Nachoipendea Chadema ni kwamba huwa wapo tayuari kukubali makosa na kufanya marekebisho haraka iwezekanavyo tofauti na CCM ambao maamuzi ya baadhi vionzogi wachache husimama kama mlima.
Mkuu Wangu Bob,
Nimekusikia, ninaomba kusema hivi sisi hapa forum wengi wetu ni watu wazima tena wenye akili timamu, ukweli wa hii ishu upo very clear sio kwamba hatuuoni lakini tunajaribu kuonyesha tu utu uzima wetu, WHY?
Wakati huu tuko kwenye vita vikubwa sana vya kuwakosesha usingizi mafisadi, kwa sababu tunajua ukweli wa siasa yetu, kwamba itachukua muda mrefu sana kwa wao kuchukuliwa hatua za kisheria, sasa sio siri kuwa kuna wabunge wa ccm na upinzani, ambao wameamua kushirikiana katika kupigana na kundi la viongozi mafisadi, kwa niaba ya wananchi, jana nilipata bahati ya kuongea na baadhi ya wabunge wa hili kundi wakanihakikishia kuwa do not read too much kwenye media, sisi wenyewe tunajua tunachokifanya,
Kinachosikitisha ni kujua ukweli kwamba kumbe hata viongozi wetu flani wa juu wanawaogopa hawa kundi la mafisadi, tena nweye madaraka makubwa, to the point kwamba in private wanawaunga mkono hawa wapinga ufisadi, lakini in public wanaogopa, sasa tunasema kuwa tunaaangalia silaha tulizonazo katika hivi vita, lakini hatupotezi muda na silaha tusizokuwa nazo,
Sasa inakuja ishu ya Wangwe na Chadema, swali ni je Wangwe yuko wapi kwenye hili la kupigana na ufisadi? Hatupati jibu clear meaning kwamba hatuwezi kumhesabu kuwa yumo kwenye vita hivi muhimu kwa taifa letu la sasa na hasa la baadaye, ndio maana tunakataa kuingilia mambo ya ndani ya Chadema, kwa sababu haya yakipewa nafasi wakati huu, tutapoteza kabisaa muelekeo na kuwapa faida mafisadi ambao since last week wamekuwa wakijaribu sana kuwasogelea kwa karibu wabunge wa kundi la Mwakyembe wakijifanya kuwa ni friends na kuwataka wawasikilize their side of story in private, tunajua kuwa walikuwa na nafasi zote za kwenda kwenye kamati kutoa hizo hadithi zao, lakini walikwepa,
Ninamaliza kwa kusema kuwa sometimes tujifunze ku-practice siasa za kitu-uzima kwa faida ya taifa, na hii ishu inahitaji sana hilo la kujaribu kuwa watu wazima politically, lakini ukweli uko wazi kabisa hapa ya kilichoijiri wala sio siri na Wangwe naye ajifunze kuitumia media kwa faida ya his course kwa sababu hapa unakosekana kabisa ni ukweli wa upande wake, ingawa tunauona lakini ni vyema uwe wake yeye mwenyewe!
Ahsante Wakuu!