Pre GE2025 CHADEMA kuweni makini na chaguzi zisiwagawe, CCM wanasubiri mkono uanguke waukamate. Macho na masikio ya CCM yako kwenu sasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Habari ndiyo hiyo. Hizi juhudi za Mbowe aondoke, ni mkono wa chuma wanaouogopà. Wanasubiri uanguke washangilie. Msiruhusu kitu kama hicho.

Msiwe wepesi wa kusahau. Mnadhani Mashinji (nadhani ndiye aliyekuwa amegombea uenyekiti? Nisahihisheni) angelipata uenyekiti Chadema ingelikuwepo?

Chukueni tahadhali kubwa sana katika kufanya maamuzi.
 
Hizi juhudi za Mbowe aondoke, ni mkono wa chuma wanaouogopà.
Ni kweli. Lkn kuendelea kwa Mbowe kuwa mwenyekiti kwa miaka zaidi ya 20 kunawapa maadui wa chadema uhalali wa kuaminiwa kuwa "ndani ya chadema hakuna demokrasia".

Chama kinapaswa kuwa na succession plan na kusimama kitaasisi badala ya kumtegemea mtu mmoja. Itakuwa vipi Mbowe akitwaliwa na muumba?

Kwa maslahi mapana ya chama, Mbowe aachie ngazi, abakie kuwa mwanachama, mshauri na mtu mashuhuri ndani ya chama
 
Cecil Mwambe Ndio aligombea Uenyekiti na Mbowe

Alishinda LAKINI kura zake wakampa Mbowe 🐼
 
Sasa mkipewa Serikali simtatawala milele?
Tukiruhusiwa na wapiga kura tutatawala milele. Siyo Kwa bao la mkono na mawazo na mipango kama ya mwenyekiti yule wa UVCCM kule Kanda ya Ziwa. Ambaye mpaka Leo sijui mmemfanyaje
 
CCM k
Ni kweli. Lkn kuendelea kwa Mbowe kuwa mwenyekiti kwa miaka zaidi ya 20 kunawapa maadui wa chadema uhalali wa kuaminiwa kuwa "ndani ya chadema hakuna demokrasia".

Chama kinapaswa kuwa na succession plan na kusimama kitaasisi badala ya kumtegemea mtu mmoja. Itakuwa vipi Mbowe akitwaliwa na muumba?

Kwa maslahi mapana ya chama, Mbowe aachie ngazi, abakie kuwa mwanachama, mshauri na mtu mashuhuri ndani ya chama
CCM kama kuna Demokrasia mnataka fomu moja ya mgombea Urais kwa nn? Kwa nini nafasi za makamu mwenyekiti, mwenezi na katibu mkuu hawawi watu kadhaa kuchukua fomu wakapigiwa kura mnaletewa na Mwenyekiti mtu anayemtaka? Eti mnaidhinisha anafaa au hafai wakati huo anayemleta kwenu nafasi yake unaijua.
 
Ni kweli. Lkn kuendelea kwa Mbowe kuwa mwenyekiti kwa miaka zaidi ya 20 kunawapa maadui wa chadema uhalali wa kuaminiwa kuwa "ndani ya chadema hakuna demokrasia".

Chama kinapaswa kuwa na succession plan na kusimama kitaasisi badala ya kumtegemea mtu mmoja. Itakuwa vipi Mbowe akitwaliwa na muumba?

Kwa maslahi mapana ya chama, Mbowe aachie ngazi, abakie kuwa mwanachama, mshauri na mtu mashuhuri ndani ya chama
Ngoja kwanza tupate katiba mpya. Akiingia mtu legelege, chadema imekwisha. Kwa ufidhuri wa ccm Ngoja kwanza Mbowe awepo, kwa Katiba hii ambayo Rais ni Mungu, kama hakuna mtu madhubuti, chadema imekwisha.

Ccm wako tayari kumuhonga hata billions of money kuiua chadema kama ilivyokufa CUF. Hapana ngoja Mbowe awepo kwanza
 
Ni kweli. Lkn kuendelea kwa Mbowe kuwa mwenyekiti kwa miaka zaidi ya 20 kunawapa maadui wa chadema uhalali wa kuaminiwa kuwa "ndani ya chadema hakuna demokrasia".

Chama kinapaswa kuwa na succession plan na kusimama kitaasisi badala ya kumtegemea mtu mmoja. Itakuwa vipi Mbowe akitwaliwa na muumba?

Kwa maslahi mapana ya chama, Mbowe aachie ngazi, abakie kuwa mwanachama, mshauri na mtu mashuhuri ndani ya chama
Magufuli aliwahi sema ukiona mpinzani wako analalamika na kukusahihisha ujue umemshika pabaya kamatia hapohapo tangu lini ccm iliitakia mema cdm? Tangu lini mashauri wa mambo ya leadership succession ndani ya cdm yakarekebishwe na ccm? Hapana hapana ccm msiyaingilie ya cdm kama ilivyo chadema haiingilii ya ccm
 
Habari ndiyo hiyo. Hizi juhudi za Mbowe aondoke, ni mkono wa chuma wanaouogopà. Wanasubiri uanguke washangilie. Msiruhusu kitu kama hicho.
Msiwe wepesi wa kusahau. Mnadhani Mashinji ( nadhani ndiye aliyekuwa amegombea uenyekiti??? Nisahihisheni) angelipata uenyekiti Chadema ingelikuwepo?

Chukueni tahadhali kubwa sana katika kufanya maamuzi.
kwann macho ya kibaraka yako wap mpaka analia kuna rushwa kwenye uchaguzi huo wa Chadema?🐒
 
CCM kama kuna Demokrasia mnataka fomu moja ya mgombea Urais kwa nn?
Kama madhaifu ya ccm ndiyo kipimo cha vyama mbadala (vya upinzani), basi vinapoteza uhalali na sababu ya uwepo wake.

Tulitegemea chadema ijipambanue kwa mazuri mengi yanayokosekana ccm.
 
Tangu lini mashauri wa mambo ya leadership succession ndani ya cdm yakarekebishwe na ccm? Hapana hapana ccm msiyaingilie ya cdm kama ilivyo chadema haiingilii ya ccm
Issue hapa siyo ccm kutoa ushauri, bali ni chadema kushindwa kufuata misingi ya demokrasia kama kinavyojitambulisha kwenye jamii.

Haileti mantiki kujiita chama cha demokrasia wakati kinatenda kinyume.
 
Back
Top Bottom