CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Mtu anapoadhibiwa kwa makosa mengi ukitaka kujua ukubwa wa kila kosa basi soma urefu wa maelezo yanayotolewa juu ya kila kosa. Kosa lililoelezewa kwa undani na urefu zaidi ni lile la kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku na swala la ukabila. Ni jukumu letu kuangalia mambo haya kwa undani.

Tuhumu za matumizi mabaya ya ruzuku zimeshasababisha viongozi kadhaa wajitoe CHADEMA, kwa mfano aliyekuwa mwenyekiti mkoa wa Morogoro. Tuhuma za ukabila kila siku zinaandikwa humu JF.Iweapo malamu mwenyekiti wa Taifa analalamikia ukabila then there is a serious problem!

Swala la kufanya mikutano ya siri ni ridiculous, hivi mtu akiwa kiongozi wa CHADEMA aruhusiwi kukutana na watu wasio CHADEMA kujadiliana nao maswala mbalimbali ya siasa.Mbona hamfukuzi Zitto kwa kufanya "vikao vya siri" na Salim A. Salim na Warioba?

CHADEMA bado haijaacha kuwa NGO.
 
Kabla WANGWE hajawekwa hapo alipotolewa kulikuwa na mjadala mzito sana hapa jf.
Na kutokana na sababu walizotoa za kumpinga CHACHA...Nilishangazwa sana na UAMUZI wao wa kumpa nafasi hiyo ya UMAKAMU Mwenye kiti.
Na ndio maana nimeona swali la FMES kuwa kwanini sasa?
KWANINI MUMPE UMAKAMU NA WAKATI HATA HAYO YANAYODAIWA KUWA KAYASEMA YALIKUWA WAAY BEFORE?
TENA KABLA HAMJAMPA UMAKAMU?
Kwenye hili CHADEMA MTANISAMEHE KWASABABU NILIWAKANYA NA KUWAAMBIA KAMA NI KWELI TUHUMA ZOTE HIZO ZA WANGWE NI ZA KWELI...THEN ILIKUWA VIPI MKAMPA UMAKAMU HUO?
NA KWANINI KOSA AMBALO MLISHAONEKANA KUMSAMEHE..MNALIRUDISHA WAKATI HUU?
AMA KUNA MENGINE MAPYA ?
Kwani nani hajui uchaguzi ni muda hata si mrefu ndugu zangu.
Kuna ambayo hamtaki kusema hapa jf?
HIVI HAPA JF KUNA KISICHOJULIKANA?
Ripoti ya EPA iko HAPA.
Na nyeti kibwena tu!
Tena hata ya madini sijui?
Anyways...Mimi wakati mkisubiri hayo ya CHADEMA...Mi nasubiri DODOMA KESHO!
 
Halafu CHADEMA acheni uhuni wa kumlaumu Chacha. Mkiendelea kumdhalilisha Chacha mnatuma ujumbe kwa taifa kuwa mtu yeyote anaweza kusneak in your system mpaka nafasi ya juu kwa lengo la kuhujumu chama kama mlivyoandika kwenye ripoti yenu which means hamuwezi kuongoza Taifa maana hamna means za kufilter out viongozi wabovu.
 
Kitila,
Mzigo wa kwanza na mkubwa zaidi wa CHADEMA ni Mbowe, otherwise kuna vijifurushi vingi tu kwenye hiyo NGO.
 
No!
Hapa si chacha vs flani ama vita ya CHADEMA.
NI MASLAHI YA TAIFA.
Chacha kweli alipiga kelele sana.
Tumesikia upande wa maamuzi yao ya kumsimamisha.
Lakini kuna mambo akifanya ya ajabu ajabu!
Nina hamu sana ya kusikia KAULI ZAKE ZA KUJITETEA ILI TUWEZE KUPATA UKWELI.
Ili tujuwe ni nani ana maslahi ya TAIFA NA NANI ANA MASLAHI MENGINE..EITHER YA CHAMA AMA WHATEVER.
Meanwhile...WARUDI BUNGENI ASAP!
 
No!
Hapa si chacha vs flani ama vita ya CHADEMA.
NI MASLAHI YA TAIFA.
Chacha kweli alipiga kelele sana.
Tumesikia upande wa maamuzi yao ya kumsimamisha.
Lakini kuna mambo akifanya ya ajabu ajabu!
Nina hamu sana ya kusikia KAULI ZAKE ZA KUJITETEA ILI TUWEZE KUPATA UKWELI.
Ili tujuwe ni nani ana maslahi ya TAIFA NA NANI ANA MASLAHI MENGINE..EITHER YA CHAMA AMA WHATEVER.
Meanwhile...WARUDI BENGENI ASAP!

Mushi hawa hawako serious na maslahi ya taifa kama unavyodhani,wangejali sana wangengoja at least kikao cha bunge kiishe!
Haohao wanaoclaim kupinga ubadhilifu ndio waliowachukua dada za girlftiends zao wakawapo ubunge wa viti maalum CHADEMA.Leo hii wanaonekana wapenda usawa.Kwenye mtego huo msikubali kunasa.

Kila mtu atimize jukumu lake na alipwe accordingly.
 
Lakini nadhani tutarudi kulekule kuwa upinzani strong ni ule wenye watu strong sio numbers peke yake. Ndio maana nikasema Wangwe simuoni kama ni dependably strong (maoni yangu).

Niliposema 'the big fuss' I meant habari ya Wangwe kaondolewa ukaimu makamu mwenyekiti tu, bado ni mbunge na mwenyekiti Mara. Lakini ukisoma kwa makini hoja za baadhi ya wachangiaji unaona kabisa kama walikuwa wanatauta nafasi ya kumsema Mbowe, uchaga nk. Nadhani hii haitakuwa thread yake, kwa sababu suala hapa ni Wangwe, na undani wa jambo lenyewe haujulikani sana (angalau kwangu) lakini watu tayari wamepamba moto kuhukumu watu, wakati nao wanalalamika Wangwe hajahukumiwa kwa haki! Mimi nadhani focus iwe Wangwe

Sawa, lakini kama mjadala ni kwamba "kaonewa au hajaonewa" itakuwa vigumu kutenganisha hilo swali na mjadala wa "kaonewa na nani"?

Hapo ndio Mbowe anakupokuja kwenye picha. Inawezekana watu wana mizizi binafsi na Mbowe, lakini nadhani, inabidi mnaodhani Mbowe hajakosea mumtetee bila kusema huu mjadala sio wa Mbowe. Inawezekana vielelezo vya "Wangwe kaonewa" ni pamoja na rekodi ya uhusiano wake na Mbowe.

Pia nataka kusema kitu kuhusu idea yako kwamba upinzani strong ni ule wa watu strong. Kuna tahadhari. Angalia jinsi NCCR ilivyo kufa ki mwamko Mrema alipokufa kisiasa. Angalia CCM ilipokufa kimaadili Nyerere alipokufa roho. Na jinsi DP kilivyo na kiongozi shupavu lakini hakiendi kokote kwa sababu Mtikila chama chake kinamzunguka mtu mmoja. Vyama vizuri vimejengwa kwenye institutions zake za ndani. Katiba nzuri, na inayofuatwa. Na Demokrasia ndani ya chama. Na ideology nzuri za chama.

Nataka kusema diversity ndani ya chama ni muhimu pia. Lakini hili neno 'diversity' nalichukia sana katika context ya Tanzania. Sisi hatukuwahi kulihitaji hili neno katika historia yetu. Marekani na South Africa ndio wana ma guilt ya ubaguzi ndio inabidi wasisitize haya mambo ya kuhakikisha kila ukoo unakuwa represented katika institutions zao. Kwa Tanzania, I wish tungekuwa hatujanza kuelekea huko. Labda ninaota!
 
Mkuu Nziku,

Heshima mbele bro, ni lini mligundua kuwa Wangwe ni mzigo mzito sana mpaka unahitaji kushushwa kwa kasi hii, kwa sababu sio muda mrefu toka achaguliwe kushika nafasi hiyo?

Au alipewa hiyo nafasi ili anyamaze na hakunyamaza kama ilivyotegemewa? just being curious

SWALI LA MSINGI NI HILI HAPA!
Maana kuna watu huwa wanalalamika hapa jf kuhusu floodings za postings!
Sasa kama tunazunguruka tuuuu!
Du!
 
...seems tunarudi NCCR enzi za kina Lamwai na yule mjinga mjinga wa usalama wa Taifa traitor marando,wanaopenda chadema huu ndio wakati wa kuziba weakness za kama hizo maana ni kweli huwezi kuwa na chama chenye nguvu kama kuna baadhi ya watu wana nguvu kuliko wengine na wanaweza kufanya maamuzi binafsi kwa faida zao na sio chama
 
Na mimi nataka nikueleze Mkuu FMES.
Wangwe akinyamaza basi hata BUBU MWENYE KUTAKA KUSEMA NI WAZI ATAPATA UWEZO HUO WA KUSEMA!
Na ndio maana naona this was a WRONG STRATEGY.
Huu hukuwa muda wa kufanya haya!
Wangekataa kumweka kwenye nafasi hiyo kama nilivyowaasa..Basi ninge waamini.
Zaidi zaidi kwasababu na sisi tunajua POLITICS...Then tunasubiri kwa hamu kubwa sana kikao cha kesho cha bunge huko DODOMA.
 
...seems tunarudi NCCR enzi za kina Lamwai na yule mjinga mjinga wa usalama wa Taifa traitor marando,wanaopenda chadema huu ndio wakati wa kuziba weakness za kama hizo maana ni kweli huwezi kuwa na chama chenye nguvu kama kuna baadhi ya watu wana nguvu kuliko wengine na wanaweza kufanya maamuzi binafsi kwa faida zao na sio chama


Koba, wanaopenda CHADEMA hawawezi kuziba weakness kwa sababu katiba ya chama imeweka kuwa wazee ndio wanaamua hatma ya chama. Vijana wa CHADEMA nawashangaa sana kukubaliana na uozo kama huu. Ninaamini kuwa kijana yeyote aliyekuwa politically smart hawezi kujiunga na CHADEMA.
 
Kesho kuna uwezekano wa mimi kufungua thread yangu ya mgombea binafsi...Tegemeana na kauli za wanasiasa wetu huko bungeni.
JF NI MKOMBOZI WA TANZANIA NA LABDA AFRIKA!
WAO HATA HAWAONI HILO?
 
Na mimi nataka nikueleze Mkuu FMES.
Wangwe akinyamaza basi hata BUBU MWENYE KUTAKA KUSEMA NI WAZI ATAPATA UWEZO HUO WA KUSEMA!
Na ndio maana naona this was a WRONG STRATEGY.
Huu hukuwa muda wa kufanya haya!
Wangekataa kumweka kwenye nafasi hiyo kama nilivyowaasa..Basi ninge waamini.
Zaidi zaidi kwasababu na sisi tunajua POLITICS...Then tunasubiri kwa hamu kubwa sana kikao cha kesho cha bunge huko DODOMA.
Hawezi kusema kwa sababu akifanya hivyo hata huo uenyekiti wa Mara ataupoteza na uanachama pia, whichi will mean atapoteza ubunge. Hata kwa namna nyingine CHADEMA wameanza kulionyesha taifa mediocre game.
 
Kwa hiyo mkuu zemacorpollo ushauri wako nini hasa?
 
Kwa hiyo mkuu zemacorpollo ushauri wako nini hasa?

Ushauri kwa Chacha ni kwamba kaamua kuingia kwenye siasa,hilo ndio joto lake.Atafute kona yenye joto analoweza kulimudu then aendeleze libeneke.
 
Haya Wangwe Tunajua Uko Hapa Na Chadema Wote.
Zemarcopolo Huyo.
 
Ni heri tumeweza kuwajua Chadema kabla ya 2010

Kwa hili genge la wahuni na mafisadi lililopo madarakani, ni sawa na kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi. Na pia msisahau kwamba CCM kuna mvutano mkubwa kati ya watetezi wa mafisadi na watetezi wa maslahi ya Watanzania na wengine wameshatoa tishio la kujiuzulu nyadhifa zao za ubunge. CCM inaweza kuona hii ya Chacha ni habari nzuri kwao, lakini yenyewe pia wako hoi bin taabani katika vurumai zinazoendelea kati ya makundi mawili yanayopingana.

Maswali ya kujiuliza kwa sasa ni je, kusimamishwa kwa Chacha kunagusa vipi maslahi ya Watanzania ukilinganisha na ufisadi mkubwa wa karibu shilingi bilioni 500 uliofanyika BoT? ufisadi uliofanywa na fisadi Mkapa wa kujimilikisha Kiwira Coal Plant katika mazingira ya kifisadi? Ufisadi wa Richmond na sasa Dowans ambapo TANESCO bado inawalipa shilingi 152 milioni kwa siku pamoja na kuwa hawazalishi chochote? Pamoja na baadhi ya mafisadi wa EPA kurudisha baadhi ya pesa ni sawa wao kuendelea kuwa huru? kwa manufaa ya nani?

Kuna haja kweli ya kuhamisha nguvu za Watanzania kuacha kujadili mambo ya kifisadi ambayo yanaathiri sana Watnzania kila kona ya nchi ili kujadili hili la Wangwe? Hili la Wangwe ni tatizo, lakini kamwe ukubwa wake hauwezi kulinganishwa na ufisadi uliofanywa na unaoendelea kufanywa dhidi ya nchi yetu. Tusipoteze nguvu na mwelekeo wetu.
 
Back
Top Bottom