IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Ndugu wana JF mjadala ni mzuri na nimecopy kwenye hardcopy nitawanye huku kwenye vijiwe vya kyela.
Asanteni sana
Nsaji Mpoki,
Usiishie kucopy my young brother, tukiwa wa kucopy na kupest basi hapa tutalishana pumba hadi tuvembewe, Tazama, kama utaona maada hii imekuingia ikakukomboa kifkra, hakika utakuwa umeboreka zaidi kuliko kushabikia bila kuzingatia yale tunayoyajadili hapa,
Nchi hii ni yetu sote, tuijenge, tuipiganie, haijalishi hata kama tutafanywa KAFARA kwa leo kizazi chetu kijacho kitashangilia, Nsaji wewe ni shaidi wa maisha ya kizazi hiki ambacho sasa wachache tu ndiyo wamiliki wa njia za uchumi wa Taifa hili, hii haiwezekani kabisa.
Na ndiyo Maaana tumeanza kufikiri na hata kutafakari ni nini tufanye ili tukiboreshe chama hiki cha CHADEMA, chama mbadala, kimbilio la Watanzania bara, na Visiwani, sauti ya wanyonge, wajane kwa mayatima hapa ndiyo mahali pao.
Tunataka Mtu mwenye uchungu na Taifa hili, Mtu mwenye mwelekeo chanya na mkombozi wa Taifa hili, huku akijitahidi kujiepusha na maslahi Binafsi(biashara) zaidi akitafakari matatizo ya watu wake hawa maskini.
Tunajua Taifa letu limeuzwa, wakoloni wamerudi kwa mlango wa nyuma, sasa wanapora na wala hakuna makubaliano hata kidogo, tukibisha tu basi hapo patasitishwa misaada na mengineyo.
Mnashuhudia taifa letu na watu wake wakiwa katika msuguano wa kimaslahi, Wafanyakazi, Walimu, Madakitari na hata wanafunzi, hii ni hatari kwa Taifa letu, hakuna pa kukimbilia, hakuna pa kusemea, tunaburuzwa kama mapunda, eee Mola iko siku utatukomboa.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu kinusuru chama cha chadema.