Mwita una akali sana, tena unafanya haya kwa malengo maalumu na unaweza kufanikiwa.
Si hadithi wala fikra zangu na sija conclude kuhusu kuachia Tarime, nimesema HATA IKIBIDI na nikaongeza "lakini iko kazi" nikijua fika kwamba CCM hawana nafasi Tarime pamoja na kampeni zao chafu na Chadema wana kazi kubwa ya kupambana na kampeni chafu. Kama nimekukera kwa hilo samahani sana na punguza maneno kama "hizo ni hadithi zako" hayo ni maneno yanayoakisi HISIA, MALENGO na MSIMAMO wako ulioegemea kwenye USHAURI ambao nadhani bado una safari ndefu.
Najua ni bahati mbaya sana kwamba hunifahamu, lakini hilo si tatizo ila tatizo kubwa ni kwamba mimi sina upenzi na chama wala mtu yeyote. Sina chama na sitarajii kuwa na chama katika siku za karibuni. Viongozi wa vyama vyote vya siasa ikiwamo CCM niko nao karibu sana. Sidhani kama unataka kukiendeleza chama unachokizungumzia yaani Chadema, labda CCM. Si wakati mwafaka kwa sasa kwa Mbowe kujiuzulu kama unataka kutenda haki. Nadhani kwa sasa Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, ndiye anayepaswa kujiuzulu ama Uenyekiti ama URAIS maana tokea achukue kofia mbili mwaka 2006, nchi/chama haijawahi kutulia na matatizo yamekua mfululizo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa. Mbona hujamshauri ajiuzulu moja ya nafasi zake?