Mgagagigikoko
JF-Expert Member
- Jul 1, 2007
- 474
- 0
KUHUSU UKABILA UKWELI HUU HAPA.
Licha ya ushahidi wa wazi kwamba viongozi wa ngazi za juu akiwemo yeye mwenyewe wametoka sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Chacha Wangwe ameendelea kutuhumu kwamba kuna upendeleo kwa Wachagga na/au watu wa kaskazini ya Tanzania. Kivuli pekee cha tuhuma hizi potofu ni madai ya uwongo kwamba Wabunge watano kati ya sita wa Viti Maalumu wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ni Wachagga. Kama wananchi wanavyofahamu, Wabunge Wachagga ni watatu tu na wengine ni Mzanzibari mmoja, Mpare mmoja na Muha mmoja. Aidha Mh. Chacha Wangwe anafahamu kwamba kati ya wajumbe thelathini na sita wa Kamati Kuu ya Chama kuna Wachagga watano tu sawa na wajumbe wa Mkoa wa Kigoma! Aidha Mh. Wangwe anafahamu fika kwamba kati ya wakurugenzi na watendaji wa ngazi za juu wa Makao Makuu wapatao zaidi ya ishirini, Wachagga wako watatu tu. Kwa msingi huo, lengo la kashfa za ukabila ndani ya chama zina lengo moja tu: kuwapaka matope viongozi na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa nia ya kuwadhoofisha na kuwapunguzia nguvu ya kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.
Mpaka Kielewe.
Mbona maneno haya ni ya Mbowe kwenye statement yake iko Klh News yaani ume copy na kupaste. lete maneno yako.