Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema chama hicho kitaanza rasmi operesheni ya mikutano ya hadhara nchi nzima mwezi huu, ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kisiasa na kijamii inayolenga kuhamasisha mabadiliko ya Katiba pamoja na kudai uhuru wa mwanasiasa Tundu Lissu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 02, 2026 wakati akisoma maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA, Mnyika amesema operesheni hiyo itajulikana kama Operesheni Katiba Mpya, Free Tundu Lissu, na itafanyika kwa awamu mbili.Amesema awamu ya kwanza itahusisha kanda za Serengeti, Victoria na Kaskazini, na inatarajiwa kuanza wiki ya tatu ya mwezi Mei mwaka huu.
Ameongeza kuwa mikutano hiyo ya hadhara inalenga kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kudai Katiba mpya pamoja na kusimamia haki na demokrasia nchini.
Katika maazimio hayo, Kamati Kuu ya CHADEMA imesisitiza kuwa operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi za chama kuendelea kushirikiana na wananchi katika kudai mabadiliko ya msingi ya kisiasa na kiutawala nchini.