CHADEMA kujazana mahakamani ili kurekodi mwenendo wa kesi kwa lengo la kupotosha jamii na kutengeneza chuki dhidi ya mahakama siyo sawa

Kwa nchi za wenzetu hiyo kesi kwa masirahi ya umma ingekuwa inaonyeshwa live runingani Ila hapa kwetu tunatakiwa tuachane nayo tukafanye kazi,Kama bunge tu jaturuhusiwi sembuse kesi!
 
Sioni kama kulikuwa na uwongo wowote kwa wanaoripoti. Toka kesi ianze, wanapowasilisha vielelezo, watoaji wa taarifa huwa wanasema, "shahidi anasoma maelezo yaliyopo kwenye vielelezo". Ujue shahidi anaposoma maelezo anaenda haraka sana, tofauti na anapohojiwa ambapo maelezo anayoyatoa, anaenda taratibu ili jaji aweze kuandika. Maelezo ya kwenye vielelezo, jaji haandiki maana maelezo atayakuta kwenye vielelezo.
 
Tunashukuru wewe umetuletea jumbe hizo kwa ukamilifu wake.

Sasa tujadili kwa maslahi ya taifa letu kama wananchi huru,

Kwako wewe kuna mahali ktka jumbe hizo umeona neno hata moja linaloashiria kuwa walikuwa wakipanga ugaidi? Maana jumbe hizi ndiyo msingi mkuu wa ushahidi tulioambiwa na Siro kuwa upo ushahidi wa kutosha.

Kama hii Ndiyo msingi wa ushahidi basi, kuna shida ktk jeshi la polisi.
 
Wewe anzi yako utupe update za mahakamani ila yule anajitahidi simjui hanijui ila kongole kwake
 
Mkuu hivi uko CHADEMA ulinzi wa mtu mkubwa kama Mbowe si ungetangazwa wazi tu

sijakuelewa mkuu unaweza kurudia tena kama hutajali?
Mbona huwa hatuoni mkitangaza nafasi za kazi za usalama wa taifa wanaomlinda Rais?
Ushawahi kujua namna wanavyorecruit hao watu?
The same reason,Mbowe akitangaza nafasi za walinzi binafsi,TISS haishindwi kupenyeza watu wao nao wakaombe!
Kama ujuavyo Kwa nchi hii,vyombo vya Dola vipo kuihudumia na kuipambania CCM!
 
Hii hawaiandiki wala hawapendi ijulikane hivyo

Wao wamekariri neno...moja tu Mchongo.

Ahsante@comte kwa kunyoosha mistari.

Kwenye ili Updates yao wamekiruka hiki kipengele chote kinachomhusu Mbowe !
 
Mleta mada sikui umewaza ninini hadi kuweka hili bandiko!
Watu kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya mpendwa wao itatengenezaje chuki dhidi ya mahakama?
Nilitamani kuona andiko lako kuelezea lakini siaona!
 
Mbona mwandishi anarukaru. Hii hapa iko mwananchi ila hapa hamna

Taarifa ya Uchunguzi:
Bado katika haya maelezo yote sijaona kiashiria chochote kile cha ugaidi! Zaidi tu ya mawasiliano baina ya watu wawili katika kusafirisha watu kutoka eneo moja kwenda lingine.

Hakuna sehemu imetolewa sababu ya kuwasafirisha! Zaidi tu ya mvutano! Watuhumiwa na upande wa utetezi kwa ujumla wakisema walisafirishwa kwa ajili ya VIP proyection, huku upande wa serikali/mashtaka wakilazimisha ni kwa sababu za kigaidi.

By the way, kama hii kesi haina harufu ya mchongo kwa namna yoyote ile, mbona huyo Dennis Urio haonekani mahakamani? Au zamu yake ya kutoa ushahidi kwa upande wa mashtaka bado haijafika?
 
Haihitaji uwe wakili msomi kugundua hii kesi siyo ya ugaidi wala uhujumu uchumi. Hii ni kesi ya kupotezeana tu muda kupitia vyombo vya dola.

Maelezo yote yamejaa stori za kawaida, tena za watu waliosafirishwa kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kumlinda mtu aliye mtumia mtu wa kati kuwatafuta.

Ni aibu kwa serikali kupoteza hela za walipa kodi kwa mambo ya kipuuzi kama haya.
 
Mkuu sijui mengine mnayatoa wapi- hoja yangu siyo tujadili kuhusu nani mkweli na ni nani muungo. Hoja yangu ni kwa nini mleta update alete taarifa nusunusu- anaficha nini? Ni kitu gani hataki tukijue? na KWA NINI?
 
Hii hawaiandiki wala hawapendi ijulikane hivyo

Wao wamekariri neno...moja tu Mchongo.

Ahsante@comte kwa kunyoosha mistari.

Kwenye ili Updates yao wamekiruka hiki kipengele chote kinachomhusu Mbowe !
Mkuu wakumbuke wapenda ukweli bado tupo humu-siyo CHADEMA siyo CCM ila wapenda UKWELI
 
Mkuu sijui mengine mnayatoa wapi- hoja yangu siyo tujadili kuhusu nani mkweli na ni nani muungo. Hoja yangu ni kwa nini mleta update alete taarifa nusunusu- anaficha nini? Ni kitu gani hataki tukijue? na KWA NINI?
Basi jibu ni hili hapa; Analeta nusunusu hizo taarifa kwa sababu ya utashi wake tu. Maana amejitolea, na hatumlipi. Hata akiamua kutoleta kabisa, bado hatuna cha kumfanya. Sisi wengine tunamshukuru hata kwa hicho kidogo anacho tuletea humu jukwaani.
 
Sikujua- na yaho ndiyo madhara ya kutaka kuishi Kidola wakati huna dola
 
Mimi siyo mahakama wala hakimu- wewe baki na hukumu yako ila ikitolewa yenyewe na wenyewe usilie
 
Basi jibu ni hili hapa; Analeta nusunusu hizo taarifa kwa sababu ya utashi wake tu. Maana amejitolea, na hatumlipi. Hata akiamua kutoleta kabisa, bado hatuna cha kumfanya. Sisi wengine tunamshukuru hata kwa hicho kidogo anacho tuletea humu jukwaani.
Na unaona ni sawa?
 
Basi jibu ni hili hapa; Analeta nusunusu hizo taarifa kwa sababu ya utashi wake tu. Maana amejitolea, na hatumlipi. Hata akiamua kutoleta kabisa, bado hatuna cha kumfanya. Sisi wengine tunamshukuru hata kwa hicho kidogo anacho tuletea humu jukwaani.
Na unaona ni sawa?
 
Sikujua- na yaho ndiyo madhara ya kutaka kuishi Kidola wakati huna dola
Hayo mambo yapo!Mbona kina mond,harmonize Wana walinzi kibao tu!!
Issue ni kuwa Mbowe ni mwanasiasa Tena mpinzani!Kuwa mpinzani imara nchi hii ni risky sana!
 
Mleta mada sikui umewaza ninini hadi kuweka hili bandiko!
Watu kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya mpendwa wao itatengenezaje chuki dhidi ya mahakama?
Nilitamani kuona andiko lako kuelezea lakini siaona!
Mkuu kwa uelewa wako hutakaa uelewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…