Ndugu zangu wanaJF sisi sote tunafahamu kuwa sasa jamaa wameamka, wamecharuka kwa njia yoyote wanataka kufanya lolote lile ili kutokomeza upinzani Tanzania, na kwa kuwa Mbowe sasa anatazamwa kwa jicho la husuda na wapinzani wenzake na pia *** sasa ushauri wa bure mbowe akae pembeni ili chama kipone
JF mnalitazamaje hili?
Mwita
Ukiangalia wapinzani sio kwamba hawalioni wanaliona sana ila kwa vile malengo yao ni umaarufu na kujipatia fedha na si kwamba wanatafuta demokrasia ya kweli.Yani ni kama wasomi wetu serikalini si kwamba hawaoni wala hawajui mbinu ambazo zinaweza kutuondolea umasikini bali kwa umasikini wetu kwao ndio raha maana wanafalsafa yao ni bora tajiri kuzungukwa na masikini maana ataabudiwa kama miungu ,kuliko tajiri ndani ya midle class.
Maana kwa umasikini wetu wao kuingia mikataba ya 10% ni rahisi mno kuliko kwa taifa lenye matajiri na midle class.
Mimi sidhani kama upinzani wa chama utabadirisha matokeo,nafikiri matekeo yatabadirishwa na mtu mmoja ambaye atakua mzalendo wa kweli ,mfurukutwa ,mwenye nia ya kuondoa umasikini na anayeungwa mkono na watanzania wengi.
Nchi ngapi za afrika zimebadirisha na kuweka wapinzani,angalia Kibaki wa kenya wakati yupo upinzani alivyokua anaimba nyimbo za demokrasia lakini kaingia madarakani nini kimetokea?
Athari za kuamini kila ukisikiacho ndo kama hizi unaweza kuja na swala jema kabisa kama hili la Mbowe ajiuzulu bila ya kuwa na fact finding kwani siku zote ukweli utabaki kuwa ukweli na ubabaishaji utajulikana hebu tujiulize maswali yafutayo
1. Je mbowe ndiyo anayefanya maamuzi yote ya chadema ama maamuzi yale hufanywa kwa misingi ya katiba ya chama ambayo ndiyo iliyosajiliwa kwa msajili wa vyama vya siasa?
2. Je mwenyekiti wa chama kama mawazo yake hayakubaliwi na vikao halali ana kura ya veto au turufu na kama ipo inafanya kazi katika mazingira yapi?
3. Je tukiyumbisha CHADEMA leo tuna chama mbadala cha kuikosoa serikali haswa kwa upande wa TZ bara?
4. Je siasa ya Tanzania inatoa mwanya wa at least fair play in the game?
pamoja na masuala mengine mengi ndipo tuchanganue hali halisi ya MBowe na CHADEMA ilipo na ilipotoka ni kina nani wapo nyuma ya pazia kama wadhamini, wajumbe wa mikutano mikuu na vikao mbali mbali vya kitaifa na je katiba ya CHADEMA inafuatwa ipasavyo ama na wenyewe katiba ni document ya kwenye shelf la vitabu ????
tusiwe wavivu wa kuchanganua mambo na kurukia kudandia gari kwa mbeli ukidhani utawahi kufika kumbe watakufikisha pahala pengine!!!!
Mkama,
Hakika ni lazima uwe na mtizamo wa kimapinduzi, achana na hayo mawazo mgando kuwa kuweka vyama vya upinzani ktk utawala huenda kusiwe na mabadiliko, hiyo si kweli, Kenya wamepiga hatua kidemokrasia, na ndiyo maana nikasema kwa kuwa CHADEMA ina sura ya kitaifa ni vema sasa tukapata viongozi imara ili kuendeleza gurudumu lile
Mwita.
Leo nimefunga kitabu cha kuongelea chadema ,ila nitaongelea mtu mmoja mmoja kama JK,Zito,Mbowe nk.
Ushauri wangu ni kua ni Jambo hatari sana kukubali kuidaganya akili yumkini akili yenyewe inatambu sivyo inavyojaribu kuamrishwa aimini.
Sitokataa wala kubali ya kua CHADEMA ni chama mbadala na nichama chenye sura ya kitaifa.Mimi nitasubiri hukumu ya mwaka 2010 ili kuthibitisha hilo.Mungu tujalie uzima hadi tarehe hiyo.
Nakutakia kila yaliyo mema ktk shughuri zako zakukifanya chama cha kitaifa.
Sasa unajichanganya kidogo mkuu. Sababu ulizotoa za kumtaka Mbowe ajiuzulu ndio hasa zinazomfanya awe na sifa za kumfanya aendelee kuwa kiongozi wa CHADEMA kuliko mwanachadema mwingine. Kama CCM wanamhara na kumwandama Mbowe hiyo ndiyo sifa tunayotaka kwa kiongozi wa upinzani. Kama wewe ni kiongozi wa upinzani na CCM hawakosi usingizi kwa ajili yako, wewe hufai kuwa kiongozi wa upinzani.
Halafu unakiri kwa maandishi yako kuwa Mbowe amefanya kazi kubwa ya kukuza demokrasia nchini, sasa cha ajabu unataka tena ajiuzulu.
Labda unisaidie kidogo hapa, wewe mwenzetu unataka sifa gani kwa kiongozi wa upinzani? Unataka kiongozi awe goigoi, asiyeikosesha CCM usingizi, anayesifiwa na akina Makamba, au namna gani, hebu tuweke sawa!
Rekebisha kichwa cha Mada yako kutoka 'JIUZURU' mpaka "JIUZULU" halafu ndio tuendelee!!! tehe tehe
Halisi,
CHADEMA ni chama cha kitaifa kwa sasa, hisia zako kuwa ni vema tukapoteza kule Tarime hakika mkuu hapo sijakuelewa, wana tarime ni wanamageuzi fikra zako kuwa huenda CCM ina nafasi kule Tarime hizo ni hadithi zako
Halisi tunajua kuwa na upenzi na ushabiki bila tija si vema, ni vema tukajikita kukiendeleza chama na kuepuka yale yote yanayoweza kuwapa watanzania kigugumizi.
CHADEMA ni chama cha kitaifa kwa sasa, hisia zako kuwa ni vema tukapoteza kule Tarime hakika mkuu hapo sijakuelewa, wana tarime ni wanamageuzi fikra zako kuwa huenda CCM ina nafasi kule Tarime hizo ni hadithi zako
Halisi tunajua kuwa na upenzi na ushabiki bila tija si vema, ni vema tukajikita kukiendeleza chama na kuepuka yale yote yanayoweza kuwapa watanzania kigugumizi
Sina ujuzi sana wa masuala ya Chadema lakini ninavyoona kupitia nmaandishi na hali ya mambo ilivyo, ni vigumu sana kutenganisha Mbowe na Chadema. Ninachomaanisha ni kuwa uhai wa Chadema unategemea zaidi Mbowe. Ninaamini kuwa Chadema itakuwa katika hatari ya kufa iwapo Mbowe ataondoka hivi sasa
Mwita una akali sana, tena unafanya haya kwa malengo maalumu na unaweza kufanikiwa.
Si hadithi wala fikra zangu na sija conclude kuhusu kuachia Tarime, nimesema HATA IKIBIDI na nikaongeza "lakini iko kazi" nikijua fika kwamba CCM hawana nafasi Tarime pamoja na kampeni zao chafu na Chadema wana kazi kubwa ya kupambana na kampeni chafu. Kama nimekukera kwa hilo samahani sana na punguza maneno kama "hizo ni hadithi zako" hayo ni maneno yanayoakisi HISIA, MALENGO na MSIMAMO wako ulioegemea kwenye USHAURI ambao nadhani bado una safari ndefu.
Najua ni bahati mbaya sana kwamba hunifahamu, lakini hilo si tatizo ila tatizo kubwa ni kwamba mimi sina upenzi na chama wala mtu yeyote. Sina chama na sitarajii kuwa na chama katika siku za karibuni. Viongozi wa vyama vyote vya siasa ikiwamo CCM niko nao karibu sana. Sidhani kama unataka kukiendeleza chama unachokizungumzia yaani Chadema, labda CCM. Si wakati mwafaka kwa sasa kwa Mbowe kujiuzulu kama unataka kutenda haki. Nadhani kwa sasa Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, ndiye anayepaswa kujiuzulu ama Uenyekiti ama URAIS maana tokea achukue kofia mbili mwaka 2006, nchi/chama haijawahi kutulia na matatizo yamekua mfululizo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa. Mbona hujamshauri ajiuzulu moja ya nafasi zake?
Ni maono yangu tu mkuu. Ninaamini kabisa kuwa Chadema inaendelea kusurvive kwa sababu ya Mbowe. Si kwa nguvu ya fedha pekee, bali kwa uwezo wake wa kuwaweka watu pamoja kama chama
Vita ya wazalendo dhidi ya mafisadi inahujumiwa na vita baina ya wanasiasa mufilisi dhidi ya CHADEMA. Mafisadi wanafurahia sana wanapoona vyama vya siasa vikiwashambulia CHADEMA na Mbowe/Zitto/Mnyika/Dr. Slaa nk. Wanawezesha huo mchezo kifedha. Wakati mkiendelea na hako kamjadala ka kipuuzi wao waleee wanaendelea kuchota madini yenu na kuwaibia kwa namna nyingi tu.
Kamende,
Hakika umenena jambo la maana mafisadi si watu wema lengo lao ni kuhakikisha wanaitokomeza demokrasia hapa nchini ili wapate nafasi tena ya kuiuza nchii hii
Kweli, mafisadi waliapa kumshughulikia, chadema chini ya mbowe ndio waliongoza vita hiyo. Hii hela na aliyeandika huenda amelipwa. Mbowe anza kazi sasa bila kurudi nyuma. Tuko na wewe