jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,556
- 25,342
Ukimuita mtu mpumbavu hali ya kuwa huyo mtu sio mpumbavu hilo linakua kosa kwa kweli!Ustaarabu ni jambo la muhimu kwenye maisha ya kila siku. Iwe ni maisha ya kawaida au kisiasa.
Hakuna ubishi kuwa serikali ya Ccm chini ya JPM inakubalika kwa wananchi. Hii ni kwa sababu imeweza kufanya kazi kubwa ya kutekekeza ilani ya uchaguzi vizuri.
Sasa ninyi Chadema mmekosa mahala ambapo mnaweza kuikosoa au kuinanga serikali ya Ccm chini ya JPM. Mlichobakiza ni kuweka watu kwenye mitandao mbali mbali kama Twitter ili wawatukane na kuwakashifu viongozi wa serikali.
Tunafahamu mnajua chama chenu kimefiliska kisiasa na sasa hakina muelekeo. Mlichobakiza ni kutumia wahuni kutukana na kutunga uongo kwenye mitandao ya kijamii. Hili sio jambo jema hata kidogo na ni uthibitisho kuwa chama chenu ni chama cha wapenda vurugu na matusi. Na October ndio mwisho wa uhai wa chama chenu.
Kinachoshangaza ni watu wazima kuwakingia kifua maiti wasiuawe.
Cha kuangali ni je matusi wanayotukanwa ni sehemu ya majina yao😁😁
E.g mwenye wazimu kuitwa mwendawazimu sio tusi.
Apuuzaye kuitwa mpuuzi hajatukanwa.
Muuaji hali kadhalika.
Au wewe unaonaje!!