CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.
Ndugu wana JF mjadala ni mzuri na nimecopy kwenye hardcopy nitawanye huku kwenye vijiwe vya kyela.
Asanteni sana

Nsaji Mpoki,

Usiishie kucopy my young brother, tukiwa wa kucopy na kupest basi hapa tutalishana pumba hadi tuvembewe, Tazama, kama utaona maada hii imekuingia ikakukomboa kifkra, hakika utakuwa umeboreka zaidi kuliko kushabikia bila kuzingatia yale tunayoyajadili hapa,

Nchi hii ni yetu sote, tuijenge, tuipiganie, haijalishi hata kama tutafanywa KAFARA kwa leo kizazi chetu kijacho kitashangilia, Nsaji wewe ni shaidi wa maisha ya kizazi hiki ambacho sasa wachache tu ndiyo wamiliki wa njia za uchumi wa Taifa hili, hii haiwezekani kabisa.

Na ndiyo Maaana tumeanza kufikiri na hata kutafakari ni nini tufanye ili tukiboreshe chama hiki cha CHADEMA, chama mbadala, kimbilio la Watanzania bara, na Visiwani, sauti ya wanyonge, wajane kwa mayatima hapa ndiyo mahali pao.

Tunataka Mtu mwenye uchungu na Taifa hili, Mtu mwenye mwelekeo chanya na mkombozi wa Taifa hili, huku akijitahidi kujiepusha na maslahi Binafsi(biashara) zaidi akitafakari matatizo ya watu wake hawa maskini.

Tunajua Taifa letu limeuzwa, wakoloni wamerudi kwa mlango wa nyuma, sasa wanapora na wala hakuna makubaliano hata kidogo, tukibisha tu basi hapo patasitishwa misaada na mengineyo.

Mnashuhudia taifa letu na watu wake wakiwa katika msuguano wa kimaslahi, Wafanyakazi, Walimu, Madakitari na hata wanafunzi, hii ni hatari kwa Taifa letu, hakuna pa kukimbilia, hakuna pa kusemea, tunaburuzwa kama mapunda, eee Mola iko siku utatukomboa.

Mungu ibariki Tanzania

Mungu kinusuru chama cha chadema.
 

Na ndiyo Maaana tumeanza kufikiri na hata kutafakari ni nini tufanye ili tukiboreshe chama hiki cha CHADEMA, chama mbadala, kimbilio la Watanzania bara, sauti ya wanyonge, wajane kwa mayatima hapa ndiyo mahali pao.

Kauli yako ina uwalakini, umeanza vizuri kwa kutaka kuijenga nchi katika misingi ya haki na mwishoe ukabagua upande mmoja unaounda nchi ya Tanzania. Itakuwa jambo la mbolea ukinifahamisha nini nafasi ya Tanzania Visiwani katika Chadema.
 
Kauli yako ina uwalakini, umeanza vizuri kwa kutaka kuijenga nchi katika misingi ya haki na mwishoe ukabagua upande mmoja unaounda nchi ya Tanzania. Itakuwa jambo la mbolea ukinifahamisha nini nafasi ya Tanzania Visiwani katika Chadema.

Kibunango,

Itahitaji Muda kidogo kukuelimisha haya yaliyo ndani ya fuadi yangu, wewe ni mtu makini sana na ninaendelea kuheshimu mchango wako kwa leo, ila naomba nikujuze haya,

Visiwani kwa sasa uwelewa wa kidemokrasia umekuwa, hatushangai kuona siku moja kule visiwani CUF wakiwa watawala, nimeongea hivyo kwa sababu huku bara ndiyo bado elimu ya kisiasi iko chini na si vinginevyo.

Unaweza kudhani nimewagawa kwa nisingi ya ramani ya kijiografia la hasha, mimi najikita kulitetea Taifa hili letu, bara na hata visiwani, jambo la kujadili sana bara ni hoja ya msingi na hii ni kwa sababu tu mageuzi yawafikie watu wengi, na kwa upande wa visiwani kazi hiyo wana CUF wameimaliza na si vinginevyo, pale CCM wanang'ang'aniza tu

Mungu Ibariki Tanzania
 
jusema kukweli mimi binafsi naunga mkono hoja hii ya Mhe mbowe kujiuzulu kwani itakuwa kwa maslahi ya wana CHADEMA wote na kwa ustawi wa "USHINDANI".
CCM wanataka kuangamiza kabisa CHADEMA kwa kumchafua Mbowe, sasa ili kuepuka haya yote ya watu kutokuwa na imani na CHADEMA ni vizuri jamaa akajiweka pembeni.
 


Joel,

Ni kweli kuwa mawazo yetu si batili na wala hatujawakosea wanachadema, tunajua kuwa kwa sasa chama hiki kina sura ya kitaifa, ni chama kinachoungwa mkono na kada mbalimbali, wasomi kwa wasiowasoni.

Tunaomba kusema itakuwa si busara kama haya tunayoyasema hapa, Mnyika na Zito msiyachukue,,Huu ni mtaji tu wa matumaini ya chama chetu, tunajua sisi kama wanachama hatuna fursa ya kuingia katika vikao vya juu ili kushauri na kufanya maamuzi, fanyeni hivyo tunavyoshauri na si vinginevyo.

Tambueni kuwa chama hiki ndiyo kimbilio la watanzania kwa sasa, msimuogope Mtu, tambueni Zitto,Dr. Slaa, Taifa hili liko mikononi mwenu kwa sasa(wapinzani), msijisahau kabisa tambueni kuwa yale ambayo mmekuwa mkiyatetea mmeweza kuungwa mkono na hata WABUNGE WA CCM, hayo yamefanyika tu ni kwa sababu mnakubalika.

Msikubali kabisa mtu(binafsi) kuharibu kazi njema mliyoifanya pale bungeni, msikubali kupewa shutuma zisizokuwa zenu, sisi watanzania tuko nyuma yenu.Mmekuwa kivutio pale bungeni, Watanzania walikuwa hawana utamaduni wa kuangalia bunge, kwa sasa watanzania wote wanaangalia bunge.

Mjadala huu utaendelea kua hapa mpaka 2010, ni mjadala wa kitaifa na si kwa ajili ya maslahi yangu bali Taifa zima.

Mungu ibariki Tanzania

Mungu kinusuru chama cha CHADEMA na hawa mafisadi
 

Ukirudi Hapa Naomba Uwe Na Hoja Badala Ya Hyo Yanayosukuma Damu Yako
 
Joel,
Kama Mbowe anapaswa kujiuzuru kwa kuwa amechafuliwa na CCM, huyo atakayechukua nafasi yake atafanyaje yeye asichafuliwe? Kama kweli una mapenzi mema kwa CHADEMA kwa nini usituelimishe wengi tusiojua kinachoendelea kuwa haya yote ni mbinu hizo unazosema kuwa in za CCM kuimaliza CHADEMA?
 
Mimi nasita mtu anapojitambulisha kama mkereketwa wa CHADEMA katika kusisitiza jambo. Kwani katika misafara ya Mamba pia kenge hawakosekani. Sababu nyingi zisizokuwa na ncha juu ya kujiuzulu kwa Mbowe zimetolewa kubwa ikiwa ni zinazodaiwa kuwa mbinu chafu za mpinzani wake mkuu CCM. Je huyo maetaka achukue madaraka atakwepa je hili? Mimi nadhani kama tatizo mmelifahamu ndio mahali pa kuendelekeza nguvu na kumwezesha anaeongoza kuhakikisha mbinu hizi chafu zinashindwa. Msijekujikuta mnatumiwa na mafisadi kujiangamiza wenyewe.

Mimi nadhani CHADEMA watulie na katika vikao vyao watafakari na kujipanga katika hali inayokikabili chama. Ila watanzania wasiwe wepesi wa kupoteza mashiko kwenye mambo yenye Msingi. Sasa hatujadili tena ufisadi na rasilimali zilizopotea za nchi, hakuna tena muafaka kati ya ccm na cuf ila zanzibar ni nchi au la! na mengine mengi yanayofana na haya. Sesemi tusijadili, ila kweli ndiyo ya msingi au ni upepo unaotengenezwa na watu wachache wenye masilahi binafsi ya kuendelea kulididimiza Taifa? Nadhani sisi Watanzania tunahitaji KUTAFAKARI vingienvyo daima tutaendelea kubakia hapa hapa. Tusiendelee kukubali kuwa kichwa cha mwendawazimu
 



Ile slogan yako ya king'ang'anizi umeibadili Mkuu?

Kesho tutegemee ipi?

Haikuwa slogan.

Mimi ni mkulima Mkuu, napenda kujifunza mazuri toka kwa wenzangu

Shamba lako litarajie mavuno mema maana mwaka huu mvua ni nzuri.

Halisi,hakika kweli nimeng'amua kile unachokijua, kisha nimelewa uelewa wako Mkuu, ila kuwa kigeugeu si jambo jema hata kidogo, umesema wewe umewahi kuwatetea CCM, CUF na haukuishia hapo mkuu, umesema wewe ni mseto, hakika umenifadhaisha sana.

Nadhani hujanielewa. Naomba nikufahamishe kwamba si kwamba nimekuwa nikitetea CCM, CUF. Ni kwamba niko karibu na wote hao, lakini kwa sababu za kikazi na si kiitikadi. Wote wananifahamu na kuniheshimu si kwa sababu nawatetea bali nakabiliana nao kwa HAKI na kuwatetea kwa HAKI na kuwahukumu kwa HAKI. Ninawapinga wanapokosea na kuwatetea inapobidi kwa MASLAHI YA TAIFA NA WATU WAKE. Situmiki, sijawahi kutumika na sitarajii kutumika kama baadhi ya wachangiaji humu ambao HAWAYUMBI.

Nataka ufanane na mimi, pigania kile unachokiamini kama kina tija kwa taifa kwa siku za usoni bila kujali upenzi wako dhidi ya muhusika.

Ungejua ukweli ungeona aibu hata kwanini unasema maneno hayo. Iko siku yatatimia kwa MASLAHI YA TAIFA.

Najua pole pole utarudi na kusimama pamoja na mimi na kuona kile ninachokiamini kina tija kwetu sote, na wewe utaniunga mkono siko moja.

Tija kwenu na nani? Jisemee kwa kuwa naamini wanaopaswa kusema hayo ni kina Mnyika na wenzake ambao nao wamo humu na si wewe.

Tazama ulivyo, unashindwa kujua 2+2= 4? Huuu nao ni mlinganyo?

Bahati mbaya SIKUSOMA kama wewe, natumia akili niliyopata katika maziwa ya mama yangu kwa hiyo sitegemei fikra za wanafalsafa wa 'kiyunani' au wengineo. Natumia falsafa ya mama yangu aliyenizaa.
Utazani umelishwa yamini, oohhhh...., ukiruka hapa tu oooohh utaota matiti, basi hapo utatetea ili mradi tu usiote matiti.

Tuko pamoja Mkuu

Aliyelishwa yamini anajulikana, anayesema Mbowe ajiuzulu kwa kuwa anaandamwa na CCM na wapinzani wenzake. He!!!!... Kesho ukija na hoja kwamba, Mbowe kapatikana na hatia kwa ushahidi A, B, C na hivyo amepoteza hadhi ya kuwa kiongozi, nitaungana na wewe, kama ambavyo nataka ukubali kwamba kwa hoja hizo hazifanyi iwe sababu ya kujizulu kwa Mwenyekiti wa chama cha upinzani chenye nguvu kama Chadema. Ungekuja na hoja kwamba, Mbowe atafute jimbo agombee na awe mbunge na aingize wabunge wengi ili awe kiongozi wa upinzani bungeni, na pengine hata apatikane mgombea ambaye ataing'oa CCM madarakani na wawe na serikali ya mseto wa vyama vilivyokuwa vya upinzani... ningekuelewa. Au ungekuja na hoja kwamba sasa Mbowe asigombee urais na aanze kuimarisha chama chake hadi vijijini kiweze kujiandaa kuchukua nchi 2015, ningeanza kukuelewa kidogo. Na kadhalika......
 

Nono,

Nimefurahishwa na mchango wako kwa siku ya leo, hakika nimebaini hiasia zako dhidi ya mabwenyenye wa Taifa hili, tunajua, tunaelewa, hawa mafisadi wana njia nyingi za kuweza kutokomeza hii demokrasia yetu hii changa inayoanza kuchipua.

Jambo la kuzingatia hapa ni kutumia nguvu ya umma kuupinga huu ubaradhuri tunaofanyiwa na hawa Mafisadi, na ndiyo maana katika hoja yangu nikashauri tuwe na mikakati ya kujiandaa ili kupambana na hawa jamaa,pia usisahau kuwa vyombo vyote vya dola wanavimiliki, tunaendelea kuumiza vichwa vyetunini kifanyike ili tujikomboe toka mikononi mwao.

Ipo njia, nayo ni kujipanga ili kuwapata wabunge wengi wa upinzani 2010, ili tuweze kuwa na serikali ya mseto hii itatoa mwanya wa kuishauri serikali na kuimarisha serikali yetu. Njia mojawapo ni kuboresha upinzani sambamba na kuwapata viongozi watakaouzika 2010.

Tumekuwa na matatizo ya kutojiandaa kwenye uchaguzi, tunajikuta tu wakati wa uchaguzi umefika na hapo ndipo sisi wanamageuzi huangukia pua, tuseme kuwa bila mikakati hakuna MAGEUZI, Tutaendelea kuukimbiza mwenge kwa muda mwingi
 
chadema ni chama kama vilivyo vyama vya watu wanaotoka sehemu moja vya vyuo vikuu kwa mfano Rubya alumni(kwa watu waliosoma hapo)...mara university students association....na kagara university students association......mwenye macho aambiwi tazama
 
chadema ni chama kama vilivyo vyama vya watu wanaotoka sehemu moja vya vyuo vikuu kwa mfano Rubya alumni(kwa watu waliosoma hapo)...mara university students association....na kagara university students association......mwenye macho aambiwi tazama

Mkuu jina lako gumu sana,

Ila naomba uainishe vizuri kisha utuweke wazi Mkuu, unataka kutuambia nini Mkuu, Sijakusoma unamaanisha Ryuba Kafanya nini?
 

Halisi,

Ninaendelea kukushukuru sana kwa kuwa na hoja mathubuti za kuweza kuipotosha jamii yetu, ni dhahili kabisa wewe mtazamo wako umebainika kwangu, nimegundua wewe ni mtu wa aina gani, nimezisoma fikra zako na upenzi wako kwa mtu mmoja mmoja.

Halisi kila siku katika mchango wangu hujitahidi kukujibu kwa busara huku hekima ikichukua mkondo wake, niliendelea kukusoma ni mtu wa aina gani hua napata kubadilishana naye mawazo, ndipo nikagundua kuwa ...

(a) Halisi ni mtu Muoga na mwenye fikra tata, Mgando zisizokubali Mabadiliko, fikra zake bado hazijaweza kutofautisha TUI NA MAZIWA.

(b) Halisi ni mtu mwenye tabia ya kujipendekeza kwa wale wenye nacho hata kama hao wenye nacho hawatakuwa na sifa za msingi kwa kipindi hicho.

Halisi naomba ufafahamu kuwa Taifa letu lilipofikia halina mtetezi kwa sasa, Tumebaki mayatima tusiyokuwa na BABA NA MAMA, tumetelekezwa, na ndito maana hatushangai Viongozi wetu kujinyakulia Mali zetu bila kuhojiwa.

Halisi Tazama,inapofikia watu(binafsi)kuandamana 23/8/2008 kama wataruhusiwa, kutetea na kuhoji mali zao bila hata kua na kiongozi wa kisiasa hii ni hatari sana.

Halisi hiki si kipindi cha kumtetea Mtu kwa sababu ya maslahi yako binafsi, tanguliza uzalendo mbele ,Taifa letu litapata shida kubwa kwa kuwa na watu kama wewe, ving'ang'anizi msiyopenda kuona mabadiliko.

M/kiti wetu yuko kimya tunajua bado anatafakari na mwisho atakuja na hoja yenye maslahi ya Taifa hili ambalo kwa sasa ni tete.

Mungu ibariki Tanzania
 

Nono,

Ninazidi kusema, hebu sisi tuna vichwa gani hivi tusiosikia hata tukiguswa na Muumba wetu?

Ni lini tutatumia akili kidogo ili kukabiliana na changa moto zilizo mbele yetu?

Hebu kweli sisi watanzania ni Mazezeta kiasi hiki jamani?

Tusipoangalia tutaendelea kuwasindikiza CCM mpaka tutakapozikwa hiki kizazi, haiwezekani tukose mikakati na maandalizi ya 2010, tunazidi kupiga soga na wakati unazidi kusonga

Maswari ya kujiuliza :

(a) Ni kweli tumejiandaa 2010 kupambana na hawa Mafisadi CCM?

(B) Watanzania watakuwa tayari kuumpa M/kiti wetu kura ili aiongoze inchi hii? na kwa kuwa hawa mafisadi wameanza kampeni za kumchafua, ni kwa nini tusiwe na mkakati ndani ya chama kwa maslahi ya Taifa?

Ninazidi kusema, upenzi na ushabiki usiozingatia Maslahi ya Taifa ni jambo la kipuuzi sana, tunaomba watanzania wenzetu tuwe na mikakati ya 2010, hii ni pamoja na kuwapata wabunge wa upinzani wa kutosha.

Naomba mtambue hivi, CCM mikakati yao ni kuona wanayarudisha Majimbo yote ya Upinzani huku Tanzania bara, na hiyo ndiyo itapelekea kuua upinzani, tutie akili jamani.
 

Halisi

Umeziona zile fikra zako? umeona mtizamo wako, nilikwambia kuwa hawa wapinzani wenza wamemsaliti Mbowe, wamemtwika zigo lisilo lake, wewe halisi ukasema ni vema tutapoteza jimbo la Tarime la kulinda maslahi ya chama hiki.

Lakini naomba utambue kuwa kila tunapozidi kuwapata wabunge wa upinzani bungeni ndipo hapo demokrasia ya kweli inapozidi kujikita hapa tanzania, laiti ungelijua hila na malengo ya CCM hakika ungetingisha kichwa, wao kwa mioyo yao ccm, wanataka kukomboa majimbo yote yaliyoodhiwa na wapinzani.
 
Nimerudi tena, baada ya kupotea siku 28, nadhani nimetimiza wajibu wangu kama mtanzania yeyote, nimerudi na ule ule mtizamo wa kuinua fikra hai zisizo na uwoga hata kidogo, nimerudi huku nikiwa nimejeruhiwa, haijalishi hata kama siku za usoni nitaendelea kuteshwa na kutisha kwa mitutu na hata magari ya upupu,

Mara nyingi nimekuwa nikiwashauri watanzania tuungane, tuonyeshe njia, na hata sasa ninafanya hivyo hivyo,

Hebu inakuweje watanzania tusiwe na mitazamo ya siku za usoni? inakuweje kama hatutataka kujua hatima za watoto wetu? ninyi wtanzania ni nani kawaroga?

Naomba sasa tuwe na mikakati ya kweli ili 2010 tuweze kuwa na upinzani wa kweli, mara kwa mara nimesema vyama vya upinzani vikiungana kuna kitu tunaweza kufanya, lakini ni pamoja na kuweka viongozi watakaouzika 2010
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…