Nimewahi kusema na sasa nasema tena kwamba, si vyema kumuingia mtu moja kwa moja, lakini ni jambo lililo dhahiri kwamba isayamwita si mwana CHADEMA na hawezi kuwa mwana Chadema, lakini kwa kutumia mbinu ya kujifanya mwana chadema, anaweza kuibeba ajenda yake ya kuivuruga na kuizika Chadema kwa urahisi zaidi kwani tokea mwanzo wa mada yake, hakuwa na hoja ya kuhalalisha kujiuzulu kwa Mbowe lakini pamoja na hoja za kumuelewesha, amelazimisha na ameshindwa hata kubadilika japo kidogo. Kwa jinsi anavyoonyesha kuwa mtu mwenye upeo, nina hakika angeweza kubadilika japo kidiogo katika hoja yake ya kumtaka Mbowe ajiuzulu, lakini kwa vile MISSION yake ni MBOWE AJIZULU, anaweza kukubaliana na hoja zote zinazotolewa lakini hitimisho lake litakuwa "Tunasubiri tu M/kiti wetu ajiengue".
Haiwezekani kwamba isayamwita hajui kwamba wakati wa vita huwezi kumtaka Amiri Jeshi mkuu ajiengue au ajiuzulu. Haiwezekani wakati wa vita ndio usema tumuondoe Rais, haiwezekani wakati wa matatizo ndio utake kukigawa chama kama kweli isayamwita ni mwana Chadema, HAIWEZEKANI hata kidogo. Kwa ujumla ninachotaka kusema hapa hii mada tena kwa kusema neno "jiuzuru" badala ya "Jiuzulu" ninaiona kama mada mahususi kwa malengo mahsusi na kwa mkakati wa kujiunga nao ili iwe rahidi kuwageuza akili zao.
Kwa maslahi ya demokrasia ya nchi hii, na kwa USALAMA WA TAIFA la Tanzania, si vyema kwa Chadema kusambaratika hata kidogo. Kuna wana CCM walioumbuka sasa wameanza kutaka kukata "VICHWA" vya nyoka (Chadema, Media) waliowatafuna kwa nia ya kurahisisha kazi yao ya kuelekea 2010-2015 kutawala kama walivyopanga kwamba watatawala kwa miaka 30 ijayo... Kwa bahati mbaya sana hawa wanaopanga hayo si TAASISI, CHAMA, AU WATANZANIA HALISI WENYE NIA NJEMA, bali ni watu waovu, wenye malengo binafsi zaidi, wenye nia ya kuendelea kuwanyonya Watanzania katika kila jambo.
Nilishasema toka mwanzo kwamba muanzisha mada amefanikiwa sana kwa kuwa hadi sasa watu wanajadili Mbowe kujiuzulu, mgogoro ndani ya upinzani,. tatizo la waandishi wa habari na si EPA, RICHMOND, Meremeta, Kiwira, Songas, Alex Stewarts, TICTS, Manji, CCM, Makamba, Lowassa, UVCCM, Nape,UWT, Wazazi, Jeetu Patel, Subash Patel, BoT, na kadhalika na kadhalika na kadhalika..... hayo sasa si ajenda tena..... Jamani TUZINDUKENI TANZANIA UHURU BADO KABISAAAAAAAAAAAAAAA ndio kwanza MAPAMBANO YAMEANZA