CHADEMA kushiriki Uchaguzi wa Diwani Handeni

CHADEMA kushiriki Uchaguzi wa Diwani Handeni

Huyo siyo mgombea Bali anawapa msaada CUF kwenye kampeni. Kuhusu kugombea , chama ndio kinafadhili mgombea , Kama chama kimekataa kushiriki huwezi kugombea labda uhame chama. Ndio maana mpaka Sasa hivi msimamo wa CHADEMA kutoshiriki uchaguzi mkuu unaendelea.
Shida yako ndio hiyo. Unaamini kushiriki ni kugombea tu. Kiongozi wa Chama akimpigia debe mgombea wa chama kingine ni ishara kuwa hicho chama kimeshiriki. Tutajuaje kuwa ni makubaliano kati ya vyama ya kupeana sapatin pale ambapo chama kingine kina nguvu zaidi? Chadema ilishiriki uchaguzi Zanzibar ingawa ilikuwa inampigia debe mgombea wa chama kingine. Kuendekeza tabia kama hizi ndio kutapelekea watu kujitokeza na kugombea kwa niaba ya Chadema katika uchaguzi ujao hata kama uongozi wa juu utasema hawashiriki.

Amandla.....
 
Chama kinastahili lawama maana hakiwachukulii hatua watu kama hawa. Msimamo wake kuhusu wale waliokubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 hauko wazi. Chadema haijaweka wazi msimamo wake kuhusu madiwani na mbunge wake ambao wanakiwakilisha kwenye Halmashauri na Bungeni. Ndio maana watu kama hawa wameanza kujitokeza na watashiriki kwenye chaguzi za 2024 na 2025 bila kujali msimamo wa chama chao.

Amandla...

Soma alama za nyakati, kikiwachukulia hatua serikali inakuja kuwatetea. Angalia akina Haliima Mdee , mahakama zetu na bunge zinawalinda.
 
Huyo ni individual sio CHADEMA Kama taasisi imemtuma. Ameenda Kama mfuasi wa upinzani sio kuiwakilisha CHADEMA.
Splitting hairs. Amesimama kama Katibu wa Chadema. Watu wote wanamjua kama ni Katibu wa Chadema. Utasemaje kuwa ni individual? Optics matter. Watu wakimuangalia wanaona Chadema hata mseme nini.

Amandla.....
 
Kimetoa tamko kupitia Mwenyekiti Mbowe na juzi hapa Kigaila Naibu Katibu Mkuu katoa maamuzi ya hata kutoshiriki uchaguzi wa 2025. Huyo katibu kaenda kwa mapenzi yake sio kwaajili ya CHADEMA.

Mbona chaguzi zote ndogo tangu 2020 CHADEMA hawajashiriiki , ije iwe nongwa katibu kahudhuria kampeni Tena kwa utashi wake sio wa chama. Usiangali mtu angalia msimamo wa chama.
Nazungumzia kitendo cha huyu Katibu na sio matamko ya jumla. Mbona hatujawahi kusikia kiongozi wa Chadema akimpigia debe mgombea wa chama kingine katika uchaguzi ambao wamegoma kushiriki? Ni yale yale ya kupenda supu ya nyama ya nguruwe wakati unasema huli nguruwe.

Amandla...
 
Katibu wa Nini?. Mnahangaika Sana kununua vichaa na kuwalazimisha ni CHADEMA, ila mtafeli.
Huyu ametambulishwa kama Katibu wa Chadema. Chadema ituambie kama ni kichaa na sio Katibu wake. Mbona kazi ndogo?

Amandla...
 
Mnamlipa mtu pesa ili asimame jukwani mpate sababu. CHADEMA wangeweka mgombea hapo ungekuwa na justification, sio kichaa mmoja kujitbulisha katibu wa CHADEMA basi unakuja mbio. Hujauliza ni katibu wa Nini? Inaeza kuwa hata sio kiongozi wa CHADEMA.
Chadema ndio wanajua kama ni Katibu wao au sio. Chadema imesema haitashiriki katika uchaguzi na haijasema kuwa haitaweka mgombea. Kushiriki ni zaidi ya kuweka mgombea.

Amandla...
 
Itoe tamko wakati tangu 2020 haijashiriki chaguzi zote ndogo?. Itoe tamko kisa mjinga mmoja kaenda kwenye mkutano wa CUF?
Ni vitu vidogo kama hivi ndio vinapunguza kuaminika. Kumtukana mtu hakusaidii kitu bali ku azidi kuaminisha watu kuwa mashabiki wa Chadema mnakimbilia matusi mnaposhindwa kujibu hoja.

Amandla..
 
Soma alama za nyakati, kikiwachukulia hatua serikali inakuja kuwatetea. Angalia akina Haliima Mdee , mahakama zetu na bunge zinawalinda.
Kwa hiyo Chadema inaogopa kuwachukulia hatua wanachama wake kwa kuhofia serikali itawatetea? Are you serious?
Alama za nyakati ni kuwa udhabiti wa msimamo wenu unapimwa. Hawa hawa watagombea kwa niaba yenu 2025 na mtajitetea tena kuwa hamna cha kuwafanya kwa sababu watatetewa naa serikali.

Amandla....
 
Hii picha na hiki kijijin cha wafuasi wa CDM ni hapa handeni? Au umetafuta tu pa kujifichia?
Mpenda chongo kweli huita kengeza. Nani amezungumzia wafuasi wa CDM? Tuelimishe tu kama una hakika kuwa huyo sio mgombea wa CUF na huyo anayempigia debe sio Katibu wa CDM na hapo sio Handeni. Mimi nimeileta kama ilivyoweka mtandaoni.

Amandla...
 
Nimeona mahali mtu aliyetambulishwa kama Katibu wa CHADEMA Handeni, Kombo Matulu akihimiza wananchi wakampigie kura mgombea wa CUF.

Inaelekea CHADEMA wamebadilisha msimamo wao kuhusu kutoshiriki katika katika uchaguzi wowote mpaka Katiba mpya itakapopatikana.

Amandla.
Matulu kikwetu ni matako
 
Mpenda chongo kweli huita kengeza. Nani amezungumzia wafuasi wa CDM? Tuelimishe tu kama una hakika kuwa huyo sio mgombea wa CUF na huyo anayempigia debe sio Katibu wa CDM na hapo sio Handeni. Mimi nimeileta kama ilivyoweka mtandaoni.

Amandla...
Kumbe naww umeokoteza mitandaon tu nikajua umefuatilia ili upate uhakika!! Bas sawa
 
Uko mtandaoni halafu unashangaa watu kupata taarifa mtandaoni!

Amandla...
Humu sio Facebook wala Instagram weka thread ukiambatanisha na evidence kutoka kwa official page ya chama husika!! Kama ni CCM hua wanaweka picha ya kunadi wagombea wao hali kadhalika CDM na wengine. Itakua bora kama ukiweka hii hbr kutoka kwa official page ya CDM! Over
 
Kote ni mtandaoni. Chadema kwenye taarifa za kwenye mtandao wako nyuma sana. Kaangalie lini wame update hiyo unayoiita official page. Ukweli ni kuwa kinachowasaidia Chadema mtandaoni ni kurasa za wakina Maria, Fatma, MM n.k. Hata wakati wa kesi ya Freeman taarifa zilikuwa zinapatikana kwa MM na sio kwao.

Wee kumbe popoma kweli 😂😂😂😂 ingia page yao Twitter ipo updated every minutes, na taarifa zote kuhusu wao huzitoa hapo.
 
Wee kumbe popoma kweli 😂😂😂😂 ingia page yao Twitter ipo updated every minutes, na taarifa zote kuhusu wao huzitoa hapo.
Chadema twitter mara ya mwisho kuwa updated ni masaa 19 iliyopita kwa clips za presa ya Mwaitenda. Kabla ya hapo wametuambia kuwa Freeman anaenda Marekani. Kabla ya hapo ni wakina Lissu wako Ulaya. Na clip za Celestine Simba. Na ya ziara ya Heche Mtama. Haina tofauti na ya CCM kwa ku prioritize viongozi wake wa juu tu. Habari zinazohusu wanachama wake wa kawaida ni chache. Ukitaka kujua kuwa wanaendelea kujenga ofisi zao nenda kwa wakina Maria. Ukitaka kujua kuwa kuna watu wanapitia wakati mgumu nchini nenda tena kwa wanaharakati. Hivi karibuni wameweka clip ya msichana aliyepigwa na DC. Waziri Gwajima amejitokeza akilaani kitendo hicho na kusema kuwa wanampa msaada aliyepigwa lakini Chadema, Bawacha na Bavicha kimyaa.

Amandla...
 
Back
Top Bottom