Tupate tusipate hamna shida ila tumeonyesha uzalendo wa hali ya juu na kuwaonyesha ccm kuwa hiki wanachokifanya kwa sasa kuhusu hao wabunge 19 si sahihi na kuna siku hili ni jipu lao wenyewe,wasidhani wanawakomoa Chadema bali wanaikomoa Tanzania iliyo huru kuwa Tanzania ya wajinga na wapumbavu.Jambo liko wazi kisheria,kifkra,kimtazamo na kiraia kuwa mbunge atatokana na chama cha siasa au atateuliwa na rais,kama rais aliona kuwa Bunge halitanoga bila kuwa na wapinzani,alikuwa na mamlaka ya kuwateua yeye,lakini kilichofanyika ni upumbavu tu wa akina Ndugai,Magufuri,Mahera na Biswalo kuhalalisha haramu kuwa halali.
Tujifunze kutenda mema kwa wote,kutii sheria za nchi tulizojiwekea kwa mujibu wa sheria,kudumisha utamaduni wetu wa umoja na mshikamano,kuenzi mazuri yaliyoanzishwa na waasisi wa taifa hili,tuepukana na mambo ya Rwanda,Uganda,Burundi na DRC ili tuweze kufaidi matunda ya uhuru wetu.