Mtanzania
Ambacho nakikataa ni watanzania kutokuhoji maneno ya CCM kwamba wabunge wa kuteuliwa wa CHADEMA wote wametoka Kilimanjaro! Ili hali watanzania wanajua kabisa kuwa Mhonga Said na Maulidah Komu hawatoki Kilimanjaro na wala sio wachaga, mmoja wa Kigoma na mwingine wa Kilimanjaro. Na hata hao wengine pamoja na kuwa na asili ya Kilimanjaro ni wawili tu ndio wametoka mkoa wa Kilimanjaro. Wengine wawili wanawakilisha mkoa wa Dar es salaam; mmoja Taasisi za Elimu ya Juu na mmoja Mkoa wa Dar es salaam. Haya ni mambo ambayo umma wa watanzania ni vyema ukaelezwa ukweli against upotofu wa CCM. Ikija kwa CHADEMA watu ni wepesi sana wa kukubali hayo maneno na kusema CHADEMA ijirekebishe! Lakini sijahi kusikia mtu akiwaambia CCM wajirekebishe kwa kuwa tu wabunge wake wa viti maalumu wanaowakilisha mkoa wa Singida wana asili ya Kilimanjaro; wala sijawahi kusikia huu mjadala kuhusu baraza la mawaziri. Let the golden rule appy and not the rule of the thumb here!
Hebu soma vizuri tena post yako- ni kwani nini umwambie mwananchi wa Iringa kuwa CHADEMA kuna ukabila? Je, huo si ubaguzi? Kama unaweza kumwambia hivyo mwananchi wa Iringa, kwa nini usimwambie wa Singida dhidi ya Viti maalumu vya CCM, kwa nini usimwambie wa Kigoma dhidi ya Baraza la Mawaziri la Kikwete?
Mfumo wa wakati huo uliruhusu uliruhusu maamuzi ya wakati huo kwa hiyo yalikuwa mazuri kwa sababu hiyo; mfumo wa 2010 utakuwa mzuri kwa wakati huo kama nilivyodokeza hapo tutatumia Baraza la Wanawake, na utakuwa mzuri kwa wakati huo!
Lakini mimi niko tofauti kabisa, sikubaliani na mifumo yote miwili- tunahitaji uwakilishi wa uwiano na lazima wanawake kwa wanaume wote wakiingizwe katika tanuru la uchaguzi 50-50 badala ya viti maalumu.
Lakini siwezi kusema kwamba haya maoni yangu pekee ndio mazuri- beauty lies on the eyes of the beholder- so I may be right in my right but wrong in yours.
Huu mjadala si mzuri, ni kujilisha upepo!
JJ