CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Kuhusu Ukabila Wa Chadema

Wao Kama Chadema Watafanyeje Ili Wasionekane Wakabila, Endapo Mikoa Mingine Imekumbatia Ccm Na Watu Hawataki Kujitoa Huko Kuja Chadema? Nani Asiyejua Ccm Ni Chama Cha Kikabila Kuliko Vyama Vyote? Nani Asiyejua Kuwa Mafisadi Wananeemeka Kwa Kulindwa Na Kukabila? Hakuna Fisadi Hata Mmoja Alithubutu Kuhutubia Dsm Baada Ya Kutimuliwa Uwaziri, Wote Walikimbilia Majimboni Mwao Wakihutubia Kwa Kilugha, Mpaka Askofu Mmoja Akasikika Akisema Wamamsai Hawaibi Pesa Wanaiba Ngombe-amkeni
 
KUHUSU UKABILA UKWELI HUU HAPA.

Licha ya ushahidi wa wazi kwamba viongozi wa ngazi za juu akiwemo yeye mwenyewe wametoka sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Chacha Wangwe ameendelea kutuhumu kwamba kuna upendeleo kwa Wachagga na/au watu wa kaskazini ya Tanzania. Kivuli pekee cha tuhuma hizi potofu ni madai ya uwongo kwamba Wabunge watano kati ya sita wa Viti Maalumu wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ni Wachagga. Kama wananchi wanavyofahamu, Wabunge Wachagga ni watatu tu na wengine ni Mzanzibari mmoja, Mpare mmoja na Muha mmoja. Aidha Mh. Chacha Wangwe anafahamu kwamba kati ya wajumbe thelathini na sita wa Kamati Kuu ya Chama kuna Wachagga watano tu sawa na wajumbe wa Mkoa wa Kigoma! Aidha Mh. Wangwe anafahamu fika kwamba kati ya wakurugenzi na watendaji wa ngazi za juu wa Makao Makuu wapatao zaidi ya ishirini, Wachagga wako watatu tu. Kwa msingi huo, lengo la kashfa za ukabila ndani ya chama zina lengo moja tu: kuwapaka matope viongozi na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa nia ya kuwadhoofisha na kuwapunguzia nguvu ya kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.
 
Wangwe alikuwa mzigo mkubwa sana kwa chama, hata huko Jimboni kwake hajui kutofautisha kazi ya mbunge na kazi za watendaji wa serikali anaweza kubishana nao hata mahala ambapo hapaitajiki ubishi, Hilo linaeleweka.

Wangwe mwenyewe hajasema kama kweli wakati wa kumuondoa hawakutumia katiba, ni kwamba katiba imefuatwa haswa. Ninachoona hapa ni kama msemaji mmoja alivyosema tumezoeshwa na CCM kuwa ukikosea sijui kuna urasimu gani unatakiwa kufuatwa, hili chama kisiparaganyike. Chama siyo Mtu chama ni wanachama. Kwa CCM Tumeona kulindana hata mpaka tumefikia kukiita majina kama ishirini hivi ya kejeli lakini wameamua kunyamaza na kubaki na fedhea (Hii ni aibu!).

Nafikiri Chadema wameonyesha ukomavu katika masrahi ya chama hawamwangalii mtu usoni potelea mbali hata kama watakosa kiti cha ubunge lakini maslahi ya chama, katiba ya chama inatakiwa kulindwa. Na kama wataendelea hivi hata mwenyekiti wao atafanya kazi akijua kuwa kuna siku nayeye yanaweza kumkuta.
 
Kick Chacha Wangwe out of that office. He is just a load of crap to serve in that capacity.

Hata akina Chitalilo walichaguliwa kuwa wawakilishi wa wananchi....lakini maajabu ya Musa wanajiwakilisha wenyewe na mafisadi.
 
Nawaangalia tu.. wenye kujua hawasemi, na wasiojua wanasema sana kana kwamba wanajua.

Kama wanajua hawasemi na tuko kwenye eneo la kupata msemaji, basi hawajui, kwani wanachokijua muda wa kukisema ni sasa.

Umetumia kigezo gani kusema kuwa hawajui? kuna mtihani mlifanya au kwa vile wewe una posts elfu kumi? siamini kuwa na posts nyingi ndio unajua,Mnyika ana posts chache au Zitto lakini huwezi kusema hajui kuliko wewe.
 
KUHUSU UKABILA UKWELI HUU HAPA.

Licha ya ushahidi wa wazi kwamba viongozi wa ngazi za juu akiwemo yeye mwenyewe wametoka sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Chacha Wangwe ameendelea kutuhumu kwamba kuna upendeleo kwa Wachagga na/au watu wa kaskazini ya Tanzania. Kivuli pekee cha tuhuma hizi potofu ni madai ya uwongo kwamba Wabunge watano kati ya sita wa Viti Maalumu wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ni Wachagga. Kama wananchi wanavyofahamu, Wabunge Wachagga ni watatu tu na wengine ni Mzanzibari mmoja, Mpare mmoja na Muha mmoja. Aidha Mh. Chacha Wangwe anafahamu kwamba kati ya wajumbe thelathini na sita wa Kamati Kuu ya Chama kuna Wachagga watano tu sawa na wajumbe wa Mkoa wa Kigoma! Aidha Mh. Wangwe anafahamu fika kwamba kati ya wakurugenzi na watendaji wa ngazi za juu wa Makao Makuu wapatao zaidi ya ishirini, Wachagga wako watatu tu. Kwa msingi huo, lengo la kashfa za ukabila ndani ya chama zina lengo moja tu: kuwapaka matope viongozi na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa nia ya kuwadhoofisha na kuwapunguzia nguvu ya kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.

Mpaka kieleweke,
usitake kutuhadaa hasa suala linalohusu Ukabila CHADEMA,linajulikana wazi..kama wewe siyo ndugu wa Mtei,Mbowe hauwezi kupewa madaraka..Lucy Owenya??

Wewe Mwenyewe unatoka huko huko,sasa unategemea nini?kama siyo kumpiga Mhe. Chahca Wangwe?ndiyo maana chache Wangwe anataka kiwepo Chama Chenye Sura ya Utaifa na wala Siyo sura ya Kasikazini.

Ni siku nyingi niliamua kukaa kimya na sasa naomba nikwambie kwanini Mbowe na Chama chenu kilikuwa maarufu sana kwa kampeni kubwa na zenye watu wengi na mkashindwa sana katika Uchaguzi wa Urais na Ubunge

1.Sura ya Chadema imekaa haswa kikabila,watu wa kaskazini wamejazwa kila nafasi ya uongozi wa CHADEMA.Na hii ilichangia kwa kiasi kikubwa kwa Wagombea wenu katika sehemu za kanda ya Ziwa na kusini Kushindwa,watu wamechoshwa na Ukabila na wanataka Vyama ambavyo vina sura ya utaifa bila udini.CCM inaendelea kushinda siyo kwamba watanzania wanakipenda sana ila ni sababu ina Sura ya Kitaifa,kamwe hauwezi kusikia CCM imejaa watu wa kaskazini au wapi na hii imechangiwa na Mfumo mzuri wa kiutawala katika Chama Cha Mapinduzi achilia mbali amaamuzi wanayoyafanya

2.Siku zote Kupanga ni Kuchagua,na kama alivyosema Mzee Mkapa Mipango Mizuri MWanzoni huleta Majibu mazuri kimkakati mbeleni,CHADEMA ni chama kizuri ila hakina watu wanoweza kupanga mambo mazuri kwa ajili ya Baadaye,inawezekana wakawepo ila wanamezwa na wachache wasiyojua nini cha kufanya.Kimsingi nahisi Mwenyekiti wenu anaogopa Kivuli Chacke na has anamhofia DR. Slaa.anatumia Mbinu ya 'Divide and Rule' ili kuwagawa wana CHADEMA ili afanikishe adhima yake.

Baada ya kusema hayo ningependa kuwashauri CHADEMA kama ifuatavyo kama kweli mna nia njema ya kutekeleza SERA zenu

1.Tengenezeni CHAMA chenye Sura ya kitaifa,kuliko ilivyo hivi sasa.kulikuwa na shida gani kugawa Viti vya nafasi za kuteuliwa Kikanda?Nani anawakilisha CHADEMA upande wa Kusini??Nani Upande wa Kanda ya Kati na Magharibi achilia Mbali zitto ambaye ni Mbunge wa kuchaguliwa.Kanda ya Ziwa Je?

2.Tafuteni wasomi waongoze Chama chenu,At least mtu mwenye Elimu na Uzoefu katika Uongozi anaweza akwa msaada mkubwa sana katika Chama,Chukulia Watu kama kina Mzee Mtei.waliweza kukiongoza Cchama sababu walishawahi kuwa Viongozi katika nafasi mbali mbali ukiachilia mbali Elimu waliyo nayo

Kwa hili namuunga Mkono CHACHA WANGWE
 
Wangwe alikuwa mzigo mkubwa sana kwa chama, hata huko Jimboni kwake hajui kutofautisha kazi ya mbunge na kazi za watendaji wa serikali anaweza kubishana nao hata mahala ambapo hapaitajiki ubishi, Hilo linaeleweka.

Wangwe mwenyewe hajasema kama kweli wakati wa kumuondoa hawakutumia katiba, ni kwamba katiba imefuatwa haswa. Ninachoona hapa ni kama msemaji mmoja alivyosema tumezoeshwa na CCM kuwa ukikosea sijui kuna urasimu gani unatakiwa kufuatwa, hili chama kisiparaganyike. Chama siyo Mtu chama ni wanachama. Kwa CCM Tumeona kulindana hata mpaka tumefikia kukiita majina kama ishirini hivi ya kejeli lakini wameamua kunyamaza na kubaki na fedhea (Hii ni aibu!).

Nafikiri Chadema wameonyesha ukomavu katika masrahi ya chama hawamwangalii mtu usoni potelea mbali hata kama watakosa kiti cha ubunge lakini maslahi ya chama, katiba ya chama inatakiwa kulindwa. Na kama wataendelea hivi hata mwenyekiti wao atafanya kazi akijua kuwa kuna siku nayeye yanaweza kumkuta.

Naona katika mjadala huu hakuna anaysema katiba haikufuatwa, kwa Afrika hata kule Zimbabwe Mugabe naye kawekwa na katiba hiyo hiyo. UDSM wanavyotimua wanafunzi wanatumia sheria hizo hizo zilikubaliwa. Hata Kibaki alivyoapishwa haraka haraka alitumia katiba ya Kenya.

Huu mjadala ni mkubwa kuliko katiba kufuatwa. Je katiba ya namna hiyo ina maana yoyote katika chama kinachotakiwa kuongoza katika mabadiliko na demokrasia?

Kama Wangwe ni mzigo basi kikao kilichomchagua ndio mahali pazuri pa kuelezea huo mzigo wake. Kama wangeridhika basi wangeweza kumwondoa.

Kama ugomvi ni kati ya Mwenyekiti na makamu wake, ni kukomaa kisiasa kwa wahusika kujiuzulu na kurudi kwa watu waliowachagua kuomba kura.

Kama mnachotaka kuongelea ni kufuata katiba basi endeleeni, hata Saddam alikuwa anafuata katiba au CCM tunaowasema kila siku hapa nao wanafuata katiba yao.
 
Kama wanajua hawasemi na tuko kwenye eneo la kupata msemaji, basi hawajui, kwani wanachokijua muda wa kukisema ni sasa.

Umetumia kigezo gani kusema kuwa hawajui? kuna mtihani mlifanya au kwa vile wewe una posts elfu kumi? siamini kuwa na posts nyingi ndio unajua,Mnyika ana posts chache au Zitto lakini huwezi kusema hajui kuliko wewe.

nimesema najua?
 
mkimaliza wangwe matakuja kusema hata Slaa ni mzigo, nyie mtoto akinyea kiganja mwakikata!wenzenu wanaosha na maji ya baridi, ya moto, sabuni na mwisho wanaweka jiki.

Sema wewe Mama yetu, kama alikuwa mzigo siku zote walikuwa wapi kutuambia hapa JF? unajua Wangwe alisema kuwa pesa za makao makuu zinatumika vibaya na kuna watu wananufaika nazo kama kina Mnyika, who knows labda na wangine wanalipiwa bills za internet kuja JF kwa pesa za makao makuu. watu wa naona hiyo lazima wafurahie kuondoka kwa Wangwe.
 
Gembe ,kusema kuwa mimi ni mchagga its very wrong.

Usifanye ,usiwaze na wala usiandike kitu kwa hisia ,kuwa eti nami ni mchagga huu ni upotoswaji wa wazi kwani kwanza wewe hata hunijui wala sura yangu huijui.

Acha kupotosha .
 
Hawa wapinzani hawatuwezi, sasa ni fimbo tu, tutawapinga chadema fimbo hapa JF, na kisha tutawachanganya kwenye uongozi na mwisho watu watajua kuwa ccm pekee ndio chama kubwa.

.... ha ha ha haha .. hawa hawaijui ccm....

Niliwaonya hapa hawakusikia.

Kama huijui kazi ya usalama wa taifa sasa umeijua, tumeshawatoa kwenye debate ya EPA, meremeta, na story zingine zote za uzushi na tumewaweka hapa ambako mtagongana hadi 2010 na ccm itashinda kwa kishindo.
 
wangapi humu wamesoma signature yangu >? well, hail..........nitarudi !

Kweli kada... wewe wavuruge tu hao wapinzani, wao wanajifanya kuongelea mambo ya richmonduli tu kumbe hata wao tunaweza kuwapata na kuwachanganya tu.

Huyu Wangwe ni mwiba na atawachanganya hadi wakome. Nakuamini kada kwa kukomesha wapinzani hapa JF. Fanya kazi yako.
 
Hawa wapinzani hawatuwezi, sasa ni fimbo tu, tutawapinga chadema fimbo hapa JF, na kisha tutawachanganya kwenye uongozi na mwisho watu watajua kuwa ccm pekee ndio chama kubwa.

.... ha ha ha haha .. hawa hawaijui ccm....

Niliwaonya hapa hawakusikia.

Kama huijui kazi ya usalama wa taifa sasa umeijua, tumeshawatoa kwenye debate ya EPA, meremeta, na story zingine zote za uzushi na tumewaweka hapa ambako mtagongana hadi 2010 na ccm itashinda kwa kishindo.

This guy must be schizophrenic.
 
"Anasingiziwa" mambo mengi huyu Wangwe yakiwemo uvutaji wa bangi! Wengi humu JF huwa hatupendi kuongelea PRIVATE LIVES zetu ingawa binafsi naamini tena kwa DHATI kuwa PRIVATE LIFE ya mtu ndio mtu mwenyewe. Na inakuwa na umuhimu wa pekee kuifahamu pale mtu huyo anapokamata MADARAKA au UONGOZI wa UMMA.

Kwa private Life ukienda huko Mbowe ni mchafu zaidi naomba huko tusiende,
kiongozi wa Conservative ya UK bwana David Cameroon alikiri kuwa alikuwa mvuta bangi mkubwa na amekiwezesha chama chake kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa hivi karibuni, Labour Party kwa miaka 30 hawajahi kupoteza nafasi za uchaguzi kama huu wa hivi karibuni chini ya David Camerron, na kwa mara ya kwanza Conservative wamepata nafasi ya umeya wa jiji la London, hata Obama alikuwa anafuta bangi alipokuwa kijana.

Mbowe alikuwa mwanachama wa Wapuki uliza wanaojua watakwambia maana yake. kwa maneno tuamini kuwa Wangwe kaondolewa kwa ajili ya private life yake? jee hamkuliona wakati mnampa uanachama, ubunge na umakamu wa mwenyekiti?
 
This guy must be schizophrenic.

Utasema chochote lakini ccm ndio mwanzo tumeanza kuwavuruga wapinzani. Kama umesahau kilichotokea kati ya Mrema na Marando, huu ni mwanzo tu.

Kama kawaida watu wa musoma dhidi ya watu wa kilimanjaro.

Wangwe=Marando
Mrema=Mbowe
 
Mkuu Mtanzania

Nafikiri hata yeye mwangwe wakati anakuwa M/Mwenyekiti aliona katiba ya chama chake na kukubaliana nayo. Kama kuna mapungufu tunatakiwa kuchallenge katiba ya chadema kwa sasa. Kwamba katiba haiko sawa, lakini vile vile unajua sasa hivi tuko katika vita zidi ya ufisadi mafisadi mpaka sasa wanajua waliangukia wapi.!

Mnapokuwa mnapigana vita ya namna hii lazima cha kwanza ni kuaminiana. Kunapokosekana uhaminifu kwa viongozi ni jambo la hatari kubwa sana. Na ikifikia hapo sijui, hawana budi kutumia mamlaka ya kikatiba kuhakikisha wanalinda chama. Sasa ni haki ya wangwe kukata rufaa lakini tayari wameisha ondoa sumu katika chama.
 
Gembe ,kusema kuwa mimi ni mchagga its very wrong.

Usifanye ,usiwaze na wala usiandike kitu kwa hisia ,kuwa eti nami ni mchagga huu ni upotoswaji wa wazi kwani kwanza wewe hata hunijui wala sura yangu huijui.

Acha kupotosha .

Sirudi Mara Mbili,na Nitasema Ukweli Daima na uongo kwangu Mwiko na Naomba kwa Heshima MMrudishe CHACHA WANGWE
 
Zemarcopolo, Mchelea Mwana, Mgagagigikoko, Kubwa Jinga,

Bahati mbaya mmesikia kile ambacho sikusema na kile ambacho nilisema hamkusikia, na hili ni kosa langu kwa sababu inaonekana nilichagua vibaya maneno yangu kiasi kwamba nikaeleweka vile ambayo sikutaka nieleweke.

Hakuna ubishi kwamba Mhe Wangwe hana maelewano na viongozi wenzake wa kitaifa na hata ndani ya kambi ya upinzani bungeni. Sasa hili huwezi kusema kwamba sio tatizo.

Natambua pia nguvu na umuhimu wa Wangwe katika chama chetu. Huyu ni kiongozi jasiri sana mwenye historia ya mapambano ambayo ni muhimu sana kwa siasa za upinzani katika bara la Afrika. Hakuna kiongozi mwingine wa CHADEMA aliyekumbana na misukosuko na mabavu ya serikali ya CCM kama Wangwe na akayashinda.

Kwa hiyo ni bahati mbaya kwamba nilitumia neno mzigo, lakini kwa kweli nilichomaanisha ni hilo la yeye kushindwa kujenga maelewano na viongozi wenzake ambayo ni muhimu sana. Kwa wale wanaopenda maendeleo ya Wangwe kisiasa kama mimi ni muhimu sana wakampa darasa la interpersonal relationships. Ni vigumu sana kufanikiwa kisiasa bila kuwa na mahusiano mazuri na viongozi wenzako. Haiwezikani wewe peke yako tu uwe sahihi na wenzako wote hawapo sahihi. Nafikiri naeleweka.

Baada ya kusema hayo naomba nieleweka kwamba, pamoja na kutambua udhaifu wa Mhe Chacha, mimi sio miongoni mwa wanachama wa CHADEMA wanaunga mkono kusimamishwa kwake uongozi. Ninapinga hili kwa sababu kusimamishwa kwake hakuiongezei CHADEMA tija yeyote zaidi ya kuturudisha nyuma katika jitihada zetu za kujenga chama mbadala kwa CCM. Ninapinga pia kwa sababu timing yake sio nzuri ukizingatia kwamba mwaka huu tuna uchaguzi ndani ya chadema. Someni tena reaction yangu kuhusu statement iliyotolewa na CHADEMA, kuna kitu ambacho nilikisema na hamjakinyaka au mlikipuzia.

Hata hivyo ninawapa the benefiti of doubt wajumbe wetu wa kamati kuu kwa sababu ninaamini kwamba walichuja vizuri pros na cons za maamuzi yao kabla hawajafika walipofika. Ninaamini pia kwamba wajumbe wa kamati kuu walimpa kila nafasi ya kujirudi mhe Wangwe lakini ndio hivyo tena ilishindikana na iliwalazimu kufanya maamuzi magumu kama viongozi wa chama.

Kitila.

Wanaounda kamati kuu wamechaguliwa na Mbowe hili halina ubishi, ni Mbowe aliyewapa nafasi hizo Baregu na Ngaiza na wengine, ni sawa na kusema waziri Pinda,Ngereja na waziri Membe ambao wamepewa ulaji na JK waitwe na kuambiwa watoe maamuzi ya yaliyo na maslahi na JK au maslahi ya JK yanahatarishwa na mtu let say Sumaye, unafikiri jibu litakuwaje?

Chacha Wangwe.

Ni mbunge pekee katika Chadema aliyeshinda kwa ushindi mkubwa kwenye ubunge kwa wastani wa asilimia 65 hadi 70 hakuna mbunge yeyote wa upinzani Tanzania Bara aliyepata kura hizo, huko kote kapita kwa kishindo na kama angeenda kwenye Uenyekiti angechukua, kusema kuwa hana interpersonal skills ni kumkandamiza kwa vile wewe Kitila, Mnyika, Tundu Lissu, Zitto mko upande wa Mbowe ambao unaitwa upande wa wasomi, ndio maana mzee Halimoja amekuwa akitukanwa na upande huu kwa kujaribu kuwa na mawazo halisi, haiwezekani Wangwe akawa mzigo na mjinga wakati ameshinda kwa kishindo kikubwa jimboni kwake.

Kama mliuvumilia mzigo wake kwanini msisubiri hadi mwezi wa nane yaani mwezi mmoja tu wakati wa uchaguzi wa mkuu wa chama? kwa akili zangu ndogo inaonekana miezi saba aliyokaa madarakani kama makamu amejijenga kiasi mnaogopa kuwa akiingia kwenye mkutano mkuu kama makamu anaweza kuchukua uenyekiti.

Chadema kwa hili mmedhihirisha kuwa sio chama bali ni platform ambayo watu wanaitumia kufikia malengo yao,
kama vikao vya faragha wakufukuzwa ni Zitto Kabwe ambaye wote mnajua kuwa ana ukaribu mkubwa na JK kuliko Mbowe.

Wangwe amepunguzwa kasi au amefungwa spidi gavana na wenye chama chao.
 
Wangwe=Marando,

Wapinzani hawaijui ccm, hili ni chama kubwa. Tutawavuruga hadi washangae
 
Back
Top Bottom