CHADEMA kuzindua Mikutano ya Hadhara Januari 21, 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Siku tatu baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza ruhusa ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa, Kamati Kuu ya Chadema imeazimia kuzindua rasmi mikutano hiyo.

Rais Samia alitangaza uamuzi huo, Januari 3, 2023 alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa na alisema: “Uwepo wangu mbele yenu ni kuja kutoa ruhusa kwamba lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoshwa”.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 6, 2023 na chama hicho na iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje, John Mrema imesema maazimio hayo yanatokana na Kamati kuu iliyoketi Januari 5, mwaka huu.

“Kamati Kuu katika kikao chake cha dharura Januari 5, 2023 ilipokea na kujadili mwenendo wa mazungumzo ya maridhiano baina ya timu ya Chadema inayoongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, Abdulrahman Kinana,” imeeleza taarifa hiyo.

Kulingana na taarifa ya Chadema, Januari 21, 2023 itazindua rasmi mikutano ya hadhara kitaifa, itakayofuatiwa na uzinduzi wa mikutano ya hadhara katika kila Makao Makuu ya Kanda na baadaye ngazi nyingine za chama hicho.

Hata hivyo, ngazi zote za chama hicho zimeagizwa kuendelea na maandalizi ya mikutano ya hadhara.

Kamati Kuu ya Chadema imeazimia kuendelea kwa mazungumzo ya maridhiano kati yake na CCM yanayoendelea kwa kile ilichokieleza kuwa imeridhishwa nayo.

MWANANCHI
 
FB_IMG_1672921103951.jpg

Taarifa ya Kamati Kuu iliyokutana Kidigitali jana , pamoja na mambo mengine Imeipanga Tarehe 21/01/2023 kuwa siku ya Uzinduzi wa Mikutano ya hadhara kitaifa.

Baada ya uzinduzi huo wa Kitaifa , Utafuatia uzinduzi wa mikutano hiyo kwenye Kanda na baadaye maeneo mengine .

Usiondoke JF kwa taarifa za Uhakika

FB_IMG_1672941151490.jpg
 
Ni muda muafaka sasa chadema nao waonyeshe uungwana kwa kuondoa ile kesi yao na akina Mdee na wenzake
 
Huo ndio ukomavu, sio kila mtu anaanza kuitisha mikutano yake utadhani chama hakina structure.

Pia ni muhimu muwape watu wenu guidelines za kuandaa mikutano yao, ajenda za chama ni zipi, kwenye mikutano nini kiongelewe, n.k.

Sio mnaacha walevi wanaanza kupanda majukwaani na kutukana watu.
 
Ni vizuri kujipa muda wa kujiandaa vizuri,mambo ya kuzungumza ni mengi hivyo ni vizuri kuwekana sawa juu ya kipi kibebe agenda.
 
Ni muda muafaka sasa chadema nao waonyeshe uungwana kwa kuondoa ile kesi yao na akina Mdee na wenzake
Kwani kwenye hiyo kesi anaelalamika ni nani na mjibu mashtaka ni nani? Anaeweza kutoa kesi mahakamani ni mlalamikaji ambae ni akina Mdee wanaopinga kufukuzwa uanachama Ili kulinda ubunge wao.

Sent from my Infinix X689F using JamiiForums mobile app
 
Siku tatu baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza ruhusa ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa, Kamati Kuu ya Chadema imeazimia kuzindua rasmi mikutano hiyo.

Rais Samia alitangaza uamuzi huo, Januari 3, 2023 alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa na alisema: “Uwepo wangu mbele yenu ni kuja kutoa ruhusa kwamba lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoshwa”.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 6, 2023 na chama hicho na iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje, John Mrema imesema maazimio hayo yanatokana na Kamati kuu iliyoketi Januari 5, mwaka huu.

“Kamati Kuu katika kikao chake cha dharura Januari 5, 2023 ilipokea na kujadili mwenendo wa mazungumzo ya maridhiano baina ya timu ya Chadema inayoongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, Abdulrahman Kinana,” imeeleza taarifa hiyo.

Kulingana na taarifa ya Chadema, Januari 21, 2023 itazindua rasmi mikutano ya hadhara kitaifa, itakayofuatiwa na uzinduzi wa mikutano ya hadhara katika kila Makao Makuu ya Kanda na baadaye ngazi nyingine za chama hicho.

Hata hivyo, ngazi zote za chama hicho zimeagizwa kuendelea na maandalizi ya mikutano ya hadhara.

Kamati Kuu ya Chadema imeazimia kuendelea kwa mazungumzo ya maridhiano kati yake na CCM yanayoendelea kwa kile ilichokieleza kuwa imeridhishwa nayo.

MWANANCHI
Ya COVID 19 ni zaidi ya kila kitu haki itendeke msijisahau mkaenda kwenye mikutano tu! Hawawezi endelea kuwepo kule.

Sent from my T810S using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom