CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.
Maendeleo ya kweli yataletwa na Mtanzania mzalendo
wote hawa ni waganga njaa tu.

mkamap:
Mbona unawatwisha mzigo mzito mno hawa ndugu zetu wawili wa hapa JF? Yaani wao wawili tu, 'Mtanzania' na 'Mzalendo' ndio wanayo majukumu ya kutuletea sisi sote maendeleo? Hiyo ni kweli?

Hebu tuwaulize kama majukumu hayo wanayakubali!
 

Iwapo CHADEMA, kama chama cha siasa hawajaweza kuwa na uwezo wa kupambanua mbinu za kisiasa, (tena dhaifu kama hii hapa) zinazoweza kutumika ili kuwasambaratisha; basi hawana, na hawawezi kuwa na uwezo wa kupewa madaraka ya kuendesha nchi. Ningependa kuamini kuwa wamekwishafikia ngazi kiasi ya 'sophistication' ya kuweza kuyajua haya na kuyapuuza, au kuyapiku inavyopasa (kichama), na pia kiuongozi katika ngazi zote. Siwezi kuamini kamwe kuwa watu mwenye ufahamu na uwezo kama wanavyouonyesha, Slaa na Zitto, wanaweza kudanganyika kiurahisi kiasi hicho. Msinipe mfano wa Walid Kabouru kufuta hoja yangu.
 
Muhimu ni kwamba Wangwe kasema openly hili ni moja message sent angalau naona tofauti ta Chadema na CCM hakuna kubanana na kusemea uvunguni .Mikiki ni kawaida penye wengi na kusema Chadema ukabila na Udini ni namna ya kuharibu mambo .Kuna weakness yeah lakini si udini na Chama kisambae Wangwe agombee akipata ataongoza sijaona shida huko Chadema .

CCM wameogopa kwa Mtoro ina watu wa CUF wametumia hata polisi nk kumweka mtu wao .Kisa wanaogopa kushindwa na nado leo hatusemi lolote .Tibaigana anakaa vikao na viongozi wa maadili wa CCM kujaribu kuangusha upinzani pale lwa mtoro si kwa dini bali CCM na uoga lakini hatuyasikii haya mnakomaa na Chadema ?
 
Japokuwa ni mvuta bangi lakini kuna alot of subtances ktk hoja za Wangwe, na mengi ya madai yake yalijadiliwa sana hapa JF...

Yu wapi John Mnyika atupe ufafanuzi kidogo hapa...
 
Kampeni ya Wangwe imeonyesha desperation.Natumia neno "Desperation" ONLY kama yuko honest!sometimes wanasiasa wanakuwa desperate...inakubalika, lakini wanasamehewa kama wako honest!Kwa maana kwamba nia yao ni nzuri kwa chama husika ama taifa kwa ujumla.Nani basi anayejua kama Wangwe is honest wakati wa sakata hilo la vipeperushi?Nani mwingine zaidi anayeweza kujua zaidi ya viongozi wenzake?Kama Chacha Wangwe alishawahi kuibua pointi hizo zilizoko kwenye vipeperushi lakini hakusikilizwa..then kuna possibility kwamba desperation yake ni honest!Sasa CHADEMA wawe makini kwani ni muhimu kusikiliza maoni ya viongozi wengine kwenye vikao muhimu vya chama,kuwa wawazi between each other wakati wa vikao hivyo na kumaliza tofauti zao during vikao hivyo ili kuepuka loopholes!Slaa na Zitto wanamwogopa Wangwe na ndio maana wakajiuzulu!Wamerudi ili kukinusuru chama..Ila nafikri wamewanusuru wapenzi wao!Inawezekana Wangwe tayari ana influence kubwa ndani ya CHADEMA na ndio maana ana nyodo!Hawawezi kumuondoa kwani wanataka kuwanusuru wanachama ambao ni wapenzi wa Wangwe.Nilijua something will happen kama Zitto atakubali kujiunga na kamati ya Rais!Ni makosa yao wao wenyewe kwa kushindwa kutambua watu hatari ndani ya chama!Kama ni kweli CHADEMA kina upendeleo na ukiritimba kiasi ambacho viongozi ndani ya chama wanalalamika waziwazi mbele ya wananchi then kuna hatari humo CHADEMA..
Kwa upande mwingine wa shilingi Mh Wangwe anatia mashaka kidogo!Tuhuma nzito ambazo zinaweza kuleta mgawanyiko ndani ya chama ni budi zikafanyiwa utafiti kabla ya kukurupuka na kuzitoa!Na kama hakuzipeleka kikaoni before then keshanunuliwa huyo..hawezi kukubali kutoka kapa..CCM watatumia loopholes..kuna watu wana pesa,hata kama ingekuwa mimi mwana CCM halafu kuna fungu la kutoa..haa unatoa..kwa sababu kuna opportunity hapo..Zitto ulaji!mimi Wangwe sina ulaji..na ni mwananchama niliyetoa mchango mkubwa na pia mwenye kukubalika na wananachama wengi.Sasa fungu likitembezwa halafu akaweza kujustify hizo kampeni zake mbovu..si mambo mdundo tu!Ni very wazi kwamba Wangwe hafai tena CHADEMA!Kama sio kwamba ni too desperate..then anataka ulaji CCM kwa madai kwamba anaweza kuisambaratisha CHADEMA!Najua CHADEMA wanaogopa kumtema hivi sasa.Lakini tujiulize swali moja..hata kama akishinda Umakamu mwenyekiti si kuna hatari atakisambaratisha chama?Kwasababu hiyo itakuwa ni a very important first step towards party's self destruction.Kwani si iko wazi kwamba sasa hakubaliani na uongozi wa chama na anataka kufanya mabadiliko?Akipewa uenyekiti na kujiimarisha zaidi then si ataondoka na wanachama wengi zaidi kuliko alionao hiv sasa? hivyo ni bora CHADEMA wakaamua kusuka ama kunyoa right now!Some people wanandai kuwa ana ghadhab ya kukosa ulaji wa Kikwete kwenye kamati!Na kama yale aliyokuwa akisema Zitto kuhusu baadhi ya makampuni binafsi kumtumia Wangwe ni kweli then Wangwe atawacost zaidi wasipolitafutia swala hili ufumbuzi ASAP!Kama tuhuma walizokuwa wakizitoa CCM kuhusu CHADEMA ndizo hizohizo anazozitoa Wangwe ambaye ni Mbunge na mwanachama wa CHADEMA anazitoa hadharani kabla ya kuzifikisha vikaoni,halafu akapata huo uongozi si kuna hatari hapo!Honestly kama Wangwe hakuyafikisha hayo maswala kwenye vikao husika kabla ya kuprint vipeperushi..then"APUNGUZWE"
 
Masatu,

Hapa mkuu nakuunga mkono, sikuona neno baya la kutisha watu hadi kufikia kutaka kusambaratika, na nimeshindwa kuelewa kwa nini Dr.Slaa na Zitto walitaka kujiuzuru nafasi zao hali hizi nni siasa za kawaida kabisa ndani ya chama chochote chenye demokrasia ya kweli. Ni maswali ambayo kila mwananchi angependa kuelewa ukweli wake uko wapi.
Kumuonya Chacha haiwezi kusaidia ikiwa maswala haya hayatafanyiwa kazi. Kama ni uongo basi ulitakiwa ukweli kujibu hoja hizo, na kama yalosemwa ni kweli basi mgombea mwenza alitakiwa kutueleza yeye atafanya nini tofauti! kwa sababu Chadema ni chama ambacho kinategemea uwezo wa viongozi wake kuleta mabadiliko hasa ktk maswala nyeti na yanayowagusa wanachama. Wala sio jambo la ajabu ama aibu kuona chama cha Kiafrika kimeshikwa na baadhi ya watu, mabadiliko hayawezi kutokea kama hatuwezi kukubali kutazama mapungufu.

J.J. Mnyika, Zitto, tafadhalini tupeni maji maanake hili tonge limekwama kooni!....
Hoja hujibiwa kwa hoja badala ya mtu kutaka kuachia ngazi....
 
jMushi1,

Mimi naamini siku zote kuwa hoja yoyote ile hujibiwa na hoja.Upinzani ndani ya chama ni dalili kubwa ya kukua kidemokrasia. hata kama maneno alozungumza Chacha yana ukweli - Uongo, awe honest au desperate, tayari ni hoja ambayo inatakiwa kujibiwa ktk uchaguzi huu sema tu alichokosea ni pale aliposhindwa kumshambulia mgombea mwenza wa kiti hicho badala yake ameyaweka madai yake kushutumu uongozi wote wa juu.
Dhahiri hii ni desperation, kwani mtu mmoja huwezi kubadilisha kila kitu ktk chama kwa kuushambulia uongozi mzima hali unachogombea ni nafasi moja. Hiyo nafasi haiwezi kupitisha agenda zote za chama kuleta mabadiliko isipokuwa ni nafasi ambayo itakuwezesha kuwakilisha hoja zako kirahisi zaidi, yet huna kura za kutosha wala vito ya kupitisha yale unayotaka kuwaahidi wananchi.
 
Inachonionyesha ni kwamba upinzani unahitaji moyo kweli kweli wa kujitolea kwa manufaa ya nchi kwa upande wa viongozi wake. Akina Nyerere wasingekuwa na moyo huo Tanganyika tusingepata uhuru mwaka 1961.
 


Udini unaotajwa inaelekea ni kuwa CHADEMA ni chama kinachoendekeza waislamu. Inasemekana uchaguzi wa mwaka 2004 viongozi wengi wa CHADEMA walimuunga mkono Shaibu Akwilombe kwa kuwa ni muislamu wakampinga Dr Kyara ambaye ni mkristu mchaga, matokeo yake ni Kyara kuacha chama na kwenda kuanzisha SAU.

Sasa inasadikiwa wapo viongozi wa CHADEMA wengi waliokuwa wakimuunga mkono Said Arfi Amour mbunge wa Mpanda kwa kuwa ni mzee wa kiislamu wa kusini, kuliko chacha wangwe. Ndio maana washabiki wa Chacha wakasambaza vipeperushi kuwa CHADEMA sio msikiti. Hivi vipeperushi nasikia vimesambazwa zaidi kwetu Zanzibar.

Hivi Maulidah Abobakary Komu naye ni mchaga? Mi nijuavyo ni kuwa huyu ni jirani yetu kule jang'ombe Zanzibar na nimngazija kama sio mtumbatu. Au siku hizi mtu anaweza kubadili kabila? Mbona gazeti la mwanachi limemweka kwamba ni mtu wa uchagani?

Asha
 


Mkandara:

Nakubaliana nawe. Nimeona kwenye tovuti Chacha Wangwe ni mjumbe wa kamati kuu. Na iliwahi kusemwa hapa kuwa ni Mwenyekiti wa mkoa wa Mara. Sasa maamuzi yote ya matumizi ya ruzuku na ripoti za fedha si zinapitia kwenye vikao ambaye yeye ni mjumbe? Kwa nini hakuhoji siku zote badala yake mpaka alipoamua kugombea ndio alalamike kwa vipeperushi? Lakini isije ikiwa wamemwekea maneno, si unakumbuka katika suala la Zitto alilalamika kuwa kuna baadhi ya mambo Mtanzania waliyaweka kumchanganisha? Hivi viongozi wa CHADEMA wako wapi watueleze ukweli wa mambo? Au bado wanaendelea na vikao? Nani ameshinda?

Asha
 
Zuma alifungwa na makuburu, Chacha Alifungwa na Chama Cha Mafisadi. Zuma anawake na watoto wengi, Chacha anawake na watoto wengi. Wote wanapenda siasa za hamasa na mapambano. Zuma ameshinda ANC, Chacha Wangwe anagombea umakamu CHADEMA. Je, akishinda, atakuwa ni Zuma mwingine?

Asha
 

Jamani hii si iinganishwe na ile? Hawa jamaa wako wapi? Mbona wako kimya? au wanaendelea na vikao virefu?

Asha
 
Hiki chama ni weakhead, nilishasema kabla na nitasema tena. Hakuna swala la demokrasia hapo, bali kuna swala la ulafi, maslahi binafsi mbele, wizi na mengineyo mengi.

Chama chenye strong leadership hakina characteristics hata moja ambayo CHADEMA wanayo. Ninachoona hapa ni siasa ya chuki, majungu, story za kinafiki na mengine mengi.

Upinzani wa wakweli utatoka sijui wapi, i can't figure out. Labda JF tuanzishe chama cha upinzani.
 

Asha,

Labda Wangwe na wenzake walihoji na hakusikilizwa na ndio maana sasa wanaamua kutoa siri yote nje?

Suala la kuwa na wabunge wote wanne wa kuteuliwa kutoka mkoa mmoja naona haikuwa judgement nzuri kwa uongozi wa CHADEMA hata kama hao ndio walikuwa na sifa zaidi ya wengine.

Kuteua mbunge toka sehemu nyingine ingelikuwa changamoto hata ya kuimarisha chama huo upande mwingine. Maana kama kuna Mbunge wa CHADEMA Rukwa, ni rahisi wananchi kuijua CHADEMA kuliko sehemu ambako hawana mbunge.
 
Mnajua tangu sera ya vyama vingi ianze nchini nadhani CCM na Sirikali yake waliashaamua kuwa kamwe chama cha upinzani hakitachukua madaraka. Na hadi sasa wameweza kufanikiwa kwani katika vyama vyote vya upinzani wengi wa viongozi wao bado wapo kwenye payroll ya CCM/Sirikali na ni Ma spy wao.

Maugomvi kwenye vyama vya upinzani si yamenza tangia mika ya tisini? Yaani wanagombana mpaka chama chenyewe kinasambaratika. Ukiangalia unaona kuwa tangia enzi za NCCR walipoanza kuwa na nguvu tu vurugu ikaanza, CUF nako vivyo hivyo, nk, sasa ni zamu ya CHADEMA na CCM watakiasambaratisha tu.
 
Fafanua ya Wangwe kuwa na wake wengi na watoto wengi au ushakuwa bint majungu....?????
 
Tunajitengenezea kivuli wenyewe na tunakigopa....MTU KUKIOGOPA KIVULI CHAKE....??
 
TAARIFA KWA UMMA


DONDOO ZA MAAZIMIO YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA CHADEMA


Taarifa hii ni kuwajulisha wanachama wa CHADEMA na watanzania kwa ujumla kuwa Baraza Kuu la CHADEMA lilifanya kikao chake katika kawaida cha kila mwaka siku ya jumanne tarehe 18 Disemba 2007 katika ukumbi wa Hoteli ya Land Mark Dar es salaam.

Ajenda katika kikao hicho zilikuwa: Kuthibitisha Muktasari wa kikao cha Baraza Kuu cha tarehe 12 Agosti 2006 na yatokanayo na muktasari huo; Taarifa ya Katibu Mkuu; Taarifa ya Fedha; Mpango Kazi na Bajeti; Kanuni za Umoja wa Madiwani; Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA mwaka 2008; Taarifa ya Ushirikiano wa Vyama na Kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti(Bara).

Zifuatazo ni dondoo za msingi kuhusu maazimio yaliyofikiwa na kikao cha Baraza Kuu kuhusu ajenda mbalimbali zilizojadiliwa:

Baraza kuu limepokea, kujadili na kupitisha taarifa ya Katibu Mkuu

Taarifa hii kwa pamoja na mambo mengine imejumuisha kazi mbalimbali ambazo CHADEMA imezifanya katika mwaka 2007. Taarifa hii imehusisha pia taarifa za kurugenzi mbalimbali za makao makuu ya CHADEMA. Baraza kuu limesikitishwa na taarifa potofu za magazeti zenye kulenga kujenga taswira kwamba kuna mgogoro. Baraza kuu limepokea na kutathmini Ziara ya helikopta ya kushukuru wananchi, kuhamasisha uwajibakaji wa serikali na kujenga chama na kubaini manufaa yaliyopatikana kutokana na ziara hiyo kwa CHADEMA na kwa taifa.

Baraza kuu imejadili na kupokea taarifa ya fedha ya CHADEMA

Taarifa hii imehusisha mapato na matumizi ya CHADEMA katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Baraza kuu limetafakari gharama za ziara za helikopta na kuwianisha na ziara nyingine na kuazimia kwa kauli moja kuendelea na kutumia helikopta katika za awamu nyingine za CHADEMA kama ambavyo iliazimiwa pia na Mkutano Mkuu wa CHADEMA mwaka 2006.

Baraza Kuu limepokea, kujadili na kupitisha Mpango Kazi na Bajeti kwa mwaka 2008:

Mpango Kazi na Bajeti unajumuisha Shughuli mbalimbali ambazo zimepangwa kufanya katika mwaka 2008 pamoja na bajeti ya kutekeleza mpango huo. Mpango Kazi huo utahusisha shughuli ambazo zitafanywa pia na kurugenzi mbalimbali za chama katika masuala ya utawala, uenezi, habari, sheria, bunge, halmashauri,vijana, wanawake, wazee, rasilimali, oganizesheni, mafunzo, mahusiano ya kimataifa nk.

Baraza Kuu limepokea, kujadili na kuthibitisha Taratibu Umoja wa Madiwani wa CHADEMA

Mwongozo wa Umoja wa Madiwani wa CHADEMA(UMC) unajumuisha madhumuni, uanachama, muundo na masuala mengine muhimu yanayohusu taratibu za umoja wa madiwani wa CHADEMA umeridhiwa. Umoja huu ambao wanachama wake ni kila diwani wa CHADEMA utawaunganisha madiwani wa CHADEMA vizuri zaidi katika kutekeleza wajibu wao katika maeneo wanayowakilisha na kwa chama kwa ujumla.

Baraza kuu limepokea na kujadili taarifa ya ushirikiano wa vyama

Taarifa ya ushirikiano ilijumuisha makubaliano na kazi mbalimbali ambazo zimefanywa na ushirikiano wa vyama vya siasa vya upinzani vya CHADEMA, CUF, TLP na NCCR Mageuzi imepokelewa. Baraza kuu limeazimia kuwa CHADEMA iendelee na ushirikiano wa vyama kwa lengo la kudumisha demokrasia nchini, kuunganisha nguvu katika kutetea maendeleo na hatimaye upinzani kuweza kuchukua dola.

Baraza kuu limepokea, kujadili na kupitisha Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA mwaka 2008:

Ratiba ya uchaguzi mkuu wa CHADEMA imepitishwa rasmi ambapo uchaguzi utafanyika mwaka 2008. Baraza Kuu lilipitisha azimio la kutangaza ratiba ya uchaguzi(Ratiba hiyo imeambatanishwa pamoja na Taarifa hii kwa umma, maelekezo zaidi kuhusu uchaguzi huo yatatolewa baadaye).

Baraza Kuu limefanya uchaguzi na kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti(Bara).

Baraza kuu lilifanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti(Bara). Wagombea wa nafasi hiyo walikuwa: Chacha Zakaya Wangwe(Mb) aliyepata kura-56. Na Said Amour Arfi(Mb) aliyepata kura:- 38 na hakuna kura ambayo iliharibika. Hivyo kwa matokeo hayo Chacha Wangwe(Mb) alitangazwa rasmi kuwa Makamu Mwenyekiti(Bara).



Taarifa hii imetolewa 20/12/2007 na:


Freeman Mbowe
Mwenyekiti Taifa
 

Hakuna ambaye anaweza kuhoji na kutosikilizwa CHADEMA. CHADEMA kama chama cha demokrasia na maendeleo tunaendeshwa na majadiliano na maridhiano. Kila mjumbe wa kikao ana haki na kujenga hoja na mwisho tunaamua kwa makubaliano ya pamoja au kwa kupiga kura.

Unachopaswa kufahamu ni kuwa uteuzi wa wabunge wa viti maalumu hufanyika kabla ya matokeo ya uchaguzi kujulikana. Hii ni kwa mujibu wa sheria. Ndio maana leo unaona Amina Chifupa alifariki nafasi yake haikuzibwa na Vijana ila Tume ya Uchaguzi ilitangaza kutokana na orodha ambayo ilikuwa nayo tayari. Kadhalika mchungaji lwakatare amemrithi hayati Salome Mbatia kutokana na orodha iliyokuwepo tayari.

Hivyo CHADEMA isingeweza kutumia matokeo ya Tarime na Rukwa kwa kuwa hayakuwepo wakati huo. Ingebidi kutumia matokeo ya mwaka 2000 ambapo wakati huo chama hakikuwa kimefanya vizuri wakati huo. Hivyo ilibidi kwa kuwa ilikuwa inajulikana kwamba chama kitapata nafasi chache, maamuzi ilibidi yafanyike centrally- tulitengeneza vigezo vya kupima waombaji wa individual merits na kuwa rank. Hili suala la vigezo vilikuwa ni vipi na mchakato gani ulipitiwa Zitto aliwahi kulijadili hapa huko nyuma, kwa hiyo nashauri MODS wavute zile facts hapa karibu. Nadhani nami nilichangia kidogo wakati huo. Ikibidi nikipata wasaa kama utahitaji nitakuandikia uchambuzi wangu kwa kina. Lakini CHADEMA ni chama kinachotaza mbali zaidi. Mwaka 2006 baada ya uchaguzi tulifanya mabadiliko ya Katiba na kuanzisha mabaraza ya chama ikiwemo la wanawake. Kwa hiyo mwaka 2010 mapendekezo ya viti maalumu vya wanawake yatatokana na uchaguzi wa kugombania miongoni mwa wanawake wenyewe kwanza badala ya chama kuteua kwa ujumla. Kwa hiyo huko mbele mfumo utakuwa bora zaidi. Na msimamo wangu mimi ni tofauti kabisa, hivi viti havipaswi kuwa maalumu kwa staili hii ambayo inaweza kujengwa hisia kwamba wanawake wanabebwa na kupendelewa. Mimi nataka tuwe na mfumo wa kura za uwakakilishi wa uwiano na kama tutapitisha pendekezo la 50-50 basi wanawake na wanaume wote watagombea kwa wananchi kwa ujumla ama kwa chama kwa ujumla na baadaye kwa wananchi bila kujenga hisia za upendeleo.

Hoja ya viti maalum ilijadiliwa kwa uwazi sana kwenye chama mara baada ya uchaguzi- na baraka zikatolewa na Kamati Kuu, Baraza Kuu na hata Mkutano mkuu Agosti 13 mwaka 2006. Ukiona mambo kama haya yanajitokeza tena sasa yakishikiwa bango na baadhi ya magazeti ambayo sera zake zinajulikana inabidi kujiuliza maswali mengi sana.

Mshairi mmoja aliwahi kuasa "Kila unachotazama, usione ukadhani"!

JJ
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…