Jina lako linathibitisha kuwa ni mchagga, kauli zako ndio kabisa zinaonesha kuwa ni mangi kuna sehemu umewapakazia Ngaiza na Baregu na ukawaacha Mtei na Ndesamburo kwa vile ni wachagga ili kutudanganya kuwa hao ndio walimfukuza Chacha Wangwe.
MK jina lako linabeba kauli mbiu ya watu wa kilimanjaro 'Aisee babaangu si kubali Mpaka kieleweke baabangu'
Nimepata nafasi ya kuzungumza na Tundu Lissu kuhusu suala hili la Chacha. Mahojiano yatarushwa baadaye kesho.
Tunakushukuru ila naomba uhoji na upande wa Wangwe, kwani Tundu Lissu yuko kwa Mbowe ili haki ipatikane.
ccm kweli chama kubwa, yaani watu hata wakisoma maandishi tu wanajua mtu katoka wapi.
Kidumu chama cha mapinduzi.
Mimi nadhani Lissu yuko karibu zaidi na Wangwe. Si ndiye Mwanasheria wake kwa muda mrefu tu.... kuna mtu anayemjua zaidi Wangwe kuliko Lissu ndani ya Chadema?
ni Mkurugenzi Wa Sheria Wa Chadema Sijawahi Kusoma Wala Kusikia Kama Mwanasheria Wa Muda Mrefu Wa Wangwe,kitila Mkumbo Ndiye Mtu Wa Karibu Wa Tundu Lissu.
Ingawa ni makosa ya hii forum kutaja majina ya members hapa, lakini sidhani kama huyu MK ni Mbowe. Mbowe alikuwa anakuja hapa lakini akabanwa na wana JF akakimbia.
Una ushahidi na maneno yako? kama wanachama na wabunge wa Chadema wapo hapa kwanini Mwenyekiti asiwepo?
Lissu Ni Mwanasheria Wa Wangwe Tangu 2004 Kabla Hata Hajawa Mkurugenzi Wa Sheria Chadema Na Mpaka Sasa Ndiye Anasimamia Kesi Ya Wangwe Mahakama Ya Rufaa ,kwani Baada Ya Kushinda Kesi Ya Uchaguzi Mahakama Kuu Ccm Wamekata Rufaaa.
ccm kweli chama kubwa, yaani watu hata wakisoma maandishi tu wanajua mtu katoka wapi.
Kidumu chama cha mapinduzi.
Hatushindanishi vyama tunajaribu kuweka mambo sawa iwe CUF,TLP,Chadema au CCM.
Kweli, viongozi wa chadema kina zitto na mnyika bado wako hapa JF, Mbowe naye alikuwa hapa zamani akitumia jina lake ila akakimbia. Kama unalijua jina lake jipya basi wewe liseme tu ila ukumbuke pia kuwa ni makosa kutaja majina halisi ya wana JF, ukifungiwa na wenyewe mi simo.
Unanitisha kuwa nitafungiwa,wakati huo huo unanipa ruhusa ya kumtaja usinipe uhuru wa masharti au na Wangwe alipewa uhuru wa kueleza ukweli halafu ikaja adhabu ya kufukuzwa? jana alitishwa Mtanzania kuwa kwanini anaingilia mambo yasiyomuhusu, jamani tusitishane nchi yetu sote.
usione aibu kuwa mwana ccm , endeleza mapambano maana kazi yako ni nzuri kabisa hapa JF.
kidumu chama cha mapinduzi
kuwa mwanaccm ni aibu? na kwanini nifiche kwa kumuogopa nani, wewe,JF au Mbowe,Mtei au Chacha Wange?
Michango hii tunayoandika inaweza kutumika vizuri huko mbele kukiimarisha chama cha Chadema au Ccm na vinginevyo,tungekuwa tunaitakia mabaya Chadema tungenyamaza tu lakini tunatoa ushauri na nini kifanyike,tunapoteza muda wetu kuipitia katiba ya Chadema kwa maslahi gani?
Leo namuandika Mnyika au Tundu Lissu tunamfanya ajulikane na jamii na kumpa jina kwa wananchi, ilitakiwa mtushukuru sana badala ya kutubeza kwa kauli zisizo na busara.
Nani alikuwa anajua kuwa Wangwe ndio mbunge wa upinzani aliyeingia bungeni kwa asilimia zaidi ya 65 ni mjadala huu umetufikisha huko.
Nimependa hayo maandishi kwenye blue, nccr na tlp vimekufa, chadema nayo itakufa karibuni, baadaye mambo yote yanahamia cuf zanzibar maana bara cuf imekufa. Baada ya muda si mrefu kutabaki vyama vya ajabu ajabu dhaifu kama chaustawi wa jamii... kwi kwi kwi
Kidumu chama cha mapinduzi na udumu usalama wa taifa kwa kazi nzuri.
Basi Mbowe ndio usalama wa Taifa.
nimekukumbusha tu sheria za JF kuwa ukitaja jina halisi la mwanachama wa JF ambaye hajajitambulisha mwenyewe utafungiwa. Soma sheria mwenzangu sio vitisho bali ni sheria za JF. Hata nikikupa ruhusa bado haitakusaidia pale ambapo sheria za JF zikichukua mkondo wake. JF inahitaji watetezi wa ccm wengi kama wewe na usitafute sababu ya kufungiwa.
Otherwise, endeleza kazi ya kutetea chama kubwa la kijani na wala usione haya. Kidumu cha mapinduzi.