Uchaguzi 2020 CHADEMA kutikisa Dar kwa siku tatu, Uchaguzi Mgombea Urais Tanzania na Zanzibar

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,358
Sasa ni Rasmi.

Chama kikuu Cha upinzani nchini CHADEMA kitaanza vikao vyake kwa siku 3 mfululizo kuanzia Jumapili tarehe 2 mpaka Jumanne tarehe 4 katika ukumbi maarufu nchini wa Mlimani City.

Kikao Cha Kamati Kuu kitafanyika kesho Jumapili huku Baraza Kuu likiwa siku ya Jumatatu na Mkutano Mkuu utakuwa siku ya Jumanne.

Agenda Kuu ya vikao hivi ni kuchambua na hatimaye kupiga kura kumpitisha Rasmi mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA.

Tayari wajumbe wa vikao hivi wameshaanza kuwasili jijini Dar es Salaam wakiwa na shauku kubwa ya kutimiza takwa la kikatiba.

Mchuano mkali kwenye nafasi ya Urais ni Kati ya mafahali wawili Lazaro Nyalandu Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Kati na Mjumbe wa Kamati Kuu akipambana na Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa na mwanasiasa mashuhuri zaidi kwa Afrika.

Ikumbukwe CHADEMA ilitikisa nchi siku ya Jumanne wiki hii wakati maelfu kwa maelfu ya watu walipojaa majiani kumlaki Tundu Lissu aliyerejea matibabuni huku kukiwa na maandamano makubwa zaidi kuwahi kutokea nchini kumsindikiza mwanasiasa huyo makao makuu ya Chama huku umati huu ukiimba 'Rais' Rais' Rais' kote alikopita ambapo Barabara ilifungwa kwa masaa manne kumsindikiza shujaa huyo.

Sisi wa Molemo Media Kama Sikuzote Tunatarajia kuwaletea matangazo ya moja kwa moja wasomaji wetu wa Jamii Forums ili Dunia kuweza kujua kinachoendelea ndani ya vikao hivyo muhimu.Tuna Imani hatukuwahi kuwaangusha wafuatiliaji wetu.

Wagombea wa CHADEMA ni;

Wakili Simba Neo

Lazaro Nyalandu

Tundu Lissu

Dk.Maryrose Majinge

Wakili Gaspar Mwanalyela

Isaya Mwita

Mchungaji Leonard Manyama

 
Dah umeandika kishabiki sana mkuu yaani maandamano ambyo hayajawahi kutokea tanzania? yepi hayo ?huyuhuyu lissu na ni siku hyo akirudi ? unachekesha kama hayo ndiyo maandamano ambayo hayajawahi kutokea utakua siyo mfuatiliaji wewe au akli yako inashida mahala kwenye medula oblangata
 
Hizo ndo habali watanzania hasa wapenda demokrasia haki na utawala bora ndo huwa wanapenda kuziskia achana na zile habali za kibaguzi
 
Lisu asipopita chadema mtakuwa mmejiangusha wenyewe. Wengine tunasubili jina la mgombea wa chadema ili tuanze kuzisaka kadi zetu za kupigia kura zilipo,

Nje ya hapo hatupigi kura, mimi nawakilisha wengi ambao tunasubili jina la lisu, kama tupo pamoja gonga likes za kutosha
 
h
apo anapita nyalandu hivi unamjua mbowe wewe>? za awali tu kambwaga lissu vibaya unategemea nini ?
 
Mungu awatangulie Chadema. Sasa ni wakati wenu wa kuithibitishia Tanzania, watanzania na dunia kwa ujumla kuwa nyie ni Chama Bora kwa sasa hapa Tanzania.

Nawatakia Heri kwenye vikao vyenu!
Mungu Akubariki Sana.Salaam zimefika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…