CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

cuf.....cuf.....cuf.....!
ukiona Mwenzako Kanyolewa Wewe Tia Maji Then Usogee Kwa Kinyozi Yuleyule Na Wembe Ule Ule. Wembe Ulionyoa Nccr Raskazone 1990's .....!

...trash talking as ussual!
 
Kilichonichosha kwenye hili saga ni hiyo statement ya Mbowe. Yaani imenikumbusha jinsi
akina Hamad na wenzake walivyotolewa CCM na statement zilizofuata baada ya hapo.

Sikutegemea statement kama hiyo itoke CHADEMA. Binafsi naamini kitendo alichofanya Mbowe na wapambe wake kitairudisha CHADEMA hatua kama tano nyuma.

Kingine kilichonishangaza ni jinsi mbowe na wapambe wake walivyojaribu kuidanganya JF hapo jana kwamba kikao kilichomwondoa ndio kilimchagua na pia kwamba Mbowe alikuwa kaimu mwenyekiti wa CHADEMA. Naamini lengo lilikuwa kuidanganya JF ili kuficha mapinduzi waliyofanya. Kaimu huwa hachaguliwi wala hagombei, huteuliwa. Kampeni zile zote za Chacha kugombea tunazikumbuka, sasa ghafla mtu anakuja hapa JF kutulisha sumu za uongo, WHY? Anataka wananchi ndio tumwamini mtu kama huyo hata kuwa rais wa nchi?
http://www.chadema.net/uongozi/index.php Wangwe alikuwa makamu wa mwenyekiti wa CHADEMA na wala sio kaimu. Unajua maana ya kusema kaimu ni kuonyesha walimpa fadhila kwa kumpa hicho cheo na sasa wamemnyang'anya kwa utovu wa nidhamu. Hiyo ni SPIN at its best.

Kwasababu uchaguzi unakuja, nafikiri wakati umefika wa watu makini wa CHADEMA kumkabili Mbowe kwenye uchaguzi. Nimewahi kuandika hapa siku za nyuma kwamba MBOWE aliifaa CHDEMA ya mwaka 2005 lakini kwasasa atakuwa mzigo kwa chama. Mbowe ana mizigo mingi sana kichwani ambayo inatokana na watu aliokuwa anashirikiana nao huko nyuma. Kwa mfanybiashara kwa mazingira ya Tanzania ni ngumu sana kuwa clean kwenye nchi iliyojaa ufisadi.

Kitu kimojawapo ambacho CHADEMA ilitakiwa wakifanyie kazi ni hii dhana ya wananchi kuamini ni chama cha Wachaga na kuna mambo ya ukabila. Hii ndio inaweza kuwa mwuuaji wa CHADEMA. Nasema dhana kwasababu huenda ukweli ni tofauti kabisa, kuna watu wengi tu CHADEMA ambao hawatoki Kilimanjaro. Kwenye siasa perception inatosha kuwafanya watu waamini hata kama wanachoamini sio kweli. Angalia yaliyompata Salim, ni hiyo hiyo perception. Kitendo cha kumfukuza Wangwe, kinakuza hii perception badala ya kuipunguza. Kwa viongozi toka makabila makubwa TZ, sio tu wasiwe na ukabila lakini pia matendo yao yaonyeshe hata kidhana kwamba hawaungi mkono ukabila. Wale wabunge wa viti maalumu CHADEMA ukiwaangalia, mtu asiyejiuliza mara mbili na akiaambiwa na Makamu mwenyekiti wa chama, anaelewa wazi hapo kuna tatizo.

Hima kwenu CHADEMA, msipigane mangumu na tumieni uchaguzi ili kupata baraka za wanachama wenu.
 
Hawa watu wananipa raha kweli.Kwa njia hizi wanadhani wtaweza kuwatoa CCM.These are times when they are supposed to stay and hold on to each other to oust this power mongers yet they are breathing under each other's throat too bad but we will stand behind you when it comes to removing mafisadi.
 
Mwanakijiji, unajua kwanini hawasemi?. TUMBO. Wanaogopa kumkosea MWENYEKITI na MWENYECHAMA CHAKE.

Muda haukuwa sahihi. Kama uchaguzi wa CHADEMA ni mwaka huu kwanini waanzishe vurugu ndani ya chama wakati wangeweza kusubiri wanachama waseme?!?.

Kwani ni dhambi ukiwa Chadema kuongea na aliyehamia CCM?, huu ni ubinafsi na kutaka kuhodhi madaraka. Kumbuka mimi sisemi kuwa Wangwe hana matatizo. Ila nasisitiza maslahi binafsi yalitangulizwa zaidi kuliko maslahi ya kichama na kinchi.

Asante

Mkulu dhambi sio kuongea na mtu aliyehama chama dhambi ni kuongea nae nini, kama mnaongea mambo yenu hamna tabu lakini kama mnakaa vikao vya nyuma ya pazia makamu mwenyekiti na watu walifukuzwa mnashirikiana na mtu wa chama cha upinzani ambaye tangia mwanzo alishaonekana ni CCM, kumb. issue ya Dr. Kitine tayari cadema walitakiwa kuwa macho na mtu wa aina hiyo.

Huyu jamaa tangia mwanzo wakati wanamchagua nilisema wamelamba garasa maana anajulikana kuwa ni timu ya akina kabouru tangia wakiwa NCCR Mageuzi kwa vitendo vyake, watu hawakuamini wakasema apewe nafasi then you can see.
 
Halafu CHADEMA acheni uhuni wa kumlaumu Chacha. Mkiendelea kumdhalilisha Chacha mnatuma ujumbe kwa taifa kuwa mtu yeyote anaweza kusneak in your system mpaka nafasi ya juu kwa lengo la kuhujumu chama kama mlivyoandika kwenye ripoti yenu which means hamuwezi kuongoza Taifa maana hamna means za kufilter out viongozi wabovu.

...very interesting 😀 ! umeponda in such a way ukaifagilia CHADEMA humo humo! Try to read 'backwards'.
 
Ndugu zangu hii ni formula MPYA YA AFRIKA....MAHESABU YA WEMBE MKALI NA USHAURI WA KUNGURU MWEUPE NA JMUSHI...NTAAWAMBIA BAADAE.
TUANGALIE DODOMA KWANZA.
 
Wangwe kuishitaki CHADEMA




na Mwandishi Wetu, Dodoma



ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chacha Wangwe, ambaye alisimamishwa uongozi juzi, amesema atakifikisha chama hicho mahakamani iwapo kitamzushia kashfa ambazo si za kweli.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, baada ya CHADEMA kutoa taarifa rasmi kuelezea kusimamishwa kwake katika nafasi ya makamu mwenyekiti, Wangwe aliwataka viongozi wa chama hicho wanaomtuhumu kwa mambo mbalimbali, kuyathibitisha madai yao, huku akionya na kusisitiza kuwa, iwapo watamzulia jambo lolote, atakwenda mahakamani.

"Hawawezi kunituhumu kwa masuala ya uongo. Inabidi wa-prove (wathibitishe) tuhuma wanazotoa dhidi yangu… kama wanasema nimevujisha nyaraka wathibitishe hivyo, kama wanasema nakihujumu chama wathibitishe pia," alisema Wangwe.

Hata hivyo, alikiri kusimamishwa uongozi, lakini akasema kusimamishwa kwake kumetokana na hila za Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye juzi katika mkutano wa Kamati Kuu alieleza kuwa hawezi na hataki kufanya kazi na yeye.

Alisema kuwa ni kweli uamuzi wa kusimamishwa kwake ulifikiwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho baada ya wajumbe wa Kamati Kuu kupiga kura ya kuafiki uamuzi huo, lakini alidai kuwa maamuzi hayo yalichagizwa na msimamo wa Mbowe.

"Tuhuma zote walizotoa walishawahi kuzitoa awali na nikazijibu… huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya CHADEMA, na nadhani wanafanya hivi kama sehemu ya kampeni dhidi yangu," alisema.

Aliliambia gazeti hili kuwa hivi sasa anataka kukata rufaa katika Baraza Kuu la chama hicho kwa sababu Kamati Kuu si chombo cha mwisho kufikia maamuzi kuhusu suala hilo.

Aidha, alisema anakusudia kuipeleka ajenda hiyo kwa wanachama, ili waweze kujua ukweli halisi kuhusu jambo hilo.

"(Viongozi wa CHADEMA) Wanajua kuwa kuna kundi kubwa la wanachama mikoani wananiunga mkono, kitendo chao kinalenga kuninyima jukwaa la kuzungumzia, lakini wanachama wananiamini na ndiyo maana waliamua kunipa jimbo Tarime na umakamu mwenyekiti mwaka jana," alisema.

Awali, viongozi kadhaa wa CHADEMA waliorodhesha tuhuma takriban nne, dhidi ya Wangwe, zilizosabisha asimamishwe kushika wadhifa huo.

Aidha, licha ya kufafanua tuhuma hizo akisaidiwa na viongozi wengine waandamizi, Mbowe aliwaeleza waandishi wa habari mlolongo wa hatua zilizochukuliwa ili kumrejesha kiongozi huyo katika mstari.

Mbowe alisema Kamati Kuu ya chama hicho, iliyokutana mjini hapa juzi hadi usiku wa manane, ilifikia hatua ya kumsimamisha Wangwe baada ya wajumbe wa kamati hiyo kupiga kura za siri, kama ambavyo inaeleza sehemu ya katiba ya CHADEMA.

Ilielezwa katika mkutano huo wa waandishi wa habari kuwa, tangu Wangwe achaguliwe kukaimu nafasi hiyo, amekuwa akikisababishia chama matatizo kwani hana ushirikiano na viongozi wenzake na ameshiriki katika kufanya mambo kadhaa ambayo yanakihujumu chama hicho, akishirikiana na watu wengine wa nje wasioitakia CHADEMA mema.

Mbowe alisema kuwa chama hicho kinaongozwa na katiba, kanuni, maadili na itifaki, na inapotokea kiongozi akakiuka hayo, kama ambavyo Wangwe anatuhumiwa kufanya, chama hakiwezi kuulea udhaifu huo.

Orodha ya tuhuma zilizosababisha Kamati Kuu ya CHADEMA imsimamishe Wangwe katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, ilitolewa na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Tundu Lissu.

Lissu aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Wangwe anajihusisha na makundi au kufanya vitendo vya uchochezi akishirikiana na mtu (jina tunalihifadhi) ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa CHADEMA kabla ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aliitaja tuhuma nyingine dhidi ya Wangwe kuwa ni kutoa tuhuma nzito, lakini zisizo na msingi wala ukweli dhidi ya viongozi wa juu na watendaji wa chama hicho bila kupitia taratibu mahsusi.

"Wangwe amesambaza vipeperushi na maandiko ya mkono wake, akikituhumu chama kwa ufujaji wa fedha na rasilimali, uzushi kuhusu kutotoa ruzuku mikoani na mahesabu ya chama wakati anajua kabisa kuwa Kamati Kuu inapokea na kupitia mahesabu yote ya chama," alisema Lissu.

Aliitaja tuhuma nyingine dhidi ya Wangwe kuwa ni kukikashifu chama, viongozi na watendaji wa chama wa ngazi za juu kwa kutumia njia zinazokiuka taratibu za chama na ukosoaji wa kisiasa.

Akiifafanua tuhuma hiyo, Lissu alisema kuwa Wangwe amekuwa akisambaza taarifa ya maandishi kuwa kuna ukabila ndani ya chama hicho, akielezea mgawanyo wa nafasi za ubunge wa viti maalum kuwa ni kigezo.

Hata hivyo, baadaye, Mkurugenzi wa Vijana wa chama hicho, John Mnyika alitoa ufafanuzi kuhusu taratibu zilizofanyika kuwapata wabunge hao na kueleza kuwa iwapo CHADEMA ingepata nafasi nyingi, ingekuwa na wabunge kutoka katika kila mkoa kwa mujibu wa orodha waliyoiwasilisha katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Lissu aliitaja tuhuma nyingine dhidi ya Wangwe kuwa ni kuvujisha taarifa za siri za vikao vya chama kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa anaonewa na kudhulumiwa ndani ya chama na baadhi ya viongozi na sekretarieti.

Akifafanua kuhusu tuhuma na hatua zilizochukuliwa dhidi ya Wangwe, Mbowe alisema kuwa kiongozi huyo amekosa ushirikiano mzuri na karibu viongozi wengine wote wa juu wa CHADEMA, wakiwamo wazee wa chama hicho na watendaji.

Alisema hali hiyo inakiathiri chama hicho na kudumaza demokrasia kwa jumla na kimeona ni bora kichukue hatua hizo pamoja na kuwa inafahamika kuwa zitakitikisa chama hicho, kwani ‘chama ni zaidi ya mtu'.

Akielezea hatua za kumrejesha Wangwe katika mstari, Mbowe alisema kuwa tayari wameshafanya vikao kadhaa, vikiwamo vya sekretarieti, yeye na katibu na Wangwe na vikao vya wazee, na amekuwa akikubali makosa na kuahidi kushirikiana, lakini hugeuka muda mfupi baada ya kutoka katika vikao hivyo.

Baadaye, Katibu Mkuu wa CHADEMA, ambaye pia ni Mbunge wa Karatu, Makamu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa wabunge wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, alisema Wangwe, ambaye pia ni Mbunge wa Tarime, amekosa ushirikiano na wabunge wenzake na kambi nzima ya upinzani bungeni.
 
Kwa Hiyo Rais Atoke Chadema?
Mwakeyembe Naye Aongee.

Kwasababu..ndugu zangu sijui kama mnakumbuka ile thread jinsi nilivyosema msimuweke kwenye umakamu!
Kama mtu alisambaza vipeperushi kila mahali vya kashfa na ikagundulika hivyo..Then umakamu mulimpa wa nini kama aliyokuwa akisema si kweli?
OK assume ni kweli...Then mulimrudisha ili muje kumtoa wakati gani?
kwanini wakati huu?
ili iweje?
Mungemkatalia umakamu wakati ule...Then hoja yenu ingekuwa ya nguvu...Lakini kumweka madarakani baada a kashfa na kusubiri wakati huu wa MIJADALA NYETI!
THEN MUTATUPANDISHA HASIRA.
Kelele nilipiga hapa utafikiri na mimi ni CHADEMA.
Sasa either mliyadharau maoni yangu...Ama mlijuwa nini kinaendelea...Na mkaendelea tu.
 
Mambo Ya Zimbawe Yameisha!
Ghafla Sasa Ya Chadema?
Who Cares About The Party At This Moment?
 
"Anasingiziwa" mambo mengi huyu Wangwe yakiwemo uvutaji wa bangi! Wengi humu JF huwa hatupendi kuongelea PRIVATE LIVES zetu ingawa binafsi naamini tena kwa DHATI kuwa PRIVATE LIFE ya mtu ndio mtu mwenyewe. Na inakuwa na umuhimu wa pekee kuifahamu pale mtu huyo anapokamata MADARAKA au UONGOZI wa UMMA.
 
Najua wamemsimamisha kwa sababu walikua hawamtaki kwasababu ana jazba, lakini hoja zake wana zikiliza? kuna madai ya kwamba 20% ya wabunge wakuteuliwa wanatoka mkoa wa kilimnjaro hilo chadema wanalijibu vipi? kuomba ruzuku kilamwenzi angalau shs 100000 ipelekwe wilayani chadema wajibu kwanza halafu suala la kumfukuza au kusimamishwa tena kwa kusingizia anatoa siri za chama sindio hayo slaa aliyo bishana na waziri mkuu ijumaa(kwamba kama siri kwa serikali ufisadi basi bora yeye afungwe)
 
Ondoeni Usanii Wenu!
Kwani Nani Hajui Hayo?
Eti Wangwe Na Mbowe!
Sasa Kuna Mtu Keshawahi Kutaja Hayo Majina Hivi Karibuni?
Na pia mlishindwa vipi kuhold on hadi tuone ni whats going on BUNGENI?
Wacha Wabunge Tuwasikie Kwanza Then Everyhing Baadae.
Chama Later...taifa Bungeni!
Pls Wakuu.
 
Kama Tumekataa Kusikiliza Mambo Ya Zimbabwe..mutatuletea Vipi Haya Mambo Wakati Kama Huu?
Nyie Mmeshaharibu Na Badala ya Kurekebisha Naona Sasa Mnamalizia Moja Kwa Moja.
We Dont Want Personal Battles In The Midst Of The Most Defining Moment.
 
Wengine tulipopata habari hii tulisinyaa. Nitakuwa mnafiki mkubwa nikisema kwamba hii sio habari mbaya kwa CHADEMA. Ukweli ni kwamba ni habari mbaya ambayo bila shaka itatusumbua kwa muda kabla haijatulia. Niseme pia kwamba hii ni habari njema kwa CCM maana ndiyo siasa ilivyo; msiba wa mpinzani wako kwako ni harusi.

Sasa kuna watu wana hamu ya kusikia sisi wengine ambao ni wanachama wa wazi wa CHADEMA tunasemaje. Mimi nikiri kwamba Chacha ni mzigo kwa uongozi wa pamoja sio tu ndani ya CHADEMA bali hata kwa kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa sio mtu wa kwenda kwa maamuzi ya pamoja (tusisahau huyu bado ni kiongozi kwa kuwa bado ni mbunge na M/Kiti wa chama chetu Mkoa wa Mara).

Pamoja na hayo, binafsi ningependa sana kutoka kwa Wangwe katika uongozi ingekuwa ni kwa njia ya kiheshima zaidi kuliko ilivyotokea. Ningependelea kwamba afike mahala akiri makosa yake na aone kwamba amekuwa ni mzigo kwa CHADEMA badala ya msaada na hivyo aone haja ya kujiuzulu mwenyewe kwa maslahi ya chama badala ya kufukuzwa. Ndivyo inavyofanyika katika vyama vinavyojiandaa kuchukua dhamana ya uongozi wa nchi. Mtaposikia kiongozi fulani wa chama fulani sehemu fulani amejiuzulu huwa mara nyingi sio kwa hiari bali kwa shinikizo ili kumtunzia heshima. Huwa ni mara chache sana inapolazimika kuanikwa makosa yote ya kiongozi mfukuzwa wazi kiasi hiki. Hata hivyo naamini Wangwe alipewa nafasi ya kujitetea na kujiuzulu na, kwa hulka yake, atakuwa aligoma na hivyo kuilazimu Kamati Kuu kuchukua maamuzi mazito na magumu kama haya.

Niseme kidogo pia kuhusu statement iliyotolewa. Kwa kiasi kikubwa maelezo yaliyopo katika tamko la CHADEMA yanajenga taswira tata kwa wananchi wa Tarime. Yatawafanya wajilaumu kuwa na mbunge wa aina ya Chacha. This is unfortunate and I must painfully acknowledge here that the statement was not carefully crafted. It would appear that there was an obsessiveness with getting rid of Chacha without due consideration to the consequences on our constituents and the future electability of Chacha and our party in Tarime. Statement kama hii itatunzwa na wapinzani wetu huko Tarime na watainyofoa kwenye uchaguzi wa 2010.

Nimalizie kwa kusema hivi uongozi ni pamoja na kuchukua maamuzi magumu ambayo ni unpopular for the time being lakini yenye tija kwa muda mrefu ujao. Ninaamini kwamba Kamati Kuu ya chama chetu ilijiridhisha kwamba hapakuwa na njia mbadala ya kutatua tatizo la kiuongozi la Wangwe isipokuwa hii walioichukua. Kamati Kuu ya CHADEMA ninaijua vizuri; siamini kwamba wangeweza kuchukua maamuzi magumu na yenye kukirudisha nyuma chama chetu kisiasa kama kungekuwa na njia ingine mbadala zaidi ya hii waliyopita.



Kitila,
Unless uwe mbumbumbu, lakini ukisoma taarifa ya kuachishwa Wangwe utaona kuwa huo uamuzi kabisa umejaa alama za ugomvi wake na Mbowe. Kila sababu iliyotajwa sio ya leo, zilikuwepo kabla hata ya Wangwe kuingia uongozini. Na tunaweza sema, Chadema mikoani ndio walizitumia hizo sababu kumchagua Wangwe. Sasaumefika wakati wa Mbowe naye kuondolewa ili chama kishikwe na watu wenye akili njema na busara na sio mtu asiyetaka kukosolewa kwa vile tu ana-support ya waasisi wa chama.
 
Nawaangalia tu.. wenye kujua hawasemi, na wasiojua wanasema sana kana kwamba wanajua.

Mkuu MJJ,
Kwani wanaojua ni akina nani? Wengine tuliambiwa na wewe ni inner circle ya CHADEMA, hebu kataa hilo au utuambie wanaojua ni akina nani?
 
Wangwe kuishitaki CHADEMA

na Mwandishi Wetu, Dodoma


ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chacha Wangwe, ambaye alisimamishwa uongozi juzi, amesema atakifikisha chama hicho mahakamani iwapo kitamzushia kashfa ambazo si za kweli.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, baada ya CHADEMA kutoa taarifa rasmi kuelezea kusimamishwa kwake katika nafasi ya makamu mwenyekiti, Wangwe aliwataka viongozi wa chama hicho wanaomtuhumu kwa mambo mbalimbali, kuyathibitisha madai yao, huku akionya na kusisitiza kuwa, iwapo watamzulia jambo lolote, atakwenda mahakamani.

“Hawawezi kunituhumu kwa masuala ya uongo. Inabidi wa-prove (wathibitishe) tuhuma wanazotoa dhidi yangu… kama wanasema nimevujisha nyaraka wathibitishe hivyo, kama wanasema nakihujumu chama wathibitishe pia,” alisema Wangwe.

Hata hivyo, alikiri kusimamishwa uongozi, lakini akasema kusimamishwa kwake kumetokana na hila za Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye juzi katika mkutano wa Kamati Kuu alieleza kuwa hawezi na hataki kufanya kazi na yeye.

Alisema kuwa ni kweli uamuzi wa kusimamishwa kwake ulifikiwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho baada ya wajumbe wa Kamati Kuu kupiga kura ya kuafiki uamuzi huo, lakini alidai kuwa maamuzi hayo yalichagizwa na msimamo wa Mbowe.

“Tuhuma zote walizotoa walishawahi kuzitoa awali na nikazijibu… huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya CHADEMA, na nadhani wanafanya hivi kama sehemu ya kampeni dhidi yangu,” alisema.

Aliliambia gazeti hili kuwa hivi sasa anataka kukata rufaa katika Baraza Kuu la chama hicho kwa sababu Kamati Kuu si chombo cha mwisho kufikia maamuzi kuhusu suala hilo.

Aidha, alisema anakusudia kuipeleka ajenda hiyo kwa wanachama, ili waweze kujua ukweli halisi kuhusu jambo hilo.

“(Viongozi wa CHADEMA) Wanajua kuwa kuna kundi kubwa la wanachama mikoani wananiunga mkono, kitendo chao kinalenga kuninyima jukwaa la kuzungumzia, lakini wanachama wananiamini na ndiyo maana waliamua kunipa jimbo Tarime na umakamu mwenyekiti mwaka jana,” alisema.

Awali, viongozi kadhaa wa CHADEMA waliorodhesha tuhuma takriban nne, dhidi ya Wangwe, zilizosabisha asimamishwe kushika wadhifa huo.

Aidha, licha ya kufafanua tuhuma hizo akisaidiwa na viongozi wengine waandamizi, Mbowe aliwaeleza waandishi wa habari mlolongo wa hatua zilizochukuliwa ili kumrejesha kiongozi huyo katika mstari.

Mbowe alisema Kamati Kuu ya chama hicho, iliyokutana mjini hapa juzi hadi usiku wa manane, ilifikia hatua ya kumsimamisha Wangwe baada ya wajumbe wa kamati hiyo kupiga kura za siri, kama ambavyo inaeleza sehemu ya katiba ya CHADEMA.

Ilielezwa katika mkutano huo wa waandishi wa habari kuwa, tangu Wangwe achaguliwe kukaimu nafasi hiyo, amekuwa akikisababishia chama matatizo kwani hana ushirikiano na viongozi wenzake na ameshiriki katika kufanya mambo kadhaa ambayo yanakihujumu chama hicho, akishirikiana na watu wengine wa nje wasioitakia CHADEMA mema.

Mbowe alisema kuwa chama hicho kinaongozwa na katiba, kanuni, maadili na itifaki, na inapotokea kiongozi akakiuka hayo, kama ambavyo Wangwe anatuhumiwa kufanya, chama hakiwezi kuulea udhaifu huo.

Orodha ya tuhuma zilizosababisha Kamati Kuu ya CHADEMA imsimamishe Wangwe katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, ilitolewa na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Tundu Lissu.

Lissu aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Wangwe anajihusisha na makundi au kufanya vitendo vya uchochezi akishirikiana na mtu (jina tunalihifadhi) ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa CHADEMA kabla ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aliitaja tuhuma nyingine dhidi ya Wangwe kuwa ni kutoa tuhuma nzito, lakini zisizo na msingi wala ukweli dhidi ya viongozi wa juu na watendaji wa chama hicho bila kupitia taratibu mahsusi.

“Wangwe amesambaza vipeperushi na maandiko ya mkono wake, akikituhumu chama kwa ufujaji wa fedha na rasilimali, uzushi kuhusu kutotoa ruzuku mikoani na mahesabu ya chama wakati anajua kabisa kuwa Kamati Kuu inapokea na kupitia mahesabu yote ya chama,” alisema Lissu.

Aliitaja tuhuma nyingine dhidi ya Wangwe kuwa ni kukikashifu chama, viongozi na watendaji wa chama wa ngazi za juu kwa kutumia njia zinazokiuka taratibu za chama na ukosoaji wa kisiasa.

Akiifafanua tuhuma hiyo, Lissu alisema kuwa Wangwe amekuwa akisambaza taarifa ya maandishi kuwa kuna ukabila ndani ya chama hicho, akielezea mgawanyo wa nafasi za ubunge wa viti maalum kuwa ni kigezo.

Hata hivyo, baadaye, Mkurugenzi wa Vijana wa chama hicho, John Mnyika alitoa ufafanuzi kuhusu taratibu zilizofanyika kuwapata wabunge hao na kueleza kuwa iwapo CHADEMA ingepata nafasi nyingi, ingekuwa na wabunge kutoka katika kila mkoa kwa mujibu wa orodha waliyoiwasilisha katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Lissu aliitaja tuhuma nyingine dhidi ya Wangwe kuwa ni kuvujisha taarifa za siri za vikao vya chama kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa anaonewa na kudhulumiwa ndani ya chama na baadhi ya viongozi na sekretarieti.

Akifafanua kuhusu tuhuma na hatua zilizochukuliwa dhidi ya Wangwe, Mbowe alisema kuwa kiongozi huyo amekosa ushirikiano mzuri na karibu viongozi wengine wote wa juu wa CHADEMA, wakiwamo wazee wa chama hicho na watendaji.

Alisema hali hiyo inakiathiri chama hicho na kudumaza demokrasia kwa jumla na kimeona ni bora kichukue hatua hizo pamoja na kuwa inafahamika kuwa zitakitikisa chama hicho, kwani ‘chama ni zaidi ya mtu’.

Akielezea hatua za kumrejesha Wangwe katika mstari, Mbowe alisema kuwa tayari wameshafanya vikao kadhaa, vikiwamo vya sekretarieti, yeye na katibu na Wangwe na vikao vya wazee, na amekuwa akikubali makosa na kuahidi kushirikiana, lakini hugeuka muda mfupi baada ya kutoka katika vikao hivyo.

Baadaye, Katibu Mkuu wa CHADEMA, ambaye pia ni Mbunge wa Karatu, Makamu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa wabunge wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, alisema Wangwe, ambaye pia ni Mbunge wa Tarime, amekosa ushirikiano na wabunge wenzake na kambi nzima ya upinzani bungeni.
 
Nafikiri kama ni mpinzani halisi aachane na kuwashtaki, hiyo itakuwa ni sawa na kumpa nafasi adui. Ugomvi wa ajabu ajabu ndani ya chama ni ufa au mwanya kwa adui. Wangwe kaa kimya kwa manufaa ya chama na upinzan kwa ujumla.
 
Lazima wadhibitishe madai yao!wasikupake matope WANGWE kisa MBOWE anakuchukua basi wote wanafuata mkumbo!Kweli CHADEMA demokrasia yenu ipo wapi?
 
chadema harakisheni mabadiliko haraka, kama ni kumwondoa mbowe sawa, sisi mbele kwa mbele na mafisadi, EHHHHEEE, nimesahau msiguse maaskari walioko mstari wa mbele kama akina slaa, zito nk
 
CHADEMA kwa hili hamna tofauti na wale wale,mnatia aibu
 
Back
Top Bottom