PreGE2025 CHADEMA kujiondoa kwenye uchaguzi ni kama nchi nzima kususia uchaguzi wa nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwa sasa CDM wanaongea lugha ya wananchi rasmi,si Ile ya 2015 kutufanyia maigizo.
Sisi tunaunga mkono HAKI
 
Yeah, sio watu wote watakosekana wa kupiga kura ila katika uhalisia chama cha upinzani kikuu kujiondoa kwenye uchaguzi iitapelekea watu wengi kujiondoa kwenye uchaguzi pia kwasababu hata mgombea wa chama tawala hakubaliki na wananchi.
Kwani anategemea kura? Kumbuka pesa nyingi sana za umma zinaibiwa, na sehemu yake zitatumika kuhonga vyombo vya habari, na chawa ili watoe hamasa kwa watu kwenda kupiga kura. Ifahamike kuna kundi kubwa la wajinga, hivyo wao wanafuata chochote kwa mazoea, usitegemee wengi wana uelewa wa mambo kama sisi.

Sasa subiri uone ni kwa kiwango gani taasisi nyingi za nchi hii zilivyoharibika, utashangaa wapiga kura watakuwa chini ya milioni saba, lakini atatangazwa kupata kura 15m+, na watasema kashinda kwa 95% na watajitokeza watu wengi kushangilia huo uhuni!
 
Pamoja na hayo hali inaweza kuwa tofauti kidogo tofauti na chaguzi zilizopita za janja janja
 
Mpaka hapa mambo yashakuwa magumu kwa kijani
 
Tuambie hapa wagombea wa ngaza za juu kupitia CHADEMA ambao wangeweza kushinda uchaguzi
Hatuongelei nani anaweza kushinda, tunazungumzia integrity ya uchaguzi. Kuna watu walikuwa wanapotosha kutufanya hatukuona upuuzi uliofanyika kwenye uchaguzi wa 2020, kwa kusema hakukuwa na wa kumshinda Magufuli, lengo ilikuwa ni kutupoteza maboya tusiongelee ukweli wa upuuzi uliofanyika kwenye uchaguzi ule. Ni sawa na mwanafunzi mwenye akili sana akutwe na majibu ya maswali kwenye chumba cha mtihani, kisha useme kwa kuwa alikuwa na akili lazima angefaulu tu.
 
Huku mtaani kwangu cjawah kuona wakiongea khs uchaguzi, chadema kususia uchaguzi, vyama vingine kushiriki uchaguzi, kwa ufupi n kila mtu ana pambana na maisha yake.
Hata kama CHADEMA wangeshiriki uchaguzi bado kila mtu angeendelea kupambana na maisha yake.nimeshuhudia hata wapinzani ktk chaguzi wanauza majimbo,kata wanasepa yanabaki wazi CCM wanapita na kupelekea malalamiko kwa wananchi
 
Pamoja na hayo hali inaweza kuwa tofauti kidogo tofauti na chaguzi zilizopita za janja janja
Hadi sasa kitendo cha cdm kujitoa muhanga kwa kugoma kusaini kanuni za uchaguzi wa kihuni kumeshatia doa uchaguzi mzima. Ndio maana unaona hujuma za wazi za dola kww cdm. Na hata ukienda kuona idadi ya watu wanaojiandikisha/kuhakiki kupiga kura ni duni sana.
 
Izo movie wanazo Fanya Chadema za kususia uchaguzi, CUF walisha zifanya tena wakiwa katika ubora wa wa hali ya juu kama Chama, lakini hazikuleta Matokeo chanya.
Kuna mambo Chadema wanatumia Nguvu wakati tayari Matokeo ya ayo mambo yanafahanika maana tayari yalisha fanyika.
Bila ubunifu na akili hakuna mabadikiko, yaani jambo lililo fanywa miaka ya nyuma na wenzako na lika feli wewe Leo 2025 unalirudia!!!
 
Dunia nzima imenyooshea vidole samia na anaonekana hakubariki analazimisha.
 
Criteria zipi umezitumia kujenga hoja Yako kwamba watanzania hawataenda kupiga kura kisa chadema kugomea uchaguzi?
 
Uamuzi wa CHADEMA kujiondoa kwenye uchaguzi ni sawa na kususia uchaguzi wa nchi nzima, kwani bila wananchi kupiga kura, hakuna rais anayeweza kujitangaza kwa haki. Kitendo hicho kinaweza kupelekea machafuko na mageuzi, maana rais bila ridhaa ya wananchi ni muhalifu anayekanyaga haki za Watanzania, na mzozo utakaoibuka hautakuwa mdogo.
hizi takwimu kuwa hakuna mtu atakwenda kupiga kura huwa mnazitoa wapi?
 
Na kwa kifupi hao wafu wa mtaani kwako hawana impact ni kama watu, ndo wale Kenyata aliwaongelea, Si unaishi lake Eyasi kwa wa Hadzabe? Kwa Chaaba na Duduqe
Ww ukipiga kura kuna faida & hasara gani?
Ww usipopiga kura kuna faida & hasara gani?
 
Chama kikuu cha upinzani ni ACT wazalendo,wana mpaka makamu wa Rais.
 
Huu ndio ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…