CHADEMA kumshitaki Makonda kwa uvunjifu wa sheria

hiyo kali tena.unamaanisha jina sio lake alilosomoea?
by the way naungana na makonda kwa haya.
1. kuwaweka ndani maafisa ardhi hata kama ni kinyume cha taratibu maana dharau walioonyesha kwake ni kubwa sana. kukubaliana wakutane saa 2 halafu wao wanakuja saa5. hapana kwa kweli.
2. na hili la kubenea nakubaliana na makonda, maana kumuita kibaka ni lugha ya udhalilishaji iliyopindukia. hivi wewe ungeitwa kibaka ungekubali?

Nilikutana naye Koromije Misungwi Mwanza miaka ya 2000 enzi hizo akiitwa DAUDI Bashite. Sifahamu kivipi anaitwa Paul Makonda. Namfahamu in and out
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari tangu jana kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Ndugu Saed Kubenea aliwekwa chini ya ulinzi na kuamriwa kwenda kituo cha polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye inadaiwa hakutaka mbunge huyo azungumze na wananchi ambao ni Wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Took Garment, waliokuwa wamemuita mbunge huyo kwa ajili ya kumweleza matatizo wanayokumbana nayo kazini hapo, ikiwa ni pamoja na ujira kidogo na mazingira magumu ya kazi.

Aidha akitambua kuwa alichofanya matumizi mabaya ya dhamana ya uongozi, hivyo akakusudia kuficha umma usijue uovu huo, katika tukio hilo Makonda aliwaagiza polisi wakamate kamera za waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo wakitimiza wajibu wao wa kikazi na kitaaluma kwa jamii.

Katika hatua ya sasa, tunaomba kusema ifuatavyo;

1. Tukitambua kuwa mamlaka ya DC kuamuru watu kukamatwa yamefafanuliwa kisheria na kuwekewa mipaka yake ambayo Makonda amedhihirisha kuivuka katika nyakati tofauti sasa, Mkuu huyo wa wilaya hana mamlaka ya kisheria wala ya kisiasa kuhalalisha amri aliyoitoa ya kumkamata mbunge, tena aliyekuwa anatekeleza wajibu wake, tunamtaka DC Makonda amwachie Ndugu Kubenea mara moja huku tukitoa wito kwa mamlaka zilizomteua kumwangalia kwa makini kama bado anazo sifa za kuwa kiongozi wa ngazi hiyo.

2. Kwa kuwa amri hiyo si halali kwa sababu haina msingi wowote wa kisheria, tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kumuachia Ndugu Kubenea ili aendelee na uhuru wake huku akitekeleza wajibu wake wa kuwawakilisha wananchi wa Ubungo badala ya kumsumbua kwa mambo yasiyokuwa ya msingi.

3. Halikadhalika, Jeshi hilo liwarudishie waandishi wa habari vifaa vyao vya kazi vikiwa katika hali salama na bila athari yoyote ama ya vifaa vyenyewe au materials yaliyoko ndani yake.

4. Tunalitaka Jeshi la Polisi kutoa kauli ya kuwahakikishia usalama waandishi wa habari na vifaa vyao kila wanapotimiza wajibu wao kwenye matukio yanayomhusisha Makonda kwa sababu tayari ushahidi unaonesha anaweza kuwa tishio kwao binafsi na vitendea kazi vyao hususan pia wanapokuwepo polisi.

5. Kwa kitendo cha DC Makonda kuamuru kiongozi wa wananchi akamatwe bila kuwepo kosa lolote la kisheria, CHADEMA tutachukua hatua za kisheria dhidi ya DC huyo ili liwe fundisho kwake mwenyewe, wakuu wa wilaya wengine na utawala mzima wa Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli, ili watambue kuwa suala la kuongoza nchi kwa kuzingatia Haki, Katiba, Sheria na taratibu si suala la kupenda bali ni lazima kuzingatiwa kwa ajili ya amani na utulivu wa kweli.

Tutachukua hatua hizo huku tayari kukiwa na kumbukumbu za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBU) ambayo hivi karibuni ilimuonya DC Makonda na wakuu wa wilaya wengine na wakuu wa mikoa ambao wameanza tabia ya kuendesha nchi kwa amri ambazo hazina uhalali wowote zikiwa nje ya mamlaka yao ya kisheria kufanya hivyo.

Tuliamini angalizo hilo la THUB ambacho ni chombo huru cha serikali, lingeweza kuwa mwongozo sahihi kwa viongozi wa serikali na kwamba kosa la awali la Makonda kuwaweka mahabusu watumishi wa Wilaya ya Kinondoni walioko chini yake lingechukuliwa kama fundisho kwake, lakini bahati mbaya watawala wanaweka nta masikioni linapofika suala la haki za binadamu na uongozi bora.

Imetolewa leo Jumanne, Nov. 15, 2015 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

hakuna mipaka iliyovukwa na keshaachiwa kwa dhamana ila kesi ipo palepale... ni kosa kumdhalilisha mteule wa raisi mbele ya watu ! hata asingelikuwa mteule wa Rais ni kosa kutoa kauli chafu kwa mtu yeyoyte yule .. ni ukosefu wa Adabu...

Amri si halali kakwambia nani ..? wito wenu umesikika kapewa dhamana lakini kesi ipo palepale .... mahakama itaamua ..

vifaa walisharudishiwa walichokitaka ni ushahidi wa video wakati kubenea akiongea hayo maneno machafu

sidhani jeshi lina muda huu wa kupoteza, inajulikana Tanzania ni nchi huru ... vitendea kazi vilichukuliwa kama ushahidi.. inabidi muwauliza hao wandishi je hawajarudisha vifaa vyao .. kabla hamjakurupuka kutoa matamko

Mbunge anamipaka yake! kubenea sio Rais wa ubungo bali ni muwakilishi tu! kazi yake ni kukusanya maoni na matatizo ya wananchi wake na kuyapeleka serikalini...!! DC ni serikali ! ... mkae muwape semina elekezi wabunge wenu wapya mipaka yao ni ipi na kuheshimu mihimili mengine ...

CRA.P!

Mkuu toka lowassa anunue CDM umepotea jukwaani .. vipi..?! mnaogopa kula matapishi yenu maana mlimnadi ni fisadi miaka 5 !!... kubenea akatoa makala kwenye mwanhalisi "LOWASSA HASAFISHIKI"

hehehe!
 
Kesi iliishaje?
 
Nilikutana naye Koromije Misungwi Mwanza miaka ya 2000 enzi hizo akiitwa DAUDI Bashite. Sifahamu kivipi anaitwa Paul Makonda. Namfahamu in and out

Labda alinunua jina la kufanyia mtihani baada ya kufeli mtihani

Yes you are very correct. Baba yake alikuwa kamanda wa Sungusungu enzi hizo wanakijiji walikoma. Mnazifahamu mboko za Sungusungu?

Jamaa kaunga unga elimu sana,usikute alivyofeli form four ikabidi atumie jina la mtu.

Nilipigwa butwaa alipoteuliwa. Kujiridhisha nikampigia Mama yake akanithibitishia..Sishangai kinachotokea

Unataka kusema hilo jina LA Paul Makonda so lake

Fuatilieni kijiji cha Koromije Misungwi Mwanza mtaupata ukweli wote bila chenga kwa wanakijiji wa hapo

Atakuwa Ali...

Mmmmh!!! Kwa hiyo huyu ni Daudi Bashite a.k.a makonda.
Duh! Alifoji cheti nini au kajibadilisha

Funguka mkuu tumjue huyu kibaka aanikwe upuuzi wake. Pumbafu kabisa huyu dogo.

Umesahau Ya Lameck Madelu Baadae Akawa Mwigulu Nchemba?. Majizi Ya Vyeti Vya Watu Siku Zote Ni Mababe Mababe Tu Na Hayatumii Akili. Ipo Siku Daud Bashite aka Paul Makonda Atanyea Ndoo Kwa Upuuzi Huu.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari tangu jana kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Ndugu Saed Kubenea aliwekwa chini ya ulinzi na kuamriwa kwenda kituo cha polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye inadaiwa hakutaka mbunge huyo azungumze na wananchi ambao ni Wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Took Garment, waliokuwa wamemuita mbunge huyo kwa ajili ya kumweleza matatizo wanayokumbana nayo kazini hapo, ikiwa ni pamoja na ujira kidogo na mazingira magumu ya kazi.

Aidha akitambua kuwa alichofanya matumizi mabaya ya dhamana ya uongozi, hivyo akakusudia kuficha umma usijue uovu huo, katika tukio hilo Makonda aliwaagiza polisi wakamate kamera za waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo wakitimiza wajibu wao wa kikazi na kitaaluma kwa jamii.

Katika hatua ya sasa, tunaomba kusema ifuatavyo;

1. Tukitambua kuwa mamlaka ya DC kuamuru watu kukamatwa yamefafanuliwa kisheria na kuwekewa mipaka yake ambayo Makonda amedhihirisha kuivuka katika nyakati tofauti sasa, Mkuu huyo wa wilaya hana mamlaka ya kisheria wala ya kisiasa kuhalalisha amri aliyoitoa ya kumkamata mbunge, tena aliyekuwa anatekeleza wajibu wake, tunamtaka DC Makonda amwachie Ndugu Kubenea mara moja huku tukitoa wito kwa mamlaka zilizomteua kumwangalia kwa makini kama bado anazo sifa za kuwa kiongozi wa ngazi hiyo.

2. Kwa kuwa amri hiyo si halali kwa sababu haina msingi wowote wa kisheria, tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kumuachia Ndugu Kubenea ili aendelee na uhuru wake huku akitekeleza wajibu wake wa kuwawakilisha wananchi wa Ubungo badala ya kumsumbua kwa mambo yasiyokuwa ya msingi.

3. Halikadhalika, Jeshi hilo liwarudishie waandishi wa habari vifaa vyao vya kazi vikiwa katika hali salama na bila athari yoyote ama ya vifaa vyenyewe au materials yaliyoko ndani yake.

4. Tunalitaka Jeshi la Polisi kutoa kauli ya kuwahakikishia usalama waandishi wa habari na vifaa vyao kila wanapotimiza wajibu wao kwenye matukio yanayomhusisha Makonda kwa sababu tayari ushahidi unaonesha anaweza kuwa tishio kwao binafsi na vitendea kazi vyao hususan pia wanapokuwepo polisi.

5. Kwa kitendo cha DC Makonda kuamuru kiongozi wa wananchi akamatwe bila kuwepo kosa lolote la kisheria, CHADEMA tutachukua hatua za kisheria dhidi ya DC huyo ili liwe fundisho kwake mwenyewe, wakuu wa wilaya wengine na utawala mzima wa Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli, ili watambue kuwa suala la kuongoza nchi kwa kuzingatia Haki, Katiba, Sheria na taratibu si suala la kupenda bali ni lazima kuzingatiwa kwa ajili ya amani na utulivu wa kweli.

Tutachukua hatua hizo huku tayari kukiwa na kumbukumbu za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBU) ambayo hivi karibuni ilimuonya DC Makonda na wakuu wa wilaya wengine na wakuu wa mikoa ambao wameanza tabia ya kuendesha nchi kwa amri ambazo hazina uhalali wowote zikiwa nje ya mamlaka yao ya kisheria kufanya hivyo.

Tuliamini angalizo hilo la THUB ambacho ni chombo huru cha serikali, lingeweza kuwa mwongozo sahihi kwa viongozi wa serikali na kwamba kosa la awali la Makonda kuwaweka mahabusu watumishi wa Wilaya ya Kinondoni walioko chini yake lingechukuliwa kama fundisho kwake, lakini bahati mbaya watawala wanaweka nta masikioni linapofika suala la haki za binadamu na uongozi bora.

Imetolewa leo Jumanne, Nov. 15, 2015 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Kusema kweli Chadema mnaboa sasa.
 
Nilikutana naye Koromije Misungwi Mwanza miaka ya 2000 enzi hizo akiitwa DAUDI Bashite. Sifahamu kivipi anaitwa Paul Makonda. Namfahamu in and out
Hawa wanoonekana wakihojiwa na Zamaradi je ndio wazazi wake kweli? Mzee BASHITE na mkewe?
 
Back
Top Bottom