CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.
Nimemkashifu au kumshutumu nani hapa? Sijamkataza mtu kutoa maoni yake kwa sababu hicho ndicho nilichokifanya mimi (kutoa maoni), sasa kwa nini niwakataze wengine kitu ambacho mimi ninakifanya?
Sijajifunga katika itikadi yoyote kisiasa, nimemua niwe huru

Mpita Njia,

Unaweza kunielewa vibaya, lakini ni vema kuzingatia mantiki na hoja iliyoko mbele yetu, jambo la kutosimama ndani ya misingi ya hoja ndipo hapo najaribu kusema si vizuri,

Mpita njia utakaporudi katika Thread hii ujaribu kubainisha ni nini kifanyike ili Demokrasia hai iendelezwe na si vinginevyo, tayari umeshasema kuwa hauna itikadi yoyote, sasa sisi wana chadema tunaendelea kuzichanga na kufikiri ni wapi tunaweza kuboresha ili demokrasia izidi kukua na mwisho tuwakimbize hawa mafisadi
 
Well,Hili suala la kusema Mbowe ajiuzulu ni sawa kama kuna hoja za kutosha.so far hakuna hoja za maana maanke yote yanaonekana ni uzushi.Mbowe ajiuzulu kwa lipi maanke kama ishu ni hii yaWangwe basi inabidi kauli ibadilike iwe kamati kuu ya CHADEMA ijiuzulu.

NCHIMBI,

Tunaomba usije ukafikiri kwa hizo hoja zako hapo juu za kujifanya uko upande wa mhe.Mbowe zitakufanya uonekane kashfa zinazokuandama kule kwenu zitazuia mawazo ya watu huru ndani ya chama chako huko kwenu kujenga hoja za kukuwajibisha.Ubabe wako ndani ya UVCCM ni wa kweli acha kujisogeza huku ili uonekane unaonewa.

Back to the point,Suala la CHADEMA kujitanua nchi nzima ndilo la msingi sasa ikizingatiwa zaidi kuna local government's election next year.

Pia kwanza kuna hili suala la Kufungua matawi nje ya Nchi,mpaka sasa huku India tuna Tawi moja lakini bado kadi hazijatolewa.Idadi kubwa ya wanachama ni wanafunzi wa mwaka wa pili na wa Tatu ambao next year watakua home.

Vijana wengi wanavutiwa na CHADEMA kutokana na sera na pia hoja za Wabunge wa CHADEMA Bungeni zinavuta hisia za vijana wengi.sasa leo hii hii stori ya kutaka Mbowe a-resign nadhani haijengi sana kwa muada huu hasa pale ambapo hoja haziwezi kusimama

Hebu Dr.W.Slaa tafadhali tunaomba utupe mkakati wa kujiandaa na election zijazo hasa katika viti vya ubunge!

Ben,

Nashukuru kwa uelewa wako, ila naomba usijenge misingi ya kusema kuwa ni uzushi, CCM wa njia nyingi sana za kuweza kukitokomeza chama hiki cha CHADEMA.

Hawa mafisadi walipoona wanafuatiliwa wakaona wabadili mwelekeo wa upepo, sasa unaona hata waandishi wameshindwa kuandika mambo ya kitaifa sasa wamejikita kwa maswala yasiyokuwa ya maana

Ni vema tukajua kuwa KWENYE ZILE MBIO ZA VIJITI HUWA KUNA WASAIDIZI,Sasa pale tunapogungua mkimbiaji anapitwa na naelekea kupumua kwa shida, hapo ndipo hutafutwa mtu mbadala wa kumsaidia
 
NCHIMBI,

Haya ndiyo yaliyojaza fuadi yako, mtizamo wako butu, sijui umeielewa mada? pole sana ndugu yangu.

Sisi wanachadema tutaendelea kubolesha ili tupate ushindani zaidi, kujiuzulu kwa m/kiti wetu ni sera wala si ushabiki wa ninyi Mafisadi, Mbowe kashaona na atafanya maamuzi yake hasa tukiendelea kumshauri ili chama chetu kipone.

Ninasema tena najua CCM mtafanya kila linalowezekana kutaka kukipiku chama chetu 2010 hata kile kidogo tulichonacho, fikra zetu hazijasahau, mlifanya hivyo kwa NCCR na ndiyo maana mafisadi sasa mnajitahidi kukichafua chama hiki cha chadema, najua Mola yu pamoja nasi.

Tunaendelea kutafakari ni jinsi gani CCM wasivyokuwa na haya jamani, wamesahau kwa kupitia vyama vya upinzani mengi yameweza kuibuliwa, tumegundua uozo kwa taifa letu

Mungu ibariki Tanzania

Mungu inusuru Tanzania
kwanza mawazo yangu siyo butu kama unavyojalipu kuonyesha bila vithibitisho wala uchambuzi yakinifu.Pia unasema kuwa kujiuzulu kwa mwenyekiti wenu ni sera[policy] na siyo ushabiki...sina uhakika kama ni sera kweli ya chadema kama unavyosema wewe kuwa inapotokea kuna msuguano ndani ya chama,mmoja wa washindani anafariki kwa bahati mbaya,aliekuwa wakisuguana naye anatakiwa ajiuzuru....ni kifungu gani cha sera kinachosema hivyo.itakuwa ni sera ya ajabu kwelikweli hio.Mbowe hapaswi kujiuzulu kwa maneno yasiyo na uthibitisho wa kinadhalia wala kisayansi,hukoatakuwa hajaitendea nafsi yake haki.
 
Well,Hili suala la kusema Mbowe ajiuzulu ni sawa kama kuna hoja za kutosha.so far hakuna hoja za maana maanke yote yanaonekana ni uzushi.Mbowe ajiuzulu kwa lipi maanke kama ishu ni hii yaWangwe basi inabidi kauli ibadilike iwe kamati kuu ya CHADEMA ijiuzulu.

NCHIMBI,

Tunaomba usije ukafikiri kwa hizo hoja zako hapo juu za kujifanya uko upande wa mhe.Mbowe zitakufanya uonekane kashfa zinazokuandama kule kwenu zitazuia mawazo ya watu huru ndani ya chama chako huko kwenu kujenga hoja za kukuwajibisha.Ubabe wako ndani ya UVCCM ni wa kweli acha kujisogeza huku ili uonekane unaonewa.

Back to the point,Suala la CHADEMA kujitanua nchi nzima ndilo la msingi sasa ikizingatiwa zaidi kuna local government's election next year.

Pia kwanza kuna hili suala la Kufungua matawi nje ya Nchi,mpaka sasa huku India tuna Tawi moja lakini bado kadi hazijatolewa.Idadi kubwa ya wanachama ni wanafunzi wa mwaka wa pili na wa Tatu ambao next year watakua home.

Vijana wengi wanavutiwa na CHADEMA kutokana na sera na pia hoja za Wabunge wa CHADEMA Bungeni zinavuta hisia za vijana wengi.sasa leo hii hii stori ya kutaka Mbowe a-resign nadhani haijengi sana kwa muada huu hasa pale ambapo hoja haziwezi kusimama

Hebu Dr.W.Slaa tafadhali tunaomba utupe mkakati wa kujiandaa na election zijazo hasa katika viti vya ubunge!

Hoja inayojadiliwa hapa siyo kujisogeza wala kujiweka karibu na Mbowe ila ni kusimamia ukweli wa yale nayoyaamini.nia yangu ni kuonyesha irrationality ya Mbowe kujiuzulu....siamini shutuma zako zinazotoka nje ya mada kama vile ubabe wako ndani ya uvccm,kuziba kashfa zako zina uhusiano na mada ilioko.Au ni njia ya kuninyima haki ya kutoa mawazo yangu????kama unaamini kuwa sipaswi kutoa mawazo yangu kama mtanzania huru basi niambie nilijue hilo.vcc
 
Lakini Haya Tunayo Yasikia Kuhusu Mbowe Na Sla Yanakatisha Tamaa Slaa Was My Gun For 2o10 But It Seems Is Fugizzi,,,,,,,,,feck
 
Hoja inayojadiliwa hapa siyo kujisogeza wala kujiweka karibu na Mbowe ila ni kusimamia ukweli wa yale nayoyaamini.nia yangu ni kuonyesha irrationality ya Mbowe kujiuzulu....siamini shutuma zako zinazotoka nje ya mada kama vile ubabe wako ndani ya uvccm,kuziba kashfa zako zina uhusiano na mada ilioko.Au ni njia ya kuninyima haki ya kutoa mawazo yangu????kama unaamini kuwa sipaswi kutoa mawazo yangu kama mtanzania huru basi niambie nilijue hilo.vcc

Hakuna aliyekunyima haki ya kutoa maoni.Tanzania tunahitaji viongozi wanosema kile wanachoweza kukiweka katika practicals.
 
kwanza mawazo yangu siyo butu kama unavyojalipu kuonyesha bila vithibitisho wala uchambuzi yakinifu.Pia unasema kuwa kujiuzulu kwa mwenyekiti wenu ni sera[policy] na siyo ushabiki...sina uhakika kama ni sera kweli ya chadema kama unavyosema wewe kuwa inapotokea kuna msuguano ndani ya chama,mmoja wa washindani anafariki kwa bahati mbaya,aliekuwa wakisuguana naye anatakiwa ajiuzuru....ni kifungu gani cha sera kinachosema hivyo.itakuwa ni sera ya ajabu kwelikweli hio.Mbowe hapaswi kujiuzulu kwa maneno yasiyo na uthibitisho wa kinadhalia wala kisayansi,hukoatakuwa hajaitendea nafsi yake haki.

Nchimbi,

Nashukuru sana kwa upenduzi wako yakinifu, tunajua mipango yenu na mikakati yetu dhidi ya CHADEMA, ni kukitokomeza na si vinginevyo.
Umenifanya nikumbuke wale wanasheria wako na jinsi walivyokuwa na mkwara,100 million, hey man, time will tell u guy,

Sawa msisitizo wako nimeupata na najua umekuja hapa kutia kazi, lakini zingatia mada na kisha jikite kuijadili Mkuu.

Hoja ni kwamba M/kiti wetu atatakiwa kukaa pembeni ili awanyime pa kusemea, haiwezekani kumpandia maneno, oooh ..., na ndiyo maana tumeamua kumshauri M/kiti wetu, na kizuri zaidi Mbowe ni msikivu na anaendelea kutafakari.
 
By Friday Simbaya, PST, Iringa

President Jakaya Kikwete on Thursday commended Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) for participating fully in his just-ended nine-day tour of Iringa Region.

Je hizi ni dalili za kumeguka kwa chama?

Hapana ilibidi wawepo watoe tathimini ya ziara ya Rais independently na kwa taarifa wameshaandika report ya ziara hiyo kwa chama chao.Ukumbuke vilevile kuwa viongozi wa ngazi za chini wa CCm ni waoga kukutana na viongozi wenzao,hivyo njia imetumika kuwafundisha kuwa upinzani sio uadui ila ni ushindani wa kisera.Kwa kifupi ilikuwa fundisho kwa wenye fikra mgando wa mfumo wa chama kimoja.
 
Hoja inayojadiliwa hapa siyo kujisogeza wala kujiweka karibu na Mbowe ila ni kusimamia ukweli wa yale nayoyaamini.nia yangu ni kuonyesha irrationality ya Mbowe kujiuzulu....siamini shutuma zako zinazotoka nje ya mada kama vile ubabe wako ndani ya uvccm,kuziba kashfa zako zina uhusiano na mada ilioko.Au ni njia ya kuninyima haki ya kutoa mawazo yangu????kama unaamini kuwa sipaswi kutoa mawazo yangu kama mtanzania huru basi niambie nilijue hilo.vcc

Bravo Mwenyekiti wa Vijana,

Kwanza kabisa siwezi kuamini kwamba uchangiji wako kwenye huu mjadala utakua sincere kwa sababu,

1. Wewe huna Tofauti na akina RA na hivyo malengo yenu kwa CHADEMA ni mabaya tu,si ni wanamtandao wote?

2. katika huu mchezo wa siasa chafu dhidi ya chama chetu wewe huwezi kulikwepa hili maanake mlishatangaza azma yenu ya kumshughulikia Mbowe na Chama chake.Kwa hili naomba usitufanye sisi wananchi wajinga maanke ingawa umekuja in a positive mood,inawezekana kabisa hata uliyoandika huwezi kuyasimamia.

3. Huwezi kuwashauri wan-CHADEMA jambo lolote ambalo ni constructive kwani hata ndani ya Chama chako wewe umeshindwa kusimamia demokrasia,kumbuka Mpango wako against kijana Nape Nnauye na jengo lenu la UVCCM.Sasa kama huna nia nzuri na wanaCCM wenzako utaweza vipi kutusaidia sisi katika huu mjadala.

Simaanishi kwamba huna haki ya kutoa maoni au CHADEMA hawataki ushauri kutoka nje,lakini inategemea huo ushauri uko motivated na nini hasa.So far umeonekana kutetea Mhe. Mbowe asijiuzulu lakini hiyo mimi najua ni kutokana na hulka yako mkuu ya kupenda madaraka kuliko ilivyo kawaida.Maanke mkuu mbinu zako unazotumia pale maslahi yako yanapoguswa ni kielelezo tosha.

Nakushauri tu ukae pembeni ingwa sikulazimishi,na uwaachie CHADEMA wajadili mambo yao kwa ufanisi maanke hadi tunafikia hatua ya baadhi ya wananchi kumtaka Mbowe ajiuzulu kwa kiasi fulani imechangiwa na mkakati wa watu wako wa karibu au ikiwezekana na wewe ni mmoja wapo.That is to say wewe unaweza kuwa sehemu ya tatizo,and it is funny indeed kama wewe utajidai kuwa part ya solution.
 
Mimi nilishindwa kumwambia sawasawa, nikabaki niking'atang'ata meno ndugu yangu, bora umemueleza,hawa jamaa ni hatari, yaani hawana hata chembe ya huruma kwa watoto wa kitanzania, yaani wee acha tu..............

Niko karibu kuanzisha mjadara wa kitaifa kuhusu anguko la CCM, na hapo ndipo tutawapata wanachama wema(Kondoo) wa CCM, watu kama Butiku, Sinde Waryoba na wengine wengi

Tunasubiri tu M/kiti wetu ajiengue, Kisha tuanze mjadala huu ambao utakuwa ni maandalizi 2010, Karibu wana CCM ndani ya behewa hili(CHADEMA) Yale mapungufu mnayoyasikia tunaendelea kuboresha, karibuni ndugu zangu, njooni na viatu vyenu
 
Nimewahi kusema na sasa nasema tena kwamba, si vyema kumuingia mtu moja kwa moja, lakini ni jambo lililo dhahiri kwamba isayamwita si mwana CHADEMA na hawezi kuwa mwana Chadema, lakini kwa kutumia mbinu ya kujifanya mwana chadema, anaweza kuibeba ajenda yake ya kuivuruga na kuizika Chadema kwa urahisi zaidi kwani tokea mwanzo wa mada yake, hakuwa na hoja ya kuhalalisha kujiuzulu kwa Mbowe lakini pamoja na hoja za kumuelewesha, amelazimisha na ameshindwa hata kubadilika japo kidogo. Kwa jinsi anavyoonyesha kuwa mtu mwenye upeo, nina hakika angeweza kubadilika japo kidiogo katika hoja yake ya kumtaka Mbowe ajiuzulu, lakini kwa vile MISSION yake ni MBOWE AJIZULU, anaweza kukubaliana na hoja zote zinazotolewa lakini hitimisho lake litakuwa "Tunasubiri tu M/kiti wetu ajiengue".

Haiwezekani kwamba isayamwita hajui kwamba wakati wa vita huwezi kumtaka Amiri Jeshi mkuu ajiengue au ajiuzulu. Haiwezekani wakati wa vita ndio usema tumuondoe Rais, haiwezekani wakati wa matatizo ndio utake kukigawa chama kama kweli isayamwita ni mwana Chadema, HAIWEZEKANI hata kidogo. Kwa ujumla ninachotaka kusema hapa hii mada tena kwa kusema neno "jiuzuru" badala ya "Jiuzulu" ninaiona kama mada mahususi kwa malengo mahsusi na kwa mkakati wa kujiunga nao ili iwe rahidi kuwageuza akili zao.

Kwa maslahi ya demokrasia ya nchi hii, na kwa USALAMA WA TAIFA la Tanzania, si vyema kwa Chadema kusambaratika hata kidogo. Kuna wana CCM walioumbuka sasa wameanza kutaka kukata "VICHWA" vya nyoka (Chadema, Media) waliowatafuna kwa nia ya kurahisisha kazi yao ya kuelekea 2010-2015 kutawala kama walivyopanga kwamba watatawala kwa miaka 30 ijayo... Kwa bahati mbaya sana hawa wanaopanga hayo si TAASISI, CHAMA, AU WATANZANIA HALISI WENYE NIA NJEMA, bali ni watu waovu, wenye malengo binafsi zaidi, wenye nia ya kuendelea kuwanyonya Watanzania katika kila jambo.

Nilishasema toka mwanzo kwamba muanzisha mada amefanikiwa sana kwa kuwa hadi sasa watu wanajadili Mbowe kujiuzulu, mgogoro ndani ya upinzani,. tatizo la waandishi wa habari na si EPA, RICHMOND, Meremeta, Kiwira, Songas, Alex Stewarts, TICTS, Manji, CCM, Makamba, Lowassa, UVCCM, Nape,UWT, Wazazi, Jeetu Patel, Subash Patel, BoT, na kadhalika na kadhalika na kadhalika..... hayo sasa si ajenda tena..... Jamani TUZINDUKENI TANZANIA UHURU BADO KABISAAAAAAAAAAAAAAA ndio kwanza MAPAMBANO YAMEANZA
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 5 (3 members and 2 guests)
Halisi, isayamwita, TechMaro
 
Mkuu Halisi umesema kweli tupu, chukua kumi zote mkuu wangu!

Ni ukweli ulio wazi kwamba hii ni janja ya kuwaacha mafisadi wezi na manyangau wote wa raslimali zetu wapumue! yaani badala watu tuwakabe makoo hao wezi wetu tuna ngangana na kuwataka wapiganaji waachie ngazi!! come'on and wake up guys! Tusi waache mafisadi wapumue hata kidogo warudishe kilicho chetu kuanzia EPA, RICHMOND BOT bila kuwasahau wadogo zake kina KIWIRA na nyumba zetu walizojigawia..
 
Ben,

Mimi nilishindwa kumwambia sawasawa, nikabaki niking'atang'ata meno ndugu yangu, bora umemueleza,hawa jamaa ni hatari, yaani hawana hata chembe ya huruma kwa watoto wa kitanzania, yaani wee acha tu..............

Niko karibu kuanzisha mjadara wa kitaifa kuhusu anguko la CCM, na hapo ndipo tutawapata wanachama wema(Kondoo) wa CCM, watu kama Butiku, Sinde Waryoba na wengine wengi

Tunasubiri tu M/kiti wetu ajiengue, Kisha tuanze mjadala huu ambao utakuwa ni maandalizi 2010, Karibu wana CCM ndani ya behewa hili(CHADEMA) Yale mapungufu mnayoyasikia tunaendelea kuboresha, karibuni ndugu zangu, njooni na viatu vyenu

Kwanza Nchimbi, J, si Mwenyekiti wa UVCCM. Mwenyekiti wa UVCCM ni Emmanuel Nchimbi.. Pia hili jina unaweza hata kulitumia wewe au yeyote hadi pale tunapoweza kuthibitisha vinginevyo, kwa hiyo kwa kutaka tuanze kujibizana tukijua tunajibizana na Nchimbi yule Naibu Waziri wa Ulinzi, yule mjumbe wa CC ya CCM, yule Mwenyekiti wa UVCCM, itakuwa kupoteza nguvu za watu bureee.... huyu siye hadi yeye mwenyewe atamke hivyo au kama aliwahi kutamka hapa, mwenye kumbukumbu atupe
 
Nimewahi kusema na sasa nasema tena kwamba, si vyema kumuingia mtu moja kwa moja, lakini ni jambo lililo dhahiri kwamba isayamwita si mwana CHADEMA na hawezi kuwa mwana Chadema, lakini kwa kutumia mbinu ya kujifanya mwana chadema, anaweza kuibeba ajenda yake ya kuivuruga na kuizika Chadema kwa urahisi zaidi kwani tokea mwanzo wa mada yake, hakuwa na hoja ya kuhalalisha kujiuzulu kwa Mbowe lakini pamoja na hoja za kumuelewesha, amelazimisha na ameshindwa hata kubadilika japo kidogo. Kwa jinsi anavyoonyesha kuwa mtu mwenye upeo, nina hakika angeweza kubadilika japo kidiogo katika hoja yake ya kumtaka Mbowe ajiuzulu, lakini kwa vile MISSION yake ni MBOWE AJIZULU, anaweza kukubaliana na hoja zote zinazotolewa lakini hitimisho lake litakuwa "Tunasubiri tu M/kiti wetu ajiengue".

Haiwezekani kwamba isayamwita hajui kwamba wakati wa vita huwezi kumtaka Amiri Jeshi mkuu ajiengue au ajiuzulu. Haiwezekani wakati wa vita ndio usema tumuondoe Rais, haiwezekani wakati wa matatizo ndio utake kukigawa chama kama kweli isayamwita ni mwana Chadema, HAIWEZEKANI hata kidogo. Kwa ujumla ninachotaka kusema hapa hii mada tena kwa kusema neno "jiuzuru" badala ya "Jiuzulu" ninaiona kama mada mahususi kwa malengo mahsusi na kwa mkakati wa kujiunga nao ili iwe rahidi kuwageuza akili zao.

Kwa maslahi ya demokrasia ya nchi hii, na kwa USALAMA WA TAIFA la Tanzania, si vyema kwa Chadema kusambaratika hata kidogo. Kuna wana CCM walioumbuka sasa wameanza kutaka kukata "VICHWA" vya nyoka (Chadema, Media) waliowatafuna kwa nia ya kurahisisha kazi yao ya kuelekea 2010-2015 kutawala kama walivyopanga kwamba watatawala kwa miaka 30 ijayo... Kwa bahati mbaya sana hawa wanaopanga hayo si TAASISI, CHAMA, AU WATANZANIA HALISI WENYE NIA NJEMA, bali ni watu waovu, wenye malengo binafsi zaidi, wenye nia ya kuendelea kuwanyonya Watanzania katika kila jambo.

Nilishasema toka mwanzo kwamba muanzisha mada amefanikiwa sana kwa kuwa hadi sasa watu wanajadili Mbowe kujiuzulu, mgogoro ndani ya upinzani,. tatizo la waandishi wa habari na si EPA, RICHMOND, Meremeta, Kiwira, Songas, Alex Stewarts, TICTS, Manji, CCM, Makamba, Lowassa, UVCCM, Nape,UWT, Wazazi, Jeetu Patel, Subash Patel, BoT, na kadhalika na kadhalika na kadhalika..... hayo sasa si ajenda tena..... Jamani TUZINDUKENI TANZANIA UHURU BADO KABISAAAAAAAAAAAAAAA ndio kwanza MAPAMBANO YAMEANZA

Halisi,
Nashukuru sana kwa Mtizamo wako huo, na nimefadhaishwa sana kwa kile kinachotawala fuadi yako, naendelea kusema na ninasema tusiwe kama kupe, nadhani hapo umenifahamu.

Hoja yangu ya Kumtaka M/kiti ajiuzulu niliisema KINADHALIA SANA,na sikutaka kuziweka reason zozote hapa, tofauti na unavyoibainisha kwa sasa, na kwa kuwa umebainisha kuwa wakati wa mapambano Amiri jeshi hapaswi kuchomoka, na hata kama yeye ndiye atakayejiuzulu na vita iishe, wewe umeona si vema,basi mimi nasema na asijiuzulu.

Ni vipi kama leo akaitisha comfrence na akatangaza kuwa amejiuzulu nini kitafuata? chama kitakufa? ninini hasa kitatokea? Hapana nimegundua yawezekana tukakosa mtu mahili kama yeye eti?

Nimefurahishwa kuwa wewe unadhani ndiye tu mwana Chadema, nataka nikufahamishe kuwa chama hiki kwa sasa ni cha kitaifa, naomba ulielewe hilo, na kwa kuwa umeonesha interest yako hadharani bila kuzingatia hoja, hakika umenisononesha sana Mkuu.

Tazama sana Mbio za vijiti, watu wanne kwenye mstari, mbio kuzitimka, akichoka mmoja basi atapokelewa na mwenza.

...M/kiti wetu ni mtu makini, na hapa jamvini anafika na pia anayasoma haya,wala usimsemeee, akaiona kwamba bado anapenda kukiendeleza chama atatueleza na pia tutamuuliza mikakati aliyonayo 2010,wenzako tumeanza kuzichanga 2010 ili tuwe na hoja, tunataka kutofautiana na CUF, TLP na HATA NCCR, mamwekiti(Lipumba, Mremana Mbatia) ni walewale miaka nenda rudi, utazadhani hakuna watu mbadala, hakika tia akili Mkuu

Mungu ibariki Tanzania

Mungu kinusuru Chama cha CHADEMA.;
 
Kwa majibu ya haya uliyoyasema, soma post uliyoijibu hapo juu. Naamini umenielewa ila MISSION bado iko pale pale.... Kwa saikolojia ndogo tu, unaweza kupata picha.... iko kazi
 
Kwanza Nchimbi, J, si Mwenyekiti wa UVCCM. Mwenyekiti wa UVCCM ni Emmanuel Nchimbi.. Pia hili jina unaweza hata kulitumia wewe au yeyote hadi pale tunapoweza kuthibitisha vinginevyo, kwa hiyo kwa kutaka tuanze kujibizana tukijua tunajibizana na Nchimbi yule Naibu Waziri wa Ulinzi, yule mjumbe wa CC ya CCM, yule Mwenyekiti wa UVCCM, itakuwa kupoteza nguvu za watu bureee.... huyu siye hadi yeye mwenyewe atamke hivyo au kama aliwahi kutamka hapa, mwenye kumbukumbu atupe

Ndugu yangu nakushukuru sana,unachosema hapa ni kweli kabisa.mimi sikutaka kujadili mimi ni nani na kuacha hoja kwa kuwa najua hapa tunajadili hoja na sio watu...Kuna watu walisema mimi ni kiongozi wa uvccm,nilinyamaza kwa kuwa ni kweli mimi ni kiongozizi wa uvccm tena baraza kuu taifa.Lakini mimi sio Emanuel Nchimbi....kama nilivyoandika mimi ni nchimbi,john.
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 5 (3 members and 2 guests)
Halisi, isayamwita, TechMaro

Halisi
Unachekesha sana, Unadhani ni nani mwanaJF anayeweza Kudhubutu kama hana kifua kama nilivyofavya mimi? hisia za uoga zimetawala sana ktk forum hii, na ndiyo maana hauwezi kuwaona watu wakijimwaga ktk thread hii, ina upupu, ni kama shumiri, hata wewe kujibu hoja hii ni tumtetea mhusika bila hoja na wala si vinginevyo.

Halisi

Ukirudi hapa unijibu, haya yafuatayo,

(a) Bila M/kiti wetu wa sasa, chama hakina vision ama?(BILA MBOWE HAKUNA CHADEMA?)

(b) Ni kwanini unadhani wewe ndiye mwanachadema pekee na hakuna yeyote anayestahili kutoa mawazo yake kwa uhuru zaidi?

(c) Je unanufaikaje na M/ kiti wetu kuwepo madarakani kwa sasa?

Mimi nimekueleza mara nyingi kuwa chama cha CHADEMA ndicho chama mbadala, na chama chenye sura ya kitaifa kwa sasa, kina wanachama wengi kwa sasa na ni nchi nzima, wapo wasomo na wasiowasomi kama mimi.

Kitendo unachofanya cha kutetea ili hali ukijua chama kinataka mabadiliko katika uongozi wa juu, hakika unakuwa unapotoka, najua yawezekana kuna chochote unachogema kwa sasa, ila tumia akili kidogo Mkuu

M/Kiti wetu popote ulipo Ujumbe huu unaupata endelea kutafakari, na fikiri sana, haya yanayosemwa ni mema kwa chama chetu ulichokijenga vyema na utanaendelea, fikiri sana kisha njoo na wazo litakolokufanya uitwe MWANAMAPINDUZI

Mungu ibariki Tanzania

Mungu kinusuru chama cha CHADEMA
 
Isayamwita mbona hueleweki? naomba unijazie majibu haya kama kweli unasababu za msingi
-Ni nani amejenga management system ya CHADEMA, ni vikao au Mbowe?
-Nani anayetekeleza? Vikao? Mbowe au Dr. Slaa?
-Panapotokea matatizo katika management system nani anaehusika kurekebisha? Vikao, Mbowe au Dr. Slaa?
-Mfumo upi wewe unapendekeza kuimarisha management system? Kubadili watu au kupitia upya system?
-Mara nyingi usipende kukimbilia kufukuza au kujiuzulu

No body is perfect, do investigation then evaluate before you conclude my friend. Pia kama unaona unahoja ya msingi na muhimu better ukajua ni nzuri based on convicing majority sio umahiri wa kusema na kuwa mtu wa magoli ya kuotea.

Nakusifu kwa kusimamia ulionalo BUT jenga hoja please.

Asante
 
Halisi
Unachekesha sana, Unadhani ni nani mwanaJF anayeweza Kudhubutu kama hana kifua kama nilivyofavya mimi? hisia za uoga zimetawala sana ktk forum hii, na ndiyo maana hauwezi kuwaona watu wakijimwaga ktk thread hii, ina upupu, ni kama shumiri, hata wewe kujibu hoja hii ni tumtetea mhusika bila hoja na wala si vinginevyo.

Halisi

Ukirudi hapa unijibu, haya yafuatayo,

(a) Bila M/kiti wetu wa sasa, chama hakina vision ama?(BILA MBOWE HAKUNA CHADEMA?)

(b) Ni kwanini unadhani wewe ndiye mwanachadema pekee na hakuna yeyote anayestahili kutoa mawazo yake kwa uhuru zaidi?

(c) Je unanufaikaje na M/ kiti wetu kuwepo madarakani kwa sasa?

Mimi nimekueleza mara nyingi kuwa chama cha CHADEMA ndicho chama mbadala, na chama chenye sura ya kitaifa kwa sasa, kina wanachama wengi kwa sasa na ni nchi nzima, wapo wasomo na wasiowasomi kama mimi.

Kitendo unachofanya cha kutetea ili hali ukijua chama kinataka mabadiliko katika uongozi wa juu, hakika unakuwa unapotoka, najua yawezekana kuna chochote unachogema kwa sasa, ila tumia akili kidogo Mkuu

M/Kiti wetu popote ulipo Ujumbe huu unaupata endelea kutafakari, na fikiri sana, haya yanayosemwa ni mema kwa chama chetu ulichokijenga vyema na utanaendelea, fikiri sana kisha njoo na wazo litakolokufanya uitwe MWANAMAPINDUZI

Mungu ibariki Tanzania

Mungu kinusuru chama cha CHADEMA
(b) Ni kwanini unadhani wewe ndiye mwanachadema pekee na hakuna yeyote anayestahili kutoa mawazo yake kwa uhuru zaidi?

Kama una kumbukumbu, rudia majibu ya mwanzo. Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Umesoma lakini unajifanya kipofu.

(c) Je unanufaikaje na M/ kiti wetu kuwepo madarakani kwa sasa?

Mwenyekiti wako na nani? Wana Chadema wanaochangia humu, hata mmoja hatumii neno "Mwenyekiti wetu, Chama Chetu" wewe kutumia maneno hayo, unajionyesha dhahiri picha na malengo yako. NImeshasema iko kazi na kwa mazingira ya Tanzania ya sasa unaweza kufanikiwa kwa Chadema lakini hutaweza kuzuia kasi ya ukombozi inayoenea kwa kasi nchi nzima.

Mimi nimekueleza mara nyingi kuwa chama cha CHADEMA ndicho chama mbadala, na chama chenye sura ya kitaifa kwa sasa, kina wanachama wengi kwa sasa na ni nchi nzima, wapo wasomo na wasiowasomi kama mimi.

Unafiki mtupu.

Kitendo unachofanya cha kutetea ili hali ukijua chama kinataka mabadiliko katika uongozi wa juu, hakika unakuwa unapotoka, najua yawezekana kuna chochote unachogema kwa sasa, ila tumia akili kidogo Mkuu

Bahati mbaya sana hujui ulisemalo, na kama unajua unapindisha ukweli kwa kulinda maslahi ya tabaka unalolitumikia si vinginevyo.

M/Kiti wetu popote ulipo Ujumbe huu unaupata endelea kutafakari, na fikiri sana, haya yanayosemwa ni mema kwa chama chetu ulichokijenga vyema na utanaendelea, fikiri sana kisha njoo na wazo litakolokufanya uitwe MWANAMAPINDUZI

Mwenyekiti wako si Mbowe, unamjua wewe na wenzako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom