Tetesi: CHADEMA kushirikiana na UKAWA kurudi Bungeni kwa kishindo kikuu

Tetesi: CHADEMA kushirikiana na UKAWA kurudi Bungeni kwa kishindo kikuu

Huu ujinga mwingine, kwani PM kaandaa mwenyewe hiyo hotuba?
Hategemei wafanyakazi wa Bunge kama Mbowe, hotuba ya Mbowe ilitakiwa ika andaliwe Ufipa pale, ila kwa vile wamejaa watu wanaojua kuropoka tu lakini kichwani f6 failure ndio maana anategemea msaada wa wafanyakazi wa Bunge.
 
NLD YA MAKAIDI VEPE SIO UKAWA TENA

Kushirikiana na ukawa Zito ukawa ni wasaka tonge leo na yeye kageuka msaka tonge

Sihasa ni ukafiri kabisa leo unapinga kesho unaunga mkono jambo lile lile ulilolikataa
tena inaweza kuwa hata kuna watu wamepoteza maisha kwa kukataa kwako.
 
Wasalaam, tetesi zilizotufikia hivi punde ni kwamba CHADEMA ,CUF, ACT-Wazalendo na NCCR Mageuzi wamejichimbia kufanya vikao vya ndani ili kuja bungeni na hoja ambazo zilitalitikisa taifa.

Aidha tetesi hizo zinasema hoja kuu ya upinzani itakua katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Hoja nyingine ni matumizi hasa manunuzi yasiopitishwa Bungeni na kutengewa bajeti ili Bunge liisimamie Serikali ni si Serikali kulisimamia bunge km ilivyo leo.

Aidha hoja nyingine ya upinzani ni kuhusu kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, mauaji na kuokotwa maiti kwenye virobo na kupotea kwa watu kama Ben Saanane na mwandishi Azory.

Katika hoja hii UKAWA wamepanga kudai Serikali iitishe uchunguzi huru kwamba Polisi washirikishe wachunguzi wa kimataifa ili kuwajua watu wasiojulikana.

Tusubiri muda ni rafiki wa kweli.
Hamna kipya hapa! Yote haya wanayaimba long time
 
kwa bunge hili ni bure.zaidi kutatokea tu malumbano kati ya wabunge wa ccm na upinzani basi.
 
hoja kuu ya upinzani itakua katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Walipewa chance enzi za Kikwete wakaipoteza. Badala yake wakawa ni kudai serikali ya mkataba, kuona original copy ya article of union, kumtukana baba wa taifa and so on. Bunge la katiba lililopangwa kukaa kwa muda usiozidi siku 30 likaendelea kwa siku 150 na kutumia matrillion ya pesa ya walipa kodi: kila mjumbe wa bunge hilo akilipwa sh 0.5 billion kwa siku kama sitting allowance. Wajumbe na supporting staff plus facilitators walikuwa zaidi ya 1,000. At the end of all this kilichopatikana ni dude moja linaitwa Ukawa, a big monster which has been terrorizing our country. Sasa ni mjinga gani atakubali zoezi hilo lirudiwe ili likazae dubwasha jingine baya kuliko hilo la mwanzo litakaloitwa Chagema? Yaani tupate mi monster miwili: Ukawa na Chagema? Tutabaki salama hapo? Hatudanganyiki tena.
 
Hizo hoja watazitolea bunge gani? Wakati huo Tulia amelazwa hospitalini ama amekalia kiti cha spika?
 
Kumbe iliacha kushirikiana na ukawa??!!
 
Mktano huu wa Bunge la JMT ni Bajeti ya Serikali 2018/2019. Ni vema kufuata ratiba ya vikao vya Bunge, Wawakilishi wetu kujikita kupanga kilicho bora kwa WaTZ katika bajeti hii badala ya kuibuka na mengine,
 
Tia akili kichwani wewe! Sasa kama vimekufa hofu ya uchaguzi huru na wa haki inatoka wapi? Hofu ya kuwa na katiba mpya ya rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi inatoka wapi!? Mnahofia upinzani uliokwishakufa!? Ujuha mwisho lumumba siyo humu.



Wafu kila wakijaribu kusimama wanaanguka zaidi. Chadema na upinzani vishakufa kabisa TZ
 
Sawa... Hizo zote ni hoja za msingi, shida ni jee yupo kiongozi yoyote wa muhimili huo atakaekuwa tayari kuona wanapata muda wa kujadili kwa Uhuru? Hata hoja zikiwasilishwa vema nani atawaungabmkono maana wale wa upande mwingine wamezoea tu kisema ndiyoooooooooooo!!!! bila kuangalia mantiki, wao wanaangalia aliesema na wala sio kilichoswmwa
Ngoja tusubiri
 
Back
Top Bottom