CHADEMA kuhodhi vuguvugu la kudai Katiba kana kwamba mahitaji ni yao pekee yanadhoofisha upatikanaji wa Katiba Mpya

CHADEMA kuhodhi vuguvugu la kudai Katiba kana kwamba mahitaji ni yao pekee yanadhoofisha upatikanaji wa Katiba Mpya

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Ukweli ndio huu. Maana wanataka kuonyesha umma kuwa mpambano wa kudai katiba mpya ni wao tu.

Na kwa mantiki hii inakuwa inaonyesha kuwa wanataka katiba mpya ili wapate madaraka tu na wala sio kwa ajili ya watanzania wote.

Kwanini hatusikii juhudi zao kuwapigia debe, waalimu, wakulima na wavuvi juu ya kuwa na katiba mpya itakayonufaisha makundi kama haya?

Wao ni juu ya kupata tume huru na mkakati wa kupata wabunge ili waweze kupata mkwanja wa kuendesha chama.

Hii inasababisha mchakato wa kudai katiba mpya kutokupata sapoti ya makundi yote hasa yasiyo na utashi wa kisiasa.
 
Lipumba na CUF wanataka katiba mpya sasa.

Mbatia na NCCR wanataka katiba mpya sasa.

Watanzania kwa mujibu wa twaweza 2017 hawa hapa:

TWAWEZA: Katika Watanzania watatu, Wawili wanataka Katiba Mpya

Kwani huwajui wanaohaha kuichelewesha katiba mpya? Ni hawa hapa:

IMG_20220329_190143_908.jpg

Ila hawataweza.

Hiyo ndiyo habari yenyewe.
 
Katiba Mpya imebeba mstakabali wa Mambo yote pamoja na Walimu.

Mfano mimi katika maoni niyotoaga ktk Rasimu ya Mzee Warioba niwazungumzia Wamasai juu ya kuhamishwahamishwa tukumbuke kokote waendako huondolewa na kuonekana hawastahili kuwepo pale wapoliona jibu la kupata malisho.

Na nikasema huko tuendako itatokea historia kama ya Wanaizrael ya kuitafuta asili yao ambayo ninaamini haitatuacha salama na umoja
 
Na maoni yangu niliyatoa mbele ya Profesa Kabudi pamoja na team yake

Kwa hiyo Katiba ni ya muhimu kuliko huduma zote Mku
 
Chadema wanataka katiba ili wapate vyeo waanze ulafi wa Mali za wananchi, huwasikii wanaongelea mwananchi wa kawaida.
 
Huwa sielewi watu kama huyu mtoa mada kuilamu Chadema..

Chama gani kingine kimetoka hadharani kudai Katiba au hata wewe umefanya nini kuidai Katiba Mpya

Iko hivi Chadema wanafanya kwa ajili ya Taifa sio chama chao sasa mbona mnakuwa wagumu sana kuelewa

Chagu wa Malunde mnakera sana Chadema waliwafanya nini?

Kama hutaki kuungana na Chadema idai Katiba kivyako kwani umekatazwa....
 
Mbowe ndiyo mpinzani pekee wa kuaminika aliyebakia kwa sasa.
 
Katiba Mpya imebeba mstakabali wa Mambo yote pamoja na Walimu.
Mfano mimi katika maoni niyotoaga ktk Rasimu ya Mzee Warioba niwazungumzia Wamasai juu ya kuhamishwahamishwa tukumbuke kokote waendako huondolewa na kuonekana hawastahili kuwepo pale wapoliona jibu la kupata malisho.
Na nikasema huko tuendako itatokea historia kama ya Wanaizrael ya kuitafuta asili yao ambayo ninaamini haitatuacha salama na umoja
Mimi nilichangia Katiba Ibainishe Haki za Mzawa!

Kama Katiba ya India ilivyo bainisha kwamba India Is For PURE Indians!
 
Ccm ni janga la Taifa, huu upuuzi unapatikana Lumumba tu.

Unawezaje kutetea wakulima na walimu wakati katiba inampa mamlaka Raise kumdhuru Kila atakae inua mdomo kuisema vibaya serikali!!!.

Ccm wapo Bungeni umesikia hata mmoja ameongelea kupanda kwa bei za bidhaa??,

Chadema wakidai katiba ccm mdai haki za raia na unafuu wa maisha na ndugu yenu Act adai tume HURU.
 
Kama CCM na Uongozi wake, CCM chama tawala na serikali yake kwa makusudi wanaacha ombwe la kuonesha njia kupata Katiba mpya wakijua wananchi wanaitaka, kwa nini CDM wasijaze hilo ombwe?

Umamuzi ni wa CCM ama wachukue uongozi wa kuwapatia Watanzania Katiba mpya au waachie sifa hiyo iende kwa CDM/Upinzani na wanaharakati.
 
Back
Top Bottom