makesi yasiyoishaa? Hivi chadema ikiachana na Jao wabunge 19 itapoteza mvuto wakee?? Chama kijikite kujenga WANACHAMA wapya kulikokushinda mahakamani na kutumia garama za bule ambazo zingefanya mambo mengine Kwa MAENDELEO ya chama.
Kabla hujailaumu chadema mlaumu yule zumwi aliyeharibu nchi na kuwagawa watanzania vipande vipande
 
Chadema badala ya kupambania haki za watanzania, matokeo yake wako wanashitakiana na wabunge wao wanao wanaotetea maslahi ya chama Chao. Nashauri chadema waachane na hii kesi matokeo yake wajikite kukijenga chama Chao. Na Jao wabunge waache waendeleza na kazii Yao, na pia chama kiazimie kuwasamehe majembe hayo yachape kazii ILI chama kisongembele na kufanya mikakati minginee. Kushinda mahakamani na WANACHAMA wako hii haileti afyaa. Chadema kutaneni na WANACHAMA wenu, Kisha sameheaneni na kumtambua hamtaongoza malaika wa mbinguni wasio na makosaa. Futeni kesi zote mahakamani peaneno mikono, jengeni upya chama. Kumbukeni suluhisho la mapambano kama hayo Huwa hayanamshindi kamili. Niushauri wangu tuuu. Asanteni
Una akili timamu kweli? Unaona ni halali hao kuendelea kuwa Wabunge kwenye ncni huru inayoheshimu Katiba yake na haki za binadamu? Hata kwenye sheria nyingine za nchi KUGHUSHI ni kosa la jinai.
 
Kuilinda nikuchalangana na WANACHAMA wennzio na makesi yasiyoishaa? Hivi chadema ikiachana na Jao wabunge 19 itapoteza mvuto wakee?? Chama kijikite kujenga WANACHAMA wapya kulikokushinda mahakamani na kutumia garama za bule ambazo zingefanya mambo mengine Kwa MAENDELEO ya chama.
Kimejikita katika kujenga chama kwa kukataa dhuluma na udhalimu wa ccm.
 
Una akili timamu kweli????Unaona ni halali hao kuendelea kuwa Wabunge kwenye ncni huru inayoheshimu Katiba yake na haki za binadamu????Hata kwenye sheria nyingine za nchi KUGHUSHI ni kosa la jinai.
Sasa unauhakika mtapata mwafaka wa hiii kesii?? Achaneni nao, jengeni chama Kwa namna nyingineee. Zaidii mtatumia fedha zenu za buree tuuu ambazo zingefanya mambo muhimu ya chamaaa
 
Kabla hujailaumu chadema mlaumu yule zumwi aliyeharibu nchi na kuwagawa watanzania vipande vipande
Kwahiyoo nanyie mumekubali aendelee kuwatafuna na huku mkijua hiloo?? Kama mnajua Hilo, yanini kushinda mnajihangaisha kumbe tatizo mnalifahamu?
 
2025 jukumu inatolewa hapo ndipo ujue kufeli school of law Ni siyo ajali
 
Sasa unauhakika mtapata mwafaka wa hiii kesii?? Achaneni nao, jengeni chama Kwa namna nyingineee. Zaidii mtatumia fedha zenu za buree tuuu ambazo zingefanya mambo muhimu ya chamaaa
Tupate tusipate hamna shida ila tumeonyesha uzalendo wa hali ya juu na kuwaonyesha ccm kuwa hiki wanachokifanya kwa sasa kuhusu hao wabunge 19 si sahihi na kuna siku hili ni jipu lao wenyewe,wasidhani wanawakomoa Chadema bali wanaikomoa Tanzania iliyo huru kuwa Tanzania ya wajinga na wapumbavu.Jambo liko wazi kisheria,kifkra,kimtazamo na kiraia kuwa mbunge atatokana na chama cha siasa au atateuliwa na rais,kama rais aliona kuwa Bunge halitanoga bila kuwa na wapinzani,alikuwa na mamlaka ya kuwateua yeye,lakini kilichofanyika ni upumbavu tu wa akina Ndugai,Magufuri,Mahera na Biswalo kuhalalisha haramu kuwa halali.
Tujifunze kutenda mema kwa wote,kutii sheria za nchi tulizojiwekea kwa mujibu wa sheria,kudumisha utamaduni wetu wa umoja na mshikamano,kuenzi mazuri yaliyoanzishwa na waasisi wa taifa hili,tuepukana na mambo ya Rwanda,Uganda,Burundi na DRC ili tuweze kufaidi matunda ya uhuru wetu.
 
Back
Top Bottom