CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.
hawa chama makini, walionekana mapema kuwa si makini


wenyewe wapo hapa lkn hawatii mkono, hii imoto.


zitto, mnyika na mafisadi wenzenu njooni muweke sawa hili.



kuna mse mo unasema mchimba kisima.......

Mtu wa Pwani

Hatukuweza kuweka sawa haya mapema hapa. Tulibanwa na vikao vya kutwa kucha. Si unajua tena Baraza Kuu ni kikao cha mara moja kwa mwaka cha kutisha maamuzi yote ya kisera, kwa hiyo ajenda zilikuwa lukuki! Baraza kuu ndio kama Bunge la Bajeti la kupokea ripoti zote za utendaji kwa kila kurugunzi na kupitisha bajeti ya mwaka...Na sisi sekretariati ndio wapishi wenyewe, hivyo wasaa wa kuja hapa ulikuwa lulu.

JJ
 

Mkuu Mnyika,

Ndio maana nilitumia neno judgement maana jambo linaweza kuwa right lakini bado ikawa judgement mbaya.

Hivyo viti ni vya upendeleo kwahiyo hata nyie lazima muwe na mfumo aina fulani wa upendeleo lakini huenda upendeleo wenu umelenga kwenye uwezo wa mtu badala ya kuangalia strategically kama hicho kitu ni jambo zuri au baya. Mungeweza kutoa ranking za wagombea Kikanda ili hata kama ni nafasi nne basi kanda nne nipate wabunge.

Ukimwambia mwananchi wa Iringa kwamba hawa CHADEMA wana ukabila na angalia hata wabunge wao wa kuteuliwa wote wametoka Kilimanjaro, huhitaji hata kutumia dakikia tano kumwelemisha. CCM sio wajinga na lazima tu makosa kama hayo watakuwa wanayatumia.

Ndio maana nafikiri mlichoamua 2005 au kabla ya hapo kwa mawazo yangu kilikuwa si uamuzi mzuri. I hope kama ulivyosema mwenyewe mtarekebisha makosa hayo kwa mwaka 2010.
 

Hongera CHADEMA kwa kumaliza uchaguzi wa makamu mwenyekiti.Kwa kumchagua Wangwe..ni wazi kwamba desperation yake ilikuwa honest!Na sasa hayo aliyoyaibua sasa mkae chini myafanyie kazi!almradi isije ikawa ndio kwanza mwanzo wa "fukuto"Next time mpeane ushirikiano wa kutosha sio muendelee kuimba wimbo wa "kuna demoksia CHADEMA" huku kampeni hatari zikitumika wakati wa uchaguzi ambao ni wa kichama!hivyo kampeni zisiwe zenye kuleta msuguano..badala yake changamoto!Ni wazi kwamba mmeukubali mchango wa Wangwe na ndio maana mmemchagua kuwa makamu m/kiti.Ushauri wangu ni kwamba aitumie nafasi hiyo kuact more professional na kujadili mistakabali muhimu humo vikaoni mwenu!Tumia demokrasia kusema yale yote yaliyo moyoni..BUT..Fumbo mfumbie mjinga mwerevu.....
GOODLUCK!
 

Mtanzania

Ambacho nakikataa ni watanzania kutokuhoji maneno ya CCM kwamba wabunge wa kuteuliwa wa CHADEMA wote wametoka Kilimanjaro! Ili hali watanzania wanajua kabisa kuwa Mhonga Said na Maulidah Komu hawatoki Kilimanjaro na wala sio wachaga, mmoja wa Kigoma na mwingine wa Kilimanjaro. Na hata hao wengine pamoja na kuwa na asili ya Kilimanjaro ni wawili tu ndio wametoka mkoa wa Kilimanjaro. Wengine wawili wanawakilisha mkoa wa Dar es salaam; mmoja Taasisi za Elimu ya Juu na mmoja Mkoa wa Dar es salaam. Haya ni mambo ambayo umma wa watanzania ni vyema ukaelezwa ukweli against upotofu wa CCM. Ikija kwa CHADEMA watu ni wepesi sana wa kukubali hayo maneno na kusema CHADEMA ijirekebishe! Lakini sijahi kusikia mtu akiwaambia CCM wajirekebishe kwa kuwa tu wabunge wake wa viti maalumu wanaowakilisha mkoa wa Singida wana asili ya Kilimanjaro; wala sijawahi kusikia huu mjadala kuhusu baraza la mawaziri. Let the golden rule appy and not the rule of the thumb here!

Hebu soma vizuri tena post yako- ni kwani nini umwambie mwananchi wa Iringa kuwa CHADEMA kuna ukabila? Je, huo si ubaguzi? Kama unaweza kumwambia hivyo mwananchi wa Iringa, kwa nini usimwambie wa Singida dhidi ya Viti maalumu vya CCM, kwa nini usimwambie wa Kigoma dhidi ya Baraza la Mawaziri la Kikwete?

Mfumo wa wakati huo uliruhusu uliruhusu maamuzi ya wakati huo kwa hiyo yalikuwa mazuri kwa sababu hiyo; mfumo wa 2010 utakuwa mzuri kwa wakati huo kama nilivyodokeza hapo tutatumia Baraza la Wanawake, na utakuwa mzuri kwa wakati huo!

Lakini mimi niko tofauti kabisa, sikubaliani na mifumo yote miwili- tunahitaji uwakilishi wa uwiano na lazima wanawake kwa wanaume wote wakiingizwe katika tanuru la uchaguzi 50-50 badala ya viti maalumu.

Lakini siwezi kusema kwamba haya maoni yangu pekee ndio mazuri- beauty lies on the eyes of the beholder- so I may be right in my right but wrong in yours.

Huu mjadala si mzuri, ni kujilisha upepo!

JJ
 

Ila hii 50-50 kupitia PR inahitaji mabadiliko ya Katiba na Sheria ya Uchaguzi. Suala la kujiuliza ni kama serikali ya CCM inadhamira ya dhati ya kutekueleza hayo? Kikwete amesema anatafakari 50-50; Kingunge amesema mjadala wa Katiba Mpya umefungwa rasmi! CCM ijifunze toka kwa ANC, tayari wamepitisha 50-50 kwenye ngazi zao zote za kichama....

Let see the bigger picture hapa guys, mambo mengine ni matokeo ya sheria-imani yangu ni kuwa kama CHADEMA ingefanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum baada ya matokeo ya uchaguzi 2005 lazima kungekuwa na mbunge mmoja wa viti maalumu toka Mara au Rukwa wa viti maalum; lakini sheria hailekezi hivyo. Kwa hiyo wakati unafanya uteuzi, unatumia vigezo vingine na matokeo ya zamani kabisa! Yani hapa naamaanisha, kufanya vizuri kwa CHADEMA Rukwa na Mara matokeo ya sasa yatasaidia wakati wa uteuzi wa 2010, hii inamaanisha nini kama Rukwa na Mara mwaka 2010 matokeo ya Uchaguzi yakishuka(Mungu apishie mbali) halafu ukaibuka mkoa mwingine(labda Mtwara au Lindi) wakafanya vizuri kweli kweli na kwa bahati mbaya wakakosa mtu badala yake akateuliwa wa Mara au Rukwa kwa matokeo ya 2005 basi Lindi na Mtwara vivyo hivyo watasema wametelekezwa! Ndio maana inabidi tutazame picha kubwa zaidi.

Badala ya mjadala kuwa uchaga au si uchaga- mjadala unapaswa kuwa ni marekebisho gani ya kikatiba na kisheria yafanyike ili pawe na mfumo wa uteuzi wa viti maalumu ambao hautaleta hisia za upendeleo wala wanawake kutezwa?

Na huu mjadala wa Viti Maalumu unasura nyingi sana- CCM isingekuwa kama chama dola, mjadala wa UVCCM kudai haki ya kuziba nafasi ya Amina Chifupa kama aliyekuwa mwakilishi wao ungekuwa out of control...the sentiments were contained just because state party as CCM is, it can use carrots and sticks to suppress dissent!

Mjadala huu ni mpana zaidi- by virtue of their appoitment process, to whom are the wabunge wa viti maalum accountable to and how, who are they serving and how? Haya ndio mambo ya kujadili kwa kweli! Why do we have women special seats? Ukisoma ripoti ya TGNP kuhusu miaka 10 ya viti maalumu bungeni utaelewa namaanisha nini


JJ
 

Jmushi1

.....apate kuligundua! Thanx

BTW: Si kila kinachoandikwa na magazeti ndivyo kilivyo au ndivyo kilivyotokea.

Tuendelee kujenga nchi yetu

JJ
 
Yote tisa hivi mnajua ya kuwa asilimia 80 ya wabunge wote ni wasanii? na haswa wabunge wa ccm licha ya kuwa wasanii je mnajua ya kuwa wengi wa wabunge wa ccm ni mbumbumbu hayo nimeyashuhudia mwenye we baada ya kumpokea mbunge mmoja wa ccm ktk uwanja wa ndege wa Hong Kong tena mbunge wa siku njingi, kwa kawaida wabunge wote wana diplomatic passiport cha ajabu yule mbunge siku zote anasafiri eti hajui kuwa pass yake ni diplomatic ni mpaka nilipomchomoa ktk line ya wasafiri wa kawaida na kumpeleka ktk line yake ila nilipatwa na aibu sana kwa kitendo cha mbunge mzima tena wa siku nyingi kutokujua hata wadhfa wake.Hilo ni moja, ushahidi wa pili ni kwamba japokua wabunge wengi utawasikia bungeni wakisema sayansi na tecnolojia tena kwa kujiamini hawajui hata kuwasha computer kama hamuamini mtumieni e mail mbunge Mgana Msindai muone kama anaweza kuifungua. Mimi huwa najiuluza huwa wanatumia mbinu gani mpaka wanakuwa viongozi nashindwa kujua. Sasa hatari ya kiongozi wa namna hii anaweza akatumia mbinu hiyo hiyo aliyotumia kupata ubunge akaukwaa Uwaziri, matokeo ya utendaji wake ikawa ni kilio kwa Taifa maana hata mikataba anayoingia hajui maana yake yeye ni mademu, nyama na bia.
 
Yote tisa hivi mnajua ya kuwa asilimia 80 ya wabunge wote ni wasanii? na haswa wabunge wa ccm

How do we know? Na je, kama hii ni kweli, walio wasanii hapoa ni hao wabunge au wananchi waliowachagua?
 

Mnyika,

Ulichoandika hapo mwanzoni ndicho mlitakiwa kuweka kwenye maelezo yenu, hiyo ni fact ambayo watu wengi, hata mimi mwenyewe nilikuwa sijui juu ya hao wabunge wawili uliowataja.

Siasa ni game na kinachofanywa ni kumzidi mpinzani wako, it doesn't matter huyo mhusika anaishi wapi kwasasa, ni rahisi mno kuwaambia wananchi kwamba kila mwenye jina la Kichaga anatoka Kilimanjaro, au kila mwenye jina la Kisukuma anatoma Mwanza na Shinyanga.

Naona makosa yenu CHADEMA ni kukimbilia kusema na CCM nao wanafanya hivyo. Lakini kwasababu CCM ina wabunge wengi itakuwa ngumu sana kuwabana kwa hilo maana wabunge wao wanatoka karibu kila mkoa wa TZ. Utaweza kuwabana CCM kwenye la ufisadi lakini utatumia nguvu kubwa mno kuwaambia wananchi kwamba CCM kuna ukabila. Hiyo ni my observation kutoka kwa mtu ambaye hana mapenzi na hayo mavyama.

Kuwaambia watu hawawasemi CCM , nafikiri hutendei haki hapa JF maana watu wanaongoza kuisema CCM kuliko CHADEMA. KIla jambo lina mahali pake. Pamoja na maelezo ya Mbowe kwa kweli ni ngumu kupata argument ya kuwalima CCM kwenye hili la kuchagua wabunge toka sehemu moja.

Bado naamini CHADEMA hawakuwa makini kwenye uteuzi wao wa wabunge
wanawake. Wameifanya kazi ya Spini Doctors wa CCM iwe rahisi mno. Kama hiyo haitoshi, inaelekea hata baadhi ya wanachama wenu na baadhi ya viongozi wenu wana question uteuzi huo.
 


Mtanzania

Nashukuru wa kuelewa ufafanuzi wangu katika mambo mengine.

Hapa umeninukuu nje ya muktadha. Nafahamu kuwa CCM inakosolewa JF. Ambacho hakikukosolewa hapa JF ni CCM waliposema CHADEMA ni chama cha wachaga kilichojaa wachaga.Na CCM waliposema wabunge wote wa viti maalum wa CCM ni wachaga, watu walimeza tu kulaumu CHADEMA badala ya kuhoji usahihi wa taarifa waliyopewa. Hakukuwa na mjadala mkali hapa kwamba CCM ni wabaguzi. Kama huu mjadala ulivyozuka hivi sasa, ipo mifano mingine lakini niishie hapa kwa kuwa nisingependa kuendeleza huu mjadala

JJ
 
Ndugu zangu wanaJF sisi sote tunafahamu kuwa sasa jamaa wameamka, wamecharuka kwa njia yoyote wanataka kufanya lolote lile ili kutokomeza upinzani Tanzania, na kwa kuwa Mbowe sasa anatazamwa kwa jicho la husuda na wapinzani wenzake na pia *** sasa ushauri wa bure mbowe akae pembeni ili chama kipone

JF mnalitazamaje hili?
 
Last edited by a moderator:
Rekebisha kichwa cha Mada yako kutoka 'JIUZURU' mpaka "JIUZULU" halafu ndio tuendelee!!! tehe tehe
 

Tueleze: Ni akina nani, wako wapi na wanafanya nini kuutokomeza upinzani?Mbowe ana tatizo gani na ni kwa namna ipi akikaa pembeni chama 'kitapona'?
 
wapinzani gani wamemtazama mbowe kwa jicho la husuda? ...ungeweza kunukuu vipengele vichache tungekuelewa zaidi
 

Changunua ili tuweze kuchangia vizuri. Je ni akina nani wanataka kutokomeza upinzani..., ni wapinzani wenzake au CCM? Hujaeleweka mkuu.
 
Hapa tusiwe na jasiba ndugu zangu, lengo letu ni kukifanya chama hiki chenye nguvu kwa sasa Tz bara kizidi kuwa na mwelekeo.
Na kwa kuwa jana muungano wa vyama vya upinzani (CUF, TLP NA NCCR) wamekanusha yale Zitto aliyokanusha kuwa Tarime hakukuwa na fujo badala yake wapinzani hao kwa pamoja wamesema kuwa kulikuwa na fujo, basi tunaweza kusema vyama hivi havina nia njema na CHADEMA, Na kwa kuwa mafisadi tayari wameshajipanga kufanya wanavyoweza kukipiga chini chama hiki, sasa basi naona ni vema Mbowe akatangaza kuwa amejiuzulu ili waendelee na uchunguzi wao
 
vyovyote iwavyo hali si shwari chadema! ajiuzulu au la? tayari mzimu wa Wangwe uta waganda hadi kila mmoja wao atakapo acha Siasa maana hata katika mila na tamaduni mbali mbali mtu akifariki ukiwa na deni nae walazimika kwenda fanya Ibada, toba nk ili uwe mtu safi mbele ya mungu na mbele ya jamii inayofahamu mgogoro kati ya mhusika mmoja au wengi na marehemu kwa wakati huo. sasa, wangwe kafariki akiwa kasimamishwa uongozi na Chadema, mungu kamchukua tusemeje? amefariki bila kumaliza mgogoro uliokuwepo, wangwe alikuwa na wafuasi kibao, wapambe wa kumwaga labda kama yale aliyokuwa akidai yatatekelezwa mapema kama vile kupeleka ruzuku mikoani kwenye ofisi za chadema, mkoa fulani nilipata kuona ofisi za Chadema ziko zipo kwenye kijiwe cha kukodishia baiskeli na Mkiti wa Mkoa ndiye anaekodisha baiskeli hizo akikusanya miambili miambili! kwa baiskeli zisizo zidi tano , kwa mfano huo waweza ona kazi kubwa aliyotaka kuifanya Wangwe kwa Chadema mikoani,MZIMU WA WANGWE LAZIMA UIGHARIMU CHADEMA KWA NAMNA YOYOTE ILE
 
Last edited:
Vita ya wazalendo dhidi ya mafisadi inahujumiwa na vita baina ya wanasiasa mufilisi dhidi ya CHADEMA. Mafisadi wanafurahia sana wanapoona vyama vya siasa vikiwashambulia CHADEMA na Mbowe/Zitto/Mnyika/Dr. Slaa nk. Wanawezesha huo mchezo kifedha. Wakati mkiendelea na hako kamjadala ka kipuuzi wao waleee wanaendelea kuchota madini yenu na kuwaibia kwa namna nyingi tu.

Haya endeleeni na haka kamchezo kenu ka hatari.
Fungukeni macho watanzania. hakuna fisadi anayechukia chama chenye nguvu. Wanachukia kuwekewa upinzani kwenye wizi wao. Hiki ndiyo chanzo cha mgogoro wao mkubwa dhidi ya CHADEMA na makamanda wake.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…