Uchaguzi 2020 CHADEMA kwa sera hii, mtakomba kura zote za wafanyakazi wa nchi hii, na haya ndio maneno tunayotaka kuyasikia yatayomuangusha Magufuli na CCM yake

Lowasa , Lijualibarid na Sumaye huenda wakapishana na gari ya salari
 
Ati kaskazini kwa wanini?
Nafsi hadi inakusuta
 
umegeuka Forbes saiv hahahaha ili muvi tamu sana haya endelea
 
Tulia
 
Ubaguzi, ubaguzi, ubaguzi! Wa kikanda, kikabila, kidini, kichama, wa kipato! Ni mara kadhaa kauli kutoka mdomoni mwa Rais zimetoka zikionesha ubaguzi wa wazi wazi. Ninavyofahamu mimi, binadamu yeyote hujisikia wa thamani anapothaminiwa nchini kwake. Yaani tuende nchi za watu tukabaguliwe na nchini kwetu wenyewe tubaguliwe! CDM mkiweza kuitumia hii turufu vizuri mtaongeza kura hasa kwa makundi ya wafanyakazi na wasomi nchini, maana makazini huko kuna moto unafukututa, kama kiongozi ametokea kanda ile basi anakua mungu-mtu ofisini, hizi kesi zipo kila ofisi. Itumieni hii turufu vizuri kuhubiri umoja na mshikamano kama nchi.

Vyovyote vile iwavyo huyu mzee lazima apate upinzani mkali sana, binafsi kama mwana CCM naamini tukipata upinzani mkali tutarudi kukaa mezani, kuangalia nyuma na kutengeneza sera mbadala za kuimarisha chama chetu. Chama tawala makini kinatokama na upinzani makini. CCM oyeee!
 
Watakuita MATAGA, Lumumba na majina mengine mengi kwa sababu you speak the facts. #wapuuze
 
Hello Mr.lord denning unadhani tunawezaje kuimarisha sekta binafsi kama nchi ili vijana tupate ajira? Nipate maoni yako tafadhali, your positive reply will be highly appreciated sir.
1. Kuwa na sera zisizobadirika za uwekezaji ( Hapa ni kwenye kodi na kila kitu) - Hakuna sehemu mtu atawekeza hela zake nyingi akitegemea baada ya miaka mitano tu raisi mpya tena wa chama kilekile atakuja na Sera mpya zitakazokinzana na sera zilizomfanya aje kuwekeza

2. Ni kuondoa influence/ disturbance kwa wawekezaji kutoka kwa viongozi wa kisiasa. Leo hii chini ya CCM mwekezaji anaweza akasumbuliwa na mkuu wa wilaya, baadae mkuu wa Mkoa a wote wanaweza toa maelekezo kwake bila kujali gharama alizoingia kwenye uwekezaji

3. Kuweka mfumo mmoja wa usajili na vibali vya Biashara/ uwekezaji. Kuna wawekezaji ninawafahamu tangu mwaka 2016 maombi yao ya uwekezaji( kupata eneo) hayajafanikiwa hadi leo. Nchi zilizoendelea na zilizo mbali mwekezaji maximum anatumia 3 weeks kupata usajili na vibali vyote vya biashara na wafanyakazi wake

4.. kuondoa influence ya serikali kwenye uwekezaji.Wawekezaji wawe huru kuwekeza sekta zote bila mizengwe.Serikali ijikite kukusanya kodi na kuhimiza mirabaha tu.

Haya yote chini ya serikali za kijamaa kama CCM haiwezekani
 

Nakusalimu mkuu, na imani miaka mitano ya mwisho ya uongozi wa Mh. JPM kutakuwa na neema kubwa kwa makundi mbalimbali ya hali ya chini.

Kwenye ukabila hapo umegusia kitu muhimu mno, nchi hii ni yote sote bila kuangalia kundi fulani.

All in all you are missed...
 
Kama wewe unaona CDM kuna wa kutekeleza sera mkuu kapige kura octaba nami nitaenda kumpigia kura JPM octaba.
 

Cha kwanza, tunashinda! Lakini Mimi naamini matokeo ya uchaguzi huu yatadetermine ujio wa neema au kiburi kikuu kwa viongozi wetu. Ndio maana nimesisitiza upinzani ni muhimu mkali ni muhimu sana uchaguzi huu.

Nimekumiss pia, ntakucheki soon WhatsApp nikilog out humu tupige stori mbili tatu, karibia Dodoma pia tunywe wine. (Ole wako unichome, unajua siku hizi huku ndio sehemu pekee tunaweza kukosoa)
 

Umetabiri vyema na nikuambie tu matokeo ya awamu hii ni muhimu sana kwa CCM zaidi ya upinzani maana ndio yatatupatia mwanga zaidi katika uchaguzi wa 2025. Watu wategemee neema zaidi zaidi ya njaa...

Huwenda kimwili tuko sehemu moja sasa [emoji41]
 

..ccm huwa wana ilani nzuri ktk kila uchaguzi.

..tatizo lao wakiingia madarakani wanaacha kutekeleza ilani wanaanza hila na ulaghai wa kushinda uchaguzi unaofuata.

..Jpm pia ana vipaumbele vyake tofauti na vipaumbele vya wananchi na vilivyoko kwenye ilani. kwa mfano ilani na ahadi za uchaguzi zilikuwa ni ujenzi wa viwanda, lakini Jpm akaenda kununua ndege kwa fedha ambazo angewekeza kwenye viwanda.

..Pia ukifuatilia bajeti za serikali za kila mwaka utashangaa sana kiwango cha fedha kinachopelekwa kusaidia kuinua sekta ya kilimo. Nchi hii ukimuinua mkulima umeinua taifa. Ukimuinua mkulima maana yake unaongeza idadi ya watu wenye purchasing power kubwa na makusanyo yako ya kodi yataongezeka, na uwezo wa ku-finance miradi na huduma za jamii utaongezeka.
 
Hapo Ufipa mmeajiri watu wangapi maana Mwita Waitara alidau hata michango ya nssf ya watumishi wawili waliopo hamuiwasilishi!
Wewe ni yohana mbatizaji au yohana mubangaizaji???


Una Mambo ya kipimbi Sana wewe!
 
Hakuna jipya hapo, JIPYA hapa ni maneno tu! Haya yote yanafanyika chini ya JPM kwa spidi kubwa. CDM hamuwezi kwani hata mkikusanya kodi ya kuyafanya hayo, hamuwezi kuyafanya kwa UFISADI wenu, kumbuka pesa za wabunge wenu zilivyoliwa itakuwa hizi za wananchi. Yataka moyo sana kufanya anayofanya JPM. halafu, Lissu anadaiwa na waliokuwa wakimtibia na waliokuwa wakimtembeza Ulaya na Marekani kubwabwaja!
 
Umeongea ukweli mkuu...

Lakini binafsi nafikiri tatizo letu Tanzania sio kumwezesha mkulima avune mazao mengi.

Tatizo tulilonalo kwasasa ni tunavuna, tukishavuna hatuwezi kuyapa thamani mazao tunayoyazalisha kisha na kuyauza.

Angalia maparachichi ya hapo Iringa...yananunuliwa kisha wakenya wanayabrand wanajiuzia SA na mataifa ya nje. Tuje kwenye nyanya na matunda...tatizo ni lilelile.

Kuna miaka ya nyuma Morogoro nyanya ukupita unaelekea Dar wanakuuzia mia tano 4kg. Tatizo hapo sio uzalishaji ila Viwanda kama ulivyosema.

Je, tunaviwanda vinavyoweza kuprocess tunachokitengeneza? Havipo. Mwisho Mkulima ataendelea kuwa maskini na vijana wetu hawatazipata ajira ghafi tunazoziuza.

Serikali inamchango mkubwa saana hasa kwenye kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na nafikiri hili JPM analijua saana. Lakini yeye anaamini zaidi mwekezaji mzuri ni mzawa (mimi na wewe) jambo ambalo litatuchukua muda mrefu saana. Hata wewe ungekuwa Rais usingejenga viwanda na wakati tuna maviwanda mengi yametufia toka kipindi cha SAP...bahati nzuri nimemskia juzi moja ya malengo yake ni kuanza kuvifufua.
 
Katika sentensi moja bila shaka unamaanisha kuboresha mazingira ya uwekezaji na urahisi wa kufanya biashara "easy of doing business " kwa kiasi Fulani nakubaliana na wewe lkn kwa upande wangu naona tatizo liko asilimia 95% kwa taasisi zinazotoa huduma yaani wale wahusika na asilimia 5%tu kwa wanasiasa. Binafsi mi ni mjasiriamali mdogo wakati naanza biashara kupata lessen ilinichukua miezi miwili nilizunguka halimashauri mpaka nikafokeana na mtumishi aliyekuwa anahusika kutoa leseni, wasomi wetu waliopewa dhamani ya kutoa huduma ama hawana kabisa elimu ya kumcare muwekezaji au wanaleta viburi ili wapewe rushwa. Imagine 2months unasubiri leseni wakati kwa mfanyabiashara hata one week ni to much time. Hiyo sio Kwenye halimashauri tu ni sehemu zote unazokwenda gov institutions are inefficient. Kwa upande wa Sera zisizobadilika naungana na wewe kwamba kuwe na dira ya maendeleo ya taifa hasa kwa upande wa Miundombinu ya kiuchumi, kwa upande wa kodi nadhani kodi nyingi zinahitaji kuwa updated annually ili kuregulate na ku stimulate uchumi. Na kwa upande wa wapi muwekezaji awekeze ni kweli serikali iweke incentives kwa sekta ambazo inataka ziwekezwe zaidi lkn otherwise wawekezaji wawehuru kuwekezapopote wanapodhani watanufaika.
Jambo la msingi ni kwamba serikali yoyote itakayo chaguliwa ijitahidi kuwekeza katika miundombinu ya kiuchumi kurahisisha ufanyaji wa biashara na uwekezaji kama vile umeme wa gharama nafuu na uhakika, barabara, bandari reli na miundombinu mingine ya Usafirishaji lkn pia iangalie namna bora ya kuinua kilimo hasa upande wa kutafuta masoko ya mazao na kuboresha kilimo kiwe cha kisasa kwa sababu ndio sekta inayoajiri watu wengi na ikiboreshwa maisha ya wengi yataimarika.
Nakushukuru kwa maoni yako chanya na nafikiri sisi vijana hatuna haja ya kutukanana na kufedheheshana kwenye mitandao na majukwaa kama haya kwa sababu lengo letu ni kujenga Nchi yetu tufike tunapopatamani. Tuje na hoja makini hata kama tutatofautiana mitazamo naamini tutafikia common ground.
Note: sina mrengo wowote wa kisiasa ila naapreciate kila mtu anayefanya kazi nzuri.
 

..binafsi sina tatizo na Wakenya kununua mazao yetu.

..hebu fikiria wasingeyanunua, mkulima hali ingekuwaje?

..naamini uzalishaji wa Tz unatosha ku-feed viwanda vya Tanzania pamoja na vilivyoko Kenya.

..Watanzania tujivunze kwamba kuwa na jirani mwenye uwezo ni jambo jema. Tujifunze changamoto wanazopitia USA dhidi ya jirani masikini kama Mexico, na jinsi USA inavyofaidika na jirani mwenye uwezo kama Canada.

..Au hapahapa, kati ya Kenya na Burundi ni jirani gani mwenye faida kubwa zaidi kwenye uchumi wa Tz? Inawezekana Burundi inatumia bandari yetu, lakini tukija ktk uchumi wa kaya Warundi wananunua mazao gani na kiasi gani kutoka kwetu?

..nakubaliana na hoja yako kuhusu upotevu wa mazao ambayo tunayavuna, na uhaba wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wetu.

..tatizo langu ni kwamba Jpm na ccm focus yao haiko kwenye wakulima au viwanda. focus ya ccm iko kwenye miradi yao mikubwa ambayo itachukua miaka 10 mpaka 15 kukamilika. sasa wengine tunataka kuona mabadiliko ya kweli ktk kizazi chetu.

..CCM inaweza kuwa chama kizuri kabisa ikiwa kitakaa benchi awamu 1 u 2 halafu ndio kirudi madarakani.
 
Aji Ajira,msisahau jaman kwenye ahadi zenu
 
Asante ndugu kwa kukubaliana nami kihoja. Watendaji serikalini wako hivo kutokana na uzembe wa viongozi tulio nao ambao ni wanasiasa. Mwanasiasa ndio kiongozi mkuu na ndio anaetunga na kusimamia sera. Sasa imewashinda nini CCM kuweka mfumo wa kuhakikisha mtu anafungua biashara na kupata vibali vyote ndani ya wiki 3????

Lingine ndugu, kwa CCM wao ukiongelea uwekezaji au wawekezaji binafsi wao wana tafsiri ya wezi au watu wanaotuibia kwa fikra kama hizi kamwe hatuwezi kupata mabadiriko tunayoyataka.

Imefika kipindi tuwape chama kingine uongozi wa nchi yetu tuone nao kwa Sera zao na mikakati yao nao watatufikisha wapi.

Kiumweli sioni mabadiriko ya msingi nchini chini ya CCM
 
[SUP]kingine kitam zaidi ni kuanza kwa mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100, hii itakuwa zawadi kubwaaa sana kwa wayanzania. [/SUP]

[SUP]napenda Jaji Walioba ashuhudie katiba hii mpya hii ingali akiwa hai[/SUP]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…