CHADEMA, kuongea na Mapambano huenda pamoja

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ni jambo la kheri kuwa CHADEMA itakuwa na ugeni mkubwa kesho. Uthibitisho thabiti kuwa upinzani siyo jinai tena.

Pongezi nyingi kwa Mama Samia Rais wetu kwa hili.

Hivyo basi itumike fursa hii vizuri kuendelea kuyaweka wazi yaliyo vipaumbele zaidi kwa maslahi ya watu. Mfano:

1. Katiba Mpya
2. Wanaoshikiliwa kwa figisu za kisiasa
3. Walioathiriwa kwa figisu za kisiasa wakiwemo waliokufa, kujeruhiwa au kupotea
4. Uchunguzi kamili na kuwajibishwa kwa waliohusika kwenye #3
5. Kuwahusu wale wadada 19 bungeni bila ridhaa ya chama
6. Nk.

Tujipange kwa ugeni huu na presentation za kistaraabu zilizoshiba.

Tanzania iliyo bora zaidi inanukia.
 
Ni jambo la kheri kuwa CHADEMA itakuwa na ugeni mkubwa kesho. Uthibitisho thabiti kuwa upinzani siyo jinai.

Pongezi nyingi kwa Mama Samia kwa hili.

Hivyo basi itumike fursa hii vizuri kuendelea kuyaweka wazi yaliyo vipaumbele kwa maslahi ya watu. Mfano:

1. Katiba Mpya
2. Wanaoishikiliwa kwa figisu za kisiasa
3. Walioathiriwa kwa figisu za kisiasa wakiwemo waliokufa, kujeruhiwa au kupotea
4. Uchunguzi na kuwajibishwa kwa waliohusika kwenye #3
5. Kuwahusu wale wadada 19 bungeni bila ridhaa ya chama
6. Nk.

Tujipange kwa ugeni huu na presentation za kistaraabu.

Tanzania iliyo bora zaidi inanukia.
Hapo kwenye namba 5 kijana usahau, kwa sababu wahusika wanakula na mwenye chama.
 
Hayo mengine yote yaliobaki yanawezwa kutekelezwa kama ulivyoshauri, kwa sababu hayana masilahi ya moja kwa moja na viongozi wa chama.

Hayo ni 80%. Nadhani si haba japo tunapenda tupate yote. Si walisema heri nusu shari? Sembuse 80%?

% yoyote tutaipokea tunapoendelea kudai zote 100.

Si ndiyo ustaarabu mkuu?
 
Ni jambo la kheri kuwa CHADEMA itakuwa na ugeni mkubwa kesho. Uthibitisho thabiti kuwa upinzani siyo jinai tena.

Pongezi nyingi kwa Mama Samia Rais wetu kwa hili.

Hivyo basi itumike fursa hii vizuri kuendelea kuyaweka wazi yaliyo vipaumbele zaidi kwa maslahi ya watu. Mfano:

1. Katiba Mpya
2. Wanaoishikiliwa kwa figisu za kisiasa
3. Walioathiriwa kwa figisu za kisiasa wakiwemo waliokufa, kujeruhiwa au kupotea
4. Uchunguzi kamili na kuwajibishwa kwa waliohusika kwenye #3
5. Kuwahusu wale wadada 19 bungeni bila ridhaa ya chama
6. Nk.

Tujipange kwa ugeni huu na presentation za kistaraabu.

Tanzania iliyo bora zaidi inanukia.
Unakumbuka ulivyokuwa ukiwapiga vita Kali akina Mdee ! Pole sana yako wapi sasa
 
Kwani nini kimebadilika kiasi kunipa pole mkuu? La kina mdee liko mahakamani.

Japo yeye huwa anafuta kesi, kumkumbusha umuhimu wa sote kuzingatia katiba. La kina mdee kama kichocheo cha udharura wa katiba mpya ukiwamo uuna ubaya gani?
 
Hayo ni 80%. Nadhani si haba japo tunapenda tupate yote. Si walisema heri nusu shari? Sembuse 80%?

% yoyote tutaipokea tunapoendelea kudai zote 100.

Si ndiyo ustaarabu mkuu?
Kama haya uliyoorodhesha hapa yapo kwenye ilani ya chama chao, basi sioni tatizo kuliongelea hilo mkuu.
 
Kwa mwendo wa masikilizano tutegemee nchi iliyo bora sana.

Kazi kwao Chadema walipo sasa ni kumleta Mdhungu.

"Yaani wajipange kwa mawasilisho ya kistaraabu yaliyo shiba."
 
Umeandika na kushauri vizuri sana. Ngoja tuone wataupokeaje ushauri wako.
 
Hivyo basi itumike fursa hii vizuri kuendelea kuyaweka wazi yaliyo vipaumbele zaidi kwa maslahi ya watu. Mfano:

1. Katiba Mpya
2. Wanaoishikiliwa kwa figisu za kisiasa
3. Walioathiriwa kwa figisu za kisiasa wakiwemo waliokufa, kujeruhiwa au kupotea
4. Uchunguzi kamili na kuwajibishwa kwa waliohusika kwenye #3
5. Kuwahusu wale wadada 19 bungeni bila ridhaa ya chama
6. Nk.
hapa umegonga penyewe.
Watu wastaarabu au nchi zilizostaarabika, upinzani katika siasa siyo uadui, kwangu mimi naona hii ni njia sahihi ya kulipeleka Taifa letu mbele! mama Samia hili litamjenga sana tena sana na kuacha historia njema. Siyo kma magufuli ambaye ameacha historia ya mauaji!
 
Kwenye maridhiano sio kila kitu lazima kiwekwe wazi...
 
Yaliyoorodheshwa pale ni vipaumbele. Fikiria katiba mpya, kina Lijenje, wasiojulikana, kutokuzingatia katiba nk.

Hayo hayawezi kuwa siri.
 
Kwani nini kimebadilika kiasi kunipa pole mkuu? La kina mdee liko mahakamani.

Japo yeye huwa anafuta kesi, kumkumbusha umuhimu wa sote kuzingatia katiba. La kina mdee kama kichocheo cha udharura wa katiba mpya ukiwamo uuna ubaya gani?
Pole sana! Nilikueleza hujui siasa
 
Hili la kina Mdee naona limeibuliwa tu from nowhere halafu linapewa uzito usiostahili.

Lilianzia pale ambapo ilithibitika Chadema wameanza kupokea ruzuku, then likaendelezwa pale tulipoambiwa Samia atakuwa mgeni rasmi BAWACHA, basi hapa vijana wa lumumba wakiongozwa na johnthebaptist ndipo wakawapachika wakina Mdee.

Kisha wakazidi kulipa nguvu hilo jambo baada Kibatala na wenzake jana mahakamani kusema kwamba hawana nia ya kuendelea kuwauliza maswali Mdee na wenzie...

Niwakumbushe tu, hayo matukio waliyounganisha hapo juu, hayana uhusiano wowote na kusamehewa kina Mdee, ile issue yao ni separate, wao kusamehewa ni lazima kwanza waombe msamaha, na ijulikane hivyo, lakini sio kinyume na hapo.
 
Lilianzia pale ambapo ilithibitika Chadema wameanza kupokea ruzuku, then likaendelezwa pale tulipoambiwa Samia atakuwa mgeni rasmi BAWACHA, basi vijana wa lumumba wakiongozwa na johnthebaptist ndipo wakawapachika wakina Mdee.

Kisha wakazidi kulipa nguvu hilo jambo baada Kibatala na wenzake jana mahakamani kusema kwamba hawana nia ya kuendelea kuwauliza maswali Mdee na wenzie...

Niwakumbushe tu, hayo matukio waliyounganusha hapo juu, hayana uhusiano wowote na kusamehewa kina Mdee, ile issue yao ni separate, wao kusamehewa lazima kwanza waombe msamaha, na ijulikane hivyo, lakini sio kinyume na hapo.
Haya
 
Hili la kina Mdee naona limeibuliwa tu from nowhere halafu linapewa uzito usiostahili.

Lilianzia pale ambapo ilithibitika Chadema wameanza kupokea ruzuku, then likaendelezwa pale tulipoambiwa Samia atakuwa mgeni rasmi BAWACHA, basi hapa vijana wa lumumba wakiongozwa na johnthebaptist ndipo wakawapachika wakina Mdee.

Kisha wakazidi kulipa nguvu hilo jambo baada Kibatala na wenzake jana mahakamani kusema kwamba hawana nia ya kuendelea kuwauliza maswali Mdee na wenzie...

Niwakumbushe tu, hayo matukio waliyounganisha hapo juu, hayana uhusiano wowote na kusamehewa kina Mdee, ile issue yao ni separate, wao kusamehewa ni lazima kwanza waombe msamaha, na ijulikane hivyo, lakini sio kinyume na hapo.

Mazungumzo yoyote na awaye yote hayapaswi kuathiri mapambano kwenye uwanja:

1. Kipaumbele katiba Mpya
2. Tuwe na mkakati wa kuipata katiba
3. #2 iambatane na action plan
4. Tuwe na mpanga mikakati mahiri.

Nani anahudhuria mkutano huu sI suala. Hata kama kina johnthebaptist wanataka kwenda na wapewe kadi.
 
Jana mlijitutumua kweli kuwarusha roho makamanda humu ndani, bora sasa mrudi kukaa kwa kutulia.
Makamanda hawapaswi kurushwa roho na vitu vidogo hivi. Roho labda zinaweza kurushwa ikisikika katiba mpya siyo kipaumbele tena na labda eti kunapangwa chaguzi zozote ndani ya katiba hii.
 
Back
Top Bottom