CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.

Kichwa Ngumu,

Naomba sana uelewe kuwa sisi hatuko hapa kujivua nguo zetu, ni vipi Kichwa ngumu ukamkuta baba yako yuko uchi utamwambia jirani yako eti baba leo alikuwa uchi?

Na ungependa nianze na lipi kukujibu Mkuu? Lakini si vema kukubishia Mkuu wangu usije ukawalazimisha hao jamaa zako wakanifungia hapa jamnvini, ila tia akili mkuu.
 


Halisi,

Nashukuru kwa kuwa nyeusi wewe unaona ni Nyekundu, Nyeupe haa.......... ni Kijani, hakuna shida Mkuu, Mawazo yako ni mazuri kama yatasadifiwa,Majority wakiyasoma haya unayoyatetea hakika wanabaki midomo wazi, wanashindwa kuamini kama na wewe una kaufahamu.Lakini wewe ni bawabu namba ngapi Mkuu? Je unamjua Bi, Kilembwe?

Halisi

Natumia sana lugha ya mficho ili kuainisha hapa hoja, natumia sana NADHALIA kuliko ..............., naomba unielewe Mkuu.

Halisi

Kila mtu huamini kile anachodhani kinaweza kuleta tija kwa taifa na si vinginevyo, na kwa kuwa wewe haunipi shida kuujua mtizamo wako, na fikra zako za sasa Mkuu, najua hayo ndiyo unayoyaamini ndani ya fuadi yako.

Halisi

Matusi na kashfa si mahali pake hapa, jenga hoja na kisha zisimamie, acha ushabiki bila hoja, kwa mantiki hii naanza kujua wewe si mpiganaji bali................, kweli taifa hili iko kazi, tukipata halisi kama 3 hakika nchii haikomboki kamwe.

Hebu wewe halisi unataka tuamini hayo unayoyaamini? ni kweli kwa sasa ndani ya chama hakuna haja ya kufanya mabadiliko ya M/ kiti? sasa tutatofautianaje na CUF, TLP hata NCCR? Itakuwa ni ajabu kama hatutaanza mikakati ya kuwa nia thabiti kwa watanzania hawa.

Halisi

Hakuna kitu kibaya kama mapenzi, unajua ukishapenda hauoni chongo, ukiambiwa mpenzi wako ana chongo basi hapo vita itazuka, zogo moja kwa moja, ndiyo maana unayoyaandika hapa hauwapi watu shida na hakuna anayekuunga Mkono bali wewe kujisimamia mwenyewe, jaribu sana kusikiliza hoja na pia pata wakati wa kutafakari.

Mungu ibariki Tanzania

Mungu Kinusuru CHADEMA na hawa Mafisadi
 
mbowe hafai hata kuongoza nzi seuze chama

muhuni si wa kumuamini anastahili na yeye auwawe tu bila ya huruma
 

Mkuu,
Jibu yote ndio niungae na wewe kusema Mbowe jiuzulu. Kwa sababu zako naona wa kwanza kujiuzulu ni Dr. Slaa na Zitto. Sasa wakisema wamemuona baba yako mida fulani halafu wakati huo alikuwa uchi si utawarahisishia kuwa hata mimi nilimuona wakati huo alikuwa uchi ili tujadili cause root na jinsi ya kumsaidia.
Mkuu weka mambo hadharani

asante
 


Agenda21......
 

Japo huna hoja ya kulazimisha unachotaka kitokee, hata ungekua na hoja unapaswa kuwa MKWELI. Jambo lililo wazi ni kwamba kazi unayoifanya ina tija na huenda ukafanikiwa lakini mujue harufu ya dhambi itawahukumu na kuwalaani. Mbowe si malaika wala nabii, ana udhaifu wake na kwamba kama ilivyo kwa kifo, hatabaki milele kuwa Mwenyekiti, lakini unapaswa ujenge hoja zenye mashiko kutaka kulazimisha unachojaribu kukiweka humu. Najua unachosimamia na pia najua pia mkakati uliopo kwa sasa. Lakini mujue fika kwamba Tanzania LAZIMA IKOMBOLEWE na inawezekana kabisa Chadema haina uwezo wa kuikomboa NCHI lakini nchi itakuja kukombolewa hata na vichaa kwa kuwa watu wamechoka Mungu aepushe mbali lakini kwa watu kuchoka watakuja hata kumpa mtu asiyestahili na hiyo ndio maana nasema mikakati ya kuua upinzani ni HATARI KWA USALAMA WA TAIFA na kama wana Usalama wetu watakubali kushirikiana na MAFISADI kuua upinzani ili kutimiza matakwa yao ya kisiasa, wajue wanahatarisha USALAMA WA TAIFA. Wewe umejilazimisha kwamba ni mwana Chadema wakati sio iko siku utabaini dhambi ya unayoyafanya itaathiri hata watu wanaokuhusu na hayo MASLAHI makubwa uliyonayo unayopigania hayatasaidia nchi yako wala wakuhusuo.



Kweli wewe ndiye mpiganaji kwa kulazimisha bila kuja na hoja. Hoja yako ya mwanzo kabisa imejengeka na tofauti iliyojitokeza kati ya Chadema na wapinzani na kwamba wewe mwenyewe umeelezea kukerwa na wapinzani lakini badala ya kuwaambia kina Lipumba wakae pembeni, unaibuka na kutaka Mbowe ajiuzulu. Niko tayari kukubaliana na wewe kama utajenga hoja zinazolenga kwa DHATI kutetea maslahi, ustawi na usalama wa Taifa la Tanzania na si kujenga kwa kujifanya unatetea Chadema kama chama chako bila kuzingatia UTAIFA.... Kama ukija na Hoja za msingi na utatuzi, hakuna atakayeweza kukupinga lakini si hoja zinazopikwa katika chungu kimoja mtaa fulani pale na kulishwa katika vinywa vya watu wakitumia vyombo na watu wanaofahamika. Tunawajua, tunapajua na tunavijua.


Sina nimpendaye, kama hutaki kuamini niliyokwambia toka mwanzo sikulazimishi. Fuatilia post zote nilizochangia toka mwanzo, nimewahi kuwatetea viongozi wa CCM kwa nguvu zangu zote na waliosema mimi CCM nikawa nawaangalia tu. Nimekuja juzi juzi kuwatetea CUF kwa nguvu zangu zote, waliokuwa wanasoma wakawa wananiita mimi Mpemba wa CUF, juzi juzi nikamtetea Lowassa katika moja ya mada humu, watu wakasema mimi nimenunuliwa na mafisadi, lakini nataka uelewe nisichopenda ni UNAFIKI na hoja za kulazimisha. Kama una jambo uliloficha weka hadharani, na kama kweli wewe ni CHADEMA nadhani ndio kabisa andika waraka kama wa WANGWE uupeleka panapohusika. Baadaye tupe chama mbadala na pia tuambie kwa kina kati ya Mbowe na Kikwete ni nani anayepaswa kujiuzulu kwanza? Maana kama Lowassa ambaye amekuwa mpiganaji akaondoka kwa tuhuma za ufisadi, kwanini wengine, akiwamo Kikwete asijiuzulu? Kwani CCM hakuna mtu anayeweza kuwa Mwenyekiti wa CCM? Miaka mitatu tumekuwa katika vurugu tupu, tukapoozwa na ujio wa Bush na baadae Sulivan... lakini hakuna kupumua. Lakini pia ukija na hoja ya kutaka Kikwete ajiuzulu, tutajadili na pia tutakupinga na kujenga hoja kwamba, inabidi abaki hadi baada ya 2010 ndio tunaweza kujadili kujiuzulu kwake, na ndio sasa tunajadili UTUPE HOJA ZA MSINGI.
 

Unakumbuka haya uliyoyasema mwanzo? Sasa kama mfano wapinzani wanataka kuitokomeza CCM, ushauri ni Mwenyekiti wa CCM ajiuzulu? Kama Osama anataka kuwamaliza Wamarekani, dawa ni Bush kujiuzulu? Nadhani leta hoja ili hata Wana-Chadema 'wenzako' wakuelewe.
 
mbowe hafai hata kuongoza nzi seuze chama

muhuni si wa kumuamini anastahili na yeye auwawe tu bila ya huruma

Mtu wa Pwani,

Hakika kwa jina lako sasa naanza kujua ni jinsi gani watu wa pwani walivyo, hebu kumbe wana maneno ya namna hii....., haipendezi, nadhani wewe mtu wa pwani hata umri wako ni kati ya 18- 23, na kama utakuwa umeuzidi umri huu, basi wewe ni mtoto wa ......, kula jasho letu si shida.

Nashangaa ni vipi unaweza kuruhusiwa kuchangia hapa jamnvini mpaka sasa, unawezaje kumuhukumu mtu asiyekuwa na hatia?

Tizama sana mbalamwezi, nadhani uponyaji wako wa ak... utaupata mkuu, si vema hata kidogo kuchupia hoja na kutoka ndani ya mada.

Tuambie mna ugomvi na jamaa?
Akili kidogo itakufanya uheshimike.
 

Kichwangumu,

Hakika nimeamini kweli kichwa chako kigumu sana , nimegunduwa kuwa wewe ni mgumu wa kuelewa pia mwepesi wa kusahau

Nimekufahanisha kuwa ukimkuta baba yako yuko uchi, unaweza kutoka nje na kuanza kulindima , ooooh!!!!! njoooni mumone baba yuko uchi? ni vema sana ukakuwa kiakili na kuzingatia mada, hasa ukijikita na yaliyopo mbele yetu na si vinginevyo.

Kwa maneno machache tu, kama leo M/kiti wa CHADEMA akijiuzulu je chadema itatoweka ktk ramani ya kisiasa Tanzania?

Nilijalibu kukujibu kikubwa sana wala sikutaka kubainisha sababu za msingi, sasa wewe Kichwangumu ilikuwa kazi kwako kutafakari na kujiuliza, yafuatayo

(a) Je kuna ulazima wowote wa M/kiti kujiweka pembeni kwa sasa?

(b) Nini mtizamo wetu wa kidemokrasia kwa siku za usoni?

Kichwa ngumu hapa kinachotakiwa ni kuiboresha Demokrasia na kuwanyima Mafisadi Fursa za kujipenyeza katika demokrasia hii changa inayochipua ndani ya Taifa letu, ili wasipate nafasi ya kuifisadi.

Tia akili Kichwangumu na si vinginevyo.
 

Halisi,

Ile slogan yako ya king'ang'anizi umeibadili Mkuu?

Kesho tutegemee ipi?

Mimi ni mkulima Mkuu, napenda kujifunza mazuri toka kwa wenzangu

Halisi,hakika kweli nimeng'amua kile unachokijua, kisha nimelewa uelewa wako Mkuu, ila kuwa kigeugeu si jambo jema hata kidogo, umesema wewe umewahi kuwatetea CCM, CUF na haukuishia hapo mkuu, umesema wewe ni mseto, hakika umenifadhaisha sana.

Nataka ufanane na mimi, pigania kile unachokiamini kama kina tija kwa taifa kwa siku za usoni bila kujali upenzi wako dhidi ya muhusika.

Najua pole pole utarudi na kusimama pamoja na mimi na kuona kile ninachokiamini kina tija kwetu sote, na wewe utaniunga mkono siko moja.

Tazama ulivyo, unashindwa kujua 2+2= 4? Huuu nao ni mlinganyo?

Utazani umelishwa yamini, oohhhh...., ukiruka hapa tu oooohh utaota matiti, basi hapo utatetea ili mradi tu usiote matiti.

Tuko pamoja Mkuu.
 

Tazama moyo wako ulivyo, tazama unavyoyajumuisha bila uchambuzi yakinifu, tazama ulivyoathirika, yaani unataka tuige mwongozo wa CCM, Halisi unajua fikra bora ni silaha njema kwa mpinzani wako, jaribu kuwa makini pale unapochangia mjadala
 

Tazama moyo wako ulivyo, tazama unavyoyajumuisha bila uchambuzi yakinifu, tazama ulivyoathirika kisaikojia, yaani unataka tuige mwongozo wa CCM, Halisi unajua fikra bora ni silaha njema kwa mpinzani wako, jaribu kuwa makini pale unapochangia mjadala,pia usisahau kuwa hapa wanapita watu waliokwenda shule.
 
Kuna watu humu nimegundua wao ni CCM au Chadema au CUF, basi kiongozi wake akikosea lazima amtetee tu hata akiiba lazima amteteee tu.

Hiyo ndio inayotutofautisha sisi na nyie.

Halisi, unapoteza muda mkuu, huyu jamaa amesha made up his mind so dont confuse him with facts!. nahisi umenielewa. Hawa ni piga ufe mimi nitabishana milele kuitete Yanga Africa. kwi kwi kwiii


Asante

Fairplayer
 

Mkuu asante kwa ushauri wako, nitabofya baadae hebu tuachane na mambo ya baba yupo uchi.

Lakini hebu niambie matatizo ya Mbowe 'personal' ambayo unahisi hayamfanyi awe na credits za kuendelea kuongoza CHADEMA ni vipi? mbali ya personal, ni zipi za ziada?

Nakushukuru tena kwa kusimamia hoja yako.
 

Eeeeh!, mbona zimetajwa humu mara nyingi sana?; usiniambie hujawahi kuzisoma!. Put in your mind sisemi ni za kweli au za uongo.
 

Kichwa ngumu,

Naanza kuamini sasa kichwa chako kimelainika, umeanza kuelewa, hata kama ni kwa mafungu, nitakuwa ninakosea sana jamii hii ya Kitanzania kama nitaanza kupotosha jamii yetu na kuiweka jamii yetu njia panda,ninafahamu kuwa hakuna kitu kibaya kama Mapenzi, unajua unaweza kumuua mtu ukimkuta mtu ana mwenza wako?

Hoja ya kumuomba M/kiti wa chadema kukaa pembeni ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa hili na watu wake wote, bila kujali rangi, kabila na hata matabaka

Kwa sasa tunataka tupate mtu makini zaidi, ambaye ataweza kurisukuma gurudumu hili linaloonekana kusuasua, hii inafanyika tu kwa mapenzi mema hasa ukizingatia Chama hiki sasa kina sura ya kitaifa

Kicha rahisi(kichwangumu)

Tazama sasa kama tunaweza kumpata mtu anayeweza kuleta umoja wetu wa kitaifa na kuzingatia maslahi ya Taifa hili, huku akijitenga kabisa na biashara na kuzingatia ukombozi wa taifa hili, inaweza kuwa vema.

Hili linawezekana kama tu, CHADEMA tutakuwa tayari kujiandaa ili kupigana na hawa mafisadi wa nchi hii, tunaelewa kuwa kuna kundi la wasomi wengi hapa Tanzania wanatuunga Mkono japo ni kwa siri , haitoshi tunazidi kusema karibuni nyote ili(wasomi) mlete ubunifu ndani ya chama chetu

Mungu ibariki Tanzania

Mungu kinusuru chadema na hawa mafisadi wa Taifa letu.
 

Kichwangumu,

Hapa hatupo kwa ajili ya kumjadili Mtu na matatizo yake, tupa hapa jamnvini ili kukiboresha chama na kuleta mabadiliko ndani ya chama chetu, tukianza kumjadili M/kiti kesho tutamjadili Katibu na kesho kutwa..........!!!,

Tazama, jiulize ni kwanini watu kama Mwanakijiji, Pundit, jmush1,invisible na wengine wengi hawaijadili hoja hii? hapa ndipo utajua hoja hii ni kama upupu, kwani imejikita sana kwenye ukweli kuliko Majungu
 
Eeeeh!, mbona zimetajwa humu mara nyingi sana?; usiniambie hujawahi kuzisoma!. Put in your mind sisemi ni za kweli au za uongo.

FairPlayer,

Naomba ukurudi hapa uje na hoja za kuboresha mjadala na si vinginevyo, zingatia sana mada, jiepushe kubainisha udhaifu wa mtu mmoja mmoja, jikite sana ni wapi tunaweza kurekebisha na Demokrasia yetu ikakua, ukizingatia kuwa hawa CCM wametusahau sisi watoto wa maskini kule vijijini.

Watoto wa Mafisadi ndiyo wenye fursa ya kusoma vizuri, ndiyo wenye haki ya kuishi,haki ya kuoa na kuelewa, Kurithishana madaraka, hatushangai kusikia Mtoto wa Mwinyi kesho ndiye Rais wa Taifa hili hali hana uwezo wa kuliongoza Taifa hili.

Tunajaribu kila tunaloweza kumpata Kiongozi wa Upinzani ATAKAYEUZIKA 2010, tunataka tuongeze wabunge wengi bungeni, na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumefanya mageuzi ya kweli, hayo yanawezekana kama tu tutafanya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya chama hiki(CHADEMA) chenye sura ya kitaifa.
 
Ndugu wana JF mjadala ni mzuri na nimecopy kwenye hardcopy nitawanye huku kwenye vijiwe vya kyela.
Asanteni sana
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…