CHADEMA kushiriki Uchaguzi wa Diwani Handeni

Fundi Mchundo

Platinum Member
Joined
Nov 9, 2007
Posts
10,448
Reaction score
8,705
Nimeona mahali mtu aliyetambulishwa kama Katibu wa CHADEMA Handeni, Kombo Matulu akihimiza wananchi wakampigie kura mgombea wa CUF.

Inaelekea CHADEMA wamebadilisha msimamo wao kuhusu kutoshiriki katika katika uchaguzi wowote mpaka Katiba mpya itakapopatikana.

Amandla.
 
..huyo bwana ni mtovu wa nidhamu.

..hapo alaumiwe mtu binafsi sio chama.
Chama kinastahili lawama maana hakiwachukulii hatua watu kama hawa. Msimamo wake kuhusu wale waliokubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 hauko wazi. Chadema haijaweka wazi msimamo wake kuhusu madiwani na mbunge wake ambao wanakiwakilisha kwenye Halmashauri na Bungeni. Ndio maana watu kama hawa wameanza kujitokeza na watashiriki kwenye chaguzi za 2024 na 2025 bila kujali msimamo wa chama chao.

Amandla...
 
Nimeona mahali mtu aliyetambulishwa kama Katibu wa CHADEMA Handeni, Kombo Matulu akihimiza wananchi wakampigie kura mgombea wa CUF.

Inaelekea CHADEMA wamebadilisha msimamo wao kuhusu kutoshiriki katika katika uchaguzi wowote mpaka Katiba mpya itakapopatikana.

Amandla.

Mbona hueleweki? Unadai CHADEMA inashiriki hapo happy unasema kawaambia waipigie kura CUF. Sasa CHADEMA imeshiriki kivipi?. Tangu ziara ya mama Lindi naona mnailazimisha CHADEMA kwenye mambo ya kijinga
 
Kusimama jukwaani na kusema mpigie kura fulani ni kushiriki katika uchaguzi. Sio lazima ukae high table ndio useme umeshiriki kwenye harusi.

Hamna mtu anaowalazimisha Chadema bali ni wenyewe ndio wanatoa nafasi ya kuonekana kama ndumila kuwili.

Amandla...
 
Chama kilishatoa tamko. Huyo katibu kahudhuria Kama mgeni tu wa CUF.
Imetoa tamko wapi? Kama Chadema hawaoni kuwa kumruhusu Katibu wake kumnadi mgombea katika uchaguzi ambao wao wanadai hawautambui kunaweza kutumika kuonyesha kuwa wao ni wanafik basi wana matatizo makubwa.

Amandla...
 
Mbona huo mkutano wa CUF?. Yeye kaenda kuwapa support CUF .
Unaendaje kumpa support mtu anaeshiriki katika uchaguzi ambao hauutambui? Kwa hiyo Chadema wanaweza kuwanadi ACT Wazalendo katika uchaguzi wa 2025 ikiwa wao watakataa kushiriki? Watawaambia nini wanachama wao waliowazuia kushiriki huku wakisimama kumpigia debe mgombea wa chama kingine?

Amandla....
 
Chama kinastahili lawama maana hakiwachukulii hatua watu kama hawa. Msimamo wake kuhusu wale waliokubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 hauko wazi. Chadema haijaweka wazi msimamo wake kuhusu madiwani na mbunge wake ambao wanakiwakilisha kwenye Halmashauri na Bungeni. Ndio maana watu kama hawa wameanza kujitokeza na watashiriki kwenye chaguzi za 2024 na 2025 bila kujali msimamo wa chama chao.

Amandla...

Huyo siyo mgombea Bali anawapa msaada CUF kwenye kampeni. Kuhusu kugombea , chama ndio kinafadhili mgombea , Kama chama kimekataa kushiriki huwezi kugombea labda uhame chama. Ndio maana mpaka Sasa hivi msimamo wa CHADEMA kutoshiriki uchaguzi mkuu unaendelea.
 
Unaendaje kumpa support mtu anaeshiriki katika uchaguzi ambao hauutambui? Kwa hiyo Chadema wanaweza kuwanadi ACT Wazalendo katika uchaguzi wa 2025 ikiwa wao watakataa kushiriki? Watawaambia nini wanachama wao waliowazuia kushiriki huku wakisimama kumpigia debe mgombea wa chama kingine?

Amandla....

Huyo ni individual sio CHADEMA Kama taasisi imemtuma. Ameenda Kama mfuasi wa upinzani sio kuiwakilisha CHADEMA.
 
Imetoa tamko wapi? Kama Chadema hawaoni kuwa kumruhusu Katibu wake kumnadi mgombea katika uchaguzi ambao wao wanadai hawautambui kunaweza kutumika kuonyesha kuwa wao ni wanafik basi wana matatizo makubwa.

Amandla...

Kimetoa tamko kupitia Mwenyekiti Mbowe na juzi hapa Kigaila Naibu Katibu Mkuu katoa maamuzi ya hata kutoshiriki uchaguzi wa 2025. Huyo katibu kaenda kwa mapenzi yake sio kwaajili ya CHADEMA.

Mbona chaguzi zote ndogo tangu 2020 CHADEMA hawajashiriiki , ije iwe nongwa katibu kahudhuria kampeni Tena kwa utashi wake sio wa chama. Usiangali mtu angalia msimamo wa chama.
 
Kusimama jukwaani na kusema mpigie kura fulani ni kushiriki katika uchaguzi. Sio lazima ukae high table ndio useme umeshiriki kwenye harusi.

Hamna mtu anaowalazimisha Chadema bali ni wenyewe ndio wanatoa nafasi ya kuonekana kama ndumila kuwili.

Amandla...

Ndio maana nikasema unalazimisha CHADEMA kwenye ujinga wenu. Hivi chaguzi zote ndogo tangu 2020 CHADEMA hiajaweka mgombea, Leo mjinga asiyejitambua kumnadi mgombea wa CUF unaona CHADEMA inashiriki uchaguzi. Lakini wakati haijaweka mgombea yeyote kwenye chaguzi ndogo za ubunge kule kigoma na udiwani nchi nzima, ilikuwa haina msimamo? Yani ujinga wa individual mmoja unauleta Kama ushahidi.
 
Kusimama jukwaani na kusema mpigie kura fulani ni kushiriki katika uchaguzi. Sio lazima ukae high table ndio useme umeshiriki kwenye harusi.

Hamna mtu anaowalazimisha Chadema bali ni wenyewe ndio wanatoa nafasi ya kuonekana kama ndumila kuwili.

Amandla...

Mnamlipa mtu pesa ili asimame jukwani mpate sababu. CHADEMA wangeweka mgombea hapo ungekuwa na justification, sio kichaa mmoja kujitbulisha katibu wa CHADEMA basi unakuja mbio. Hujauliza ni katibu wa Nini? Inaeza kuwa hata sio kiongozi wa CHADEMA.
 
Back
Top Bottom