Chadema kutumia watu wasiojulikana kutukana viongozi sio ustaarabu wa kisiasa

Chadema kutumia watu wasiojulikana kutukana viongozi sio ustaarabu wa kisiasa

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Ustaarabu ni jambo la muhimu kwenye maisha ya kila siku. Iwe ni maisha ya kawaida au kisiasa.

Hakuna ubishi kuwa serikali ya CCM chini ya JPM inakubalika kwa wananchi. Hii ni kwa sababu imeweza kufanya kazi kubwa ya kutekekeza ilani ya uchaguzi vizuri.

Sasa ninyi Chadema mmekosa mahala ambapo mnaweza kuikosoa au kuinanga serikali ya CCM chini ya JPM. Mlichobakiza ni kuweka watu kwenye mitandao mbali mbali kama Twitter ili wawatukane na kuwakashifu viongozi wa Serikali.

Tunafahamu mnajua chama chenu kimefiliska kisiasa na sasa hakina muelekeo. Mlichobakiza ni kutumia wahuni kutukana na kutunga uongo kwenye mitandao ya kijamii.

Hili sio jambo jema hata kidogo na ni uthibitisho kuwa chama chenu ni chama cha wapenda vurugu na matusi. Na October ndio mwisho wa uhai wa chama chenu.
 
Ili muwafungulie mashitaka uhujumu uchumi...haya mmeyatengeneza wenyew nyie vibwengu kukosolewa na watu wasiojulikana....hvi mdude yuko wapi baada ya kukosoa hadharan
 
Muulize mkubwa wako,kwa nini anatumia nguvu nyingi kumtafuta huyo kigogo 2014?

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
Kwa upuuzi na uongo anaopost? Anadanganya Ndugulile anaumwa alafu mnafurahi. Hana muda nae.
 
Ili muwafungulie mashitaka uhujumu uchumi...haya mmeyatengeneza wenyew nyie vibwengu kukosolewa na watu wasiojulikana....hvi mdude yuko wapi baada ya kukosoa hadharan
Tofautisha kutukana na kukosoa.
 
MADA : FAIDA NA ATHARI ZA PROPAGANDA KWA TAIFA


Source : Star TV Habari

Nchi nyingi za kigandamizaji na kidikteta huanzisha misamiati na misemo mipya hata 'lugha' mpya pia huanziashwa. Pia tawala hizo huhariri historia kuja na historia wanayoitaka wao isisike.

Kubwa ni kutaka kuwanyamazisha wakosoaji kwa kuwasema wanatukana. Mfano neno 'mbaya' CCM Mpya watataka ktk sentensi au uwasilishaji hoja iwe badala ya : Barabara hii ni mbaya watataka isemwe au iandikwe Barabara hii hairidhishi. Kuna tofauti kubwa kati ya neno Mbaya / Hairidhishi.
Hivyo kutumia mbaya kuelezea uhalisia wa hali ya barabara utaambiwa umetukana.

Mfano mwingine wa lugha mpya ya CCM Mpya : Reli ya SGR ujenzi wake unalegalega wao CCM Mpya watasema Reli ya SGR imekamilika 33%

Tanzania imeshindwa kujinafasi kama mwenyekiti wa SADC ktk siasa za ki-GeoPolitiki kushawishi. CCM Mpya watasema Tanzania siku zote toka enzi za kupigania uhuru na kuondoa ubaguzi imekuwa kinara kuongoza mapambano.

Na tukiangali kipindi hiki kuna maneno mengi yatabadilishwa au kusemwa ni tusi na hii siyo imetokea kwa bahati mbaya bali ni propaganda za CCM Mpya.

Kuwanyamazisha wasomi wa wasichambue historia ya kweli bali wanalazimisha waichambue ile wanaoitaka iliyo haririwa.
 
Utaongeleaje yule chizi Lipumba? Tunaongelea chadema sababu Kuna jambazi la michango ya wabunge na jizi la wake za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuvumiliane tu jamani. Isiwe nyani acheka kundu la mwenziwe. Wote mnatukanana. CCM mnatukana. CHADEMA mnatukana, na ACT mnatukana. Watu husema: "don't throw stones if you are leaving in a glass-house".
 
Back
Top Bottom